Tigo kuna wizi!!!

Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
23
Mambo wanajf??
Kuna wizi mkubwa unafanyika TIGO kitengo cha
tigo pesa!!
Wafanyakazi wa hicho kitengo wanaswap line za wateja wao esp Agents wa tigo pesa na kureset password then wanachukua pesa yote. ukiwasha simu inaonesha
Limited Service!!!

Hii imenitokea mimi mwenyewe Juzi. Angalizo, TIGO inabidi mchukue hatua lasivyo mtaonekana kampuni ya wezi.

Nawasilisha jamvini.
 
Boss haya malalamiko yako ni very serious, unahitajika udhibitisho ili kuichukulia hatua kampuni hii. Kama una ushahidi wa kutosha wafungule mashitaka hawa jamaa. Yaani bongo hii kila mahali ni utapeli...utapeli....utapeli mtindo mmoja.
 
Nina udhibitisho wote ndo nipo kwenye process hadi wahusika wote nimeshawajua!!!

Boss haya malalamiko yako ni very serious, unahitajika udhibitisho ili kuichukulia hatua kampuni hii. Kama una ushahidi wa kutosha wafungule mashitaka hawa jamaa. Yaani bongo hii kila mahali ni utapeli...utapeli....utapeli mtindo mmoja.
 
Wananichosha sana na tabia yao, jana nimeenda kwa agent kutoa pesa yaani huyu kaka amenipa tu kwasababu ananifahamu na uaminifu pia. Bila hivyo ningeenda sehemu nyengine ningejuta nimepewa pesa bila message ya kutoka tigo kumruhusu agent anipe changu.
 
Tunaishi tigo kimazoea tu mkuu...
Swadakta maneno yako, kitengo chao cha huduma kwa wateja ni ziro, mara sita zote nilizowapigia simu kuomba msaada sikufanikiwa. Ukipiga simu lazima iwe mara 3 mpaka nne ndo inaunga, mfumo wao kulinda akaunti ya mteja una walakini. Wanatengeneza line mpya kirahisi mno tena bila uthibitisho muafaka wa mteja. Hiki kikampuni nafikiri kimo mbioni kuuzwa au kufilisika kabisa.
 
HAO TIGO NI WEZI WA KWELI KWELI.
mimi ilinitokea mwaka jana,mwezi wa saba.walihamisha salio lote na kibaya zaidi wakaiharibu na laini yangu ya simu kwa kuifanya isifanye kazi tena.kila ukiwasha simu inakuletea meseji kuwa sim card regstration failled.
nimehangaika weee mpaka kwa mabosi wao lakini ni usanii tu na kupoteza mda wangu ndicho nilichokiambulia. ni wasumbufu sana na hawatoi ushirikiano kama yalivyo makampuni mengine ya simu.
 
hawa jamaa ni hovyo kwa huduma zote i.e tigo pesa,huduma ya simu(wanakata hela hovyo),....ni waongo!
 
Tena wanaboa sana pale wanapokuwa wanakatakata salio kwenye simu bila taarifa,mtu unaweka jelo usiku halafu asb unakuta haipo.
 
Mimi kila siku humu nimekuwa nikirudiarudia kuwataka TCRA waamke, watoke usingizini wawasaidie Watanzania
ambao ndio hugharamia mishahara yao, Tigo wamekuwa ni tatizo kubwa, hata ukiibiwa pesa kwa NMB Mobile halafu
namba iliyotumika iwe ni ya Tigo, hawatoi ushirikiano kwa polisi hata kidogo, wamelewa na hisa za wakubwa.
 
Tigo. Express yourself. Jamani njoon kwenye basi kubwa la Airtel. Tigo ni kwa watoto wa o-level
 
hata bila ku'swap line hawa tigo ni wezi sana, kwenye vocha nako niwezi wakubwa, naungana na feis buku kuwa tunaishi tigo kwa mazoea tu, ndo maana hata neno lenyewe linatafsiliwa kisodoma sodoma tu.
 
Boss haya malalamiko yako ni very serious, unahitajika udhibitisho ili kuichukulia hatua kampuni hii. Kama una ushahidi wa kutosha wafungule mashitaka hawa jamaa. Yaani bongo hii kila mahali ni utapeli...utapeli....utapeli mtindo mmoja.

Mkuu unajua process za mahakama hapa TZ???? Una uhakika mteja atatendewa haki mbele ya haya makampnuni international?? You sound to be not living in TZ!!!
 
Kesi ya nini hapa Bongo?? Nimewabana jamaa wakarudisha pesa yote!!!!!! Tigo ni wezi aiseee!!!

Mkuu unajua process za mahakama hapa TZ???? Una uhakika mteja atatendewa haki mbele ya haya makampnuni international?? You sound to be not living in TZ!!!
 
Mkuu unajua process za mahakama hapa TZ???? Una uhakika mteja atatendewa haki mbele ya haya makampnuni international?? You sound to be not living in TZ!!!

Atatumia gharama mara 100 zaid ya ile aliyoibiwa.
 
Back
Top Bottom