Acheni majungu wakubwa, kwani mafanikio ni lazima aanzishe media? huwezi jua ame invest kwenye sector gani. Hayo ni mambo binafsi acheni umbeaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Tido piga kazi yako uki staafu anza kufanya vitu vyako. Kama utarudi Tanga kuanzisha kilabu cha pombe ya denge au utabaki Dar ufungue genge uwanja wa fisi yote maisha.
Mwanalugali, ninamaanisha fanya comparison ya TBC aliyoikuta Tido na TBC hii ya sasa ya Tido. For the sake of credibility, unapo toa lawama pia unatakiwa kuwe mkweli ili hizo lawama zisigeuzwe chuki binafsi.TBC kabla ya Tido ilikuwa TVT, Tido alipokuja akaikarabati kwa kuigiza KBC, BBC ikawa TBC. Hope umenipata mzee Pasco. Vinginevyo alianzisha ushindani wa chuki dhidi ya ITV na kukumbatia mafisadi!
hv kunani hapo TBC leo asubuhi mtangazaji mmo1 alikuwa akisoma vichwa vya hbr vya magazeti alipofika gazeti la TZ DAIMA akastop fasta na kuanza kusoma hbr za michezo za magazeti mengine.
MWANALUGALI, just be fair, hivi wewe uliijua TBC kabla Tido hajaja, ama umeijua tuu TBC ya Tido na kutaka iwe kama BBC?.Hiyo ndiyo TBC ya Tido Mhando anayotaka Pasco tuipe credits!! Taaluma waliiacha uingereza kwenye BBC na kutuletea ubabaishaji tu hapa!
Uswe, asante kwa hii, MWANALUGALI izingatie hii ili kuepuka kuifanya JF ni kichaka cha wapika majungu!.pia nasikitika sana sana kwamba home of great thinkers imevamiwa, mtu katoa hoja, yumkini hoja yake iko na kasoro mi sina shida na hilo, tatizo wachangiaji, no reasoning, no research watu wanakurupuka tu na kuanza kuponda.
No research, No right to comment!
geek, asante kwa kuliona hili, wakati wa kampeni, kampuni moja ya kutayarisha vipindi vya redio na Televisheni kwa jina la PPR, ilipeleka program kadhaa kwa ajili ya uchaguzi, zile zole zilizoonekana kumpigia JK chapuo kiaina, zilipigwa chini, wakaambia Tido kazigomea kata kata!Sisi wabongo wachoyo wa credit, na hutoa credit kwa mtu asiyestahili. Hivi umeshajiuliza na kukumbuka kabla ya Tido kuwa mkurugenzi wa TBC, enzi hizo TVT ilikuwaje? Nani alikuwa anaangalia hiyo channel?
Huenda kweli Tido ana matatizo yake, lakini siwezi kumkosoa kwa mageuzi makubwa aliyofanya, siyo tu TBC, lakini TV industry ya Tanzania ilikuwa imelala mpaka alipowaamsha usingizini.
Kuhusu kuonekana anapendelea upande fulani, lazima mtambue kuwa kosa siyo lake, bali ni la wanasiasa wa Tanzania ( mfumo wa uendeshaji wa mambo yetu ni mbovu across the board). I can assure you, siku Tido akiondoka pale, mtamkumbuka kuwa at least alikuwa na msimamo wa kufanya kazi zake anavyoona yeye ni sahihi. Sioni mtu mwingine atakuwa na balls za kuwakatalia "wazito" wasiendeshe agenda ya TBC. Tuombe uzima tu.
Wacha weeee! acha kumjaza mwenzio ujinga,sema kweli ili umuokoe,kusema ukweli siwezi kufanya kazi nje kwa miaka yote hiyo nije kuajiriwa tena!wa tz tunauoga wa kujitegemea mbao sijui ni nani atatuondoleaAcheni majungu wakubwa, kwani mafanikio ni lazima aanzishe media? huwezi jua ame invest kwenye sector gani. Hayo ni mambo binafsi acheni umbeaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Tido piga kazi yako uki staafu anza kufanya vitu vyako. Kama utarudi Tanga kuanzisha kilabu cha pombe ya denge au utabaki Dar ufungue genge uwanja wa fisi yote maisha.
Nyerere na serikali yake walituongoza kwa uadilifu na kutufundisha Elimu ya ujamaa na kujitegemea lakini inaelekea katika masomo yao haya walishindwa kabisa! Kwa nini wana taaluma wetu hawakujifunza kujitegemea?
Tido Mhando alifanya kazi BBC kwa mafanikio makubwa, lakini alivyorejea hapa Tanzania alirudi mikono mitupu na kuajiriwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la taifa ambako amejisahau na hajali taaluma yake wala uzoefu aliopata akiwa BBC.
Mwenzake Jeff Koinage WA Kenya alifanya kazi CNN kwa mafanikio lakini aliporejea kwao akaanzisha kituo cha television cha K24 ambacho kinafanya vizuri sana ( kiko kwenye DSTV channel 413) Hiki ni kituo kinachokuza na kuonyesha Taaluma inavyo thaminiwa na kumjenga mtu!
Kwa Tido, vijana wa Tanzania wanajifunza kujipendekeza na kutokuthamini taaluma lakini kwa Koinage, vijana wa Kenya wanajifunza umuhimu wa taaluma na taaluma kuwasaidia kujitegemea!
Nawasilisha kwa mjadala!
Kuna tetesi zisizothibitishwa za ubadhirifu chini ya uongozi wa Tido, ndani ta TBC.Inase,emkana kuna vifaa(spares) hewa zimeagizwa na hazionekani, wakuu wanajikanyaga!
Ahsante sana mkuu, mwanzoni nilihisi kaonewa. Lakini sasa nimeamini kuwa kwa kufananisha na wadhifa liokuwa nao hakupaswa kuishia hapo alipofikia. Tido chukua hiyo kuwa ni changamoto ujipange na sio kufikiria kuajiriwa na EL kwenye ABC Media Group. Muulize Sango kipozi amewezaje na unashindwaje?Nyerere na serikali yake walituongoza kwa uadilifu na kutufundisha Elimu ya ujamaa na kujitegemea lakini inaelekea katika masomo yao haya walishindwa kabisa! Kwa nini wana taaluma wetu hawakujifunza kujitegemea?
Tido Mhando alifanya kazi BBC kwa mafanikio makubwa, lakini alivyorejea hapa Tanzania alirudi mikono mitupu na kuajiriwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la taifa ambako amejisahau na hajali taaluma yake wala uzoefu aliopata akiwa BBC.
Mwenzake Jeff Koinage WA Kenya alifanya kazi CNN kwa mafanikio lakini aliporejea kwao akaanzisha kituo cha television cha K24 ambacho kinafanya vizuri sana ( kiko kwenye DSTV channel 413) Hiki ni kituo kinachokuza na kuonyesha Taaluma inavyo thaminiwa na kumjenga mtu!
Kwa Tido, vijana wa Tanzania wanajifunza kujipendekeza na kutokuthamini taaluma lakini kwa Koinage, vijana wa Kenya wanajifunza umuhimu wa taaluma na taaluma kuwasaidia kujitegemea!
Nawasilisha kwa mjadala!