TICTS Wanaajiri Watu bila kuwaambia Mishahara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TICTS Wanaajiri Watu bila kuwaambia Mishahara?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Jaxx, Apr 22, 2011.

 1. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF kwani nitangulize shukrani zangu kwa ushirikiano weenu wa kila cku, nitakuwa tofauti kidogo na hisia zenu kutokana na heading ila lengo ni moja tu kusaidiana maisha maggumu kama hayo
  Kuna kampuni Inaitwa Lukundo Co. ltd ni agent wa TICTS hapa bandarini kitengo cha uhakiki wa mizigo yani Tallying, Bahati nzuri jamaa (Lukundo) walitangaza kazi za Tallying Clerk nikaomba na nikapata japo pia zoezi lilitawaliwa na Rushwa,chakushangaza na kilichofanya ni post hii thread ni kuwa leo yani tarehe 22/04/2011 tuliambiwa tuanze kazi na mpaka hapo tukawa hatujaambiwa mshahara ila mbaya zaidi mimi nimefukuzwa kazi eti KISA nimeuliza mshahara ni kiasi gani?, hivyo nimepoteza kazi na wote zaidi ya 80 walioajiliwa mpaka sasa wameanza kazi ila hawajaambiwa mshahara ni kiasi gani na hakuna mkataba, eti hili ndilo soko la ajira,Mtu anaeenda kufanya kazi ya kuidhinisha na kukagua mizigo ya Billions of shillins anaanza kazi bila mkataba wala kujua mshahara?, ni hatari sana hivyo TICTS kuweni macho sana na hizi kampuni mnazozipa kazi

  Naomba kuwasilisha!!
   
 2. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana,hiyo kampuni isije ikawa ndio ile washikaji wangu wawili walienda jumapili kwenye usahili,na usahili wenyewe ulikuwa kama wanatafuta watu wakuimba au kuigiza filamu;Washikaji walichoka wakaambiwa mshahara ni 140,000/= inaonekana hao jamaa ni wahuni tu.
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! Sasa ulitakiwa uanze kazi bila kupewa majukumu n.k? Utafanyakazi gani?? Well, labda tujuze uongoze ukoje hapo .... nani alikupa interview, nani alikuambia ukaanze kazi na nani alikufukuza (Majina na vyeo vyao)... Tutawashughulikia tu!
   
 4. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ...jicho kwa hiyo Lukundo Ltd. utakuta ni chakachua ya humo humo ndani.
   
 5. M

  Major JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  mimi jana nilikuwa bandarini nikijaribu kung'ang'ana kutoa kakontena kangu. niliyoyashuhudia ni aibu tupu hata kuyaongelea, ila nilitoka pale saa kumi usiku na sikufaninikiwa kutoa kakontena kangu japo nilikuwa nimeshamaliza utaratibu wote tangu asubuhi, hao waliongia wapya ni sawa na wendawazimu kwa maana hawajui hata kusoma docoment, jana nilichoka mpaka meno. ETI SISI NDIWO TUMEINGIA KTK JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI!!!!!!
   
 6. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi ni ngumu kumjua mtu kwa jina hata kwa cheo mtu anayekufanyia interview, maana tulijengewa mazingira ya nidhamu ya uoga, anyways?,Interview nilifanya Jumamosi iliyopita pale kanisa la Mennonite Upanga na kuhaidiwa kuanza kazi leo na nikaenda nikiwa tayari nimeshapewa kitambulisho na Uniform kwaajili ya kuanza leo hii, kosa nilipouliza mshahara nikatimuliwa kama mbwa
   
 7. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muulize kama alifanyia pale Kanisa la Mennonite Upanga maana ndipo tulfanyia
   
 8. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mm nahisi hivyo maana full mizengwe
   
 9. U

  Uswe JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kha siamini, hata Kilimanjaro Kempiski wanajitahidi
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,852
  Likes Received: 23,468
  Trophy Points: 280
  Heading ya thread yako na ulichokiandika ni tofauti kabisa....Nani mwajiri hapo TICTS au LUKUNDO?
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,852
  Likes Received: 23,468
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri mimi pia nililifuatilia hili suala....

  Mkuu inaelekea hukujua waliotakiwa na LUKUNDO kuwa ni tallying clerks, kazi ambayo elimu itakiwayo ikizidi sana ni kidato cha nne. Kazi ya tallying haihusiani na kukagua wala kuidhinisha mizigo bandarini. Kazi hizo hufanywa na makarani na maafisa wenye sifa stahiki walioajiriwa na TICTS. Kazi hii ya talying ilikuwa ikifanya na kampuni ya Contours Ltd ambao mkataba wao uliisha tarehe 21/04. Vijana waliokuwa Contours asilimia kubwa wamehamia Lukundo. Ni kazi isiyo rasmi, twaweza kuiita vibarua. Ndio maana uliona vijana lukuki pamoja na kutojua mishahara, bado wameigombea kwa wingi na bado wanaendelea kufurika kuigombea. Mkuu kama una digrii yako au hata diploma ya kawaida, hiyo kazi isingekufaa, twaweza sema uliingia msala wa jinsia tofauti.
   
 12. N

  Ngo JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi ni ngumu kumjua mtu kwa jina hata kwa cheo mtu anayekufanyia interview, maana tulijengewa mazingira ya nidhamu ya uoga, anyways?,Interview nilifanya Jumamosi iliyopita pale kanisa la Mennonite Upanga na kuhaidiwa kuanza kazi leo na nikaenda nikiwa tayari nimeshapewa kitambulisho na Uniform kwaajili ya kuanza leo hii, kosa nilipouliza mshahara nikatimuliwa kama mbwa

  Nadhani unayo haki ya kumjuwa mtu anayekufanyia Interview, jina na cheo chake. Unless kama huyo mtu anayekufanyia Interview hajiamini katika kazi yake. Asipojitambulisha jina lake mie namuuliza maana Interview ni two way conversation na inakupa kujiamini ukijuwa unaongea na nani...... haina maana kuwa unavyoenda Interview umeenda mahakamani wewe ni kundunguliwa maswali tu na kujibu... hata huko nako unaweza kumuomba judge kuulza upande mwingine swali. Ni kuacha uoga na kujiamini.

  Sasa unaanza kazi majukumu yako huyajui na mshahara wake pia? Kweli hii ni bongo!
   
 13. D

  Dungu Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli! Nami alikuwa na uzoefu huo katika kazi mahali wangu! Wazo ya cheo ya mtu na mshahara lakini hakuna tatizo kusimamia na kuishi pamoja na hivyo fedha cheo ... Nini Thayer ni kufanya hili .. Demoracry wapi?
   
 14. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vizuri sana japo unaonekana unahucka moja kwa moja na hii Co. achilia mbali zengwe nyingi ulizosema,,,,swala cyo Elimu ,swala ni kwamba nilikubaliwa kufanya kazi na hata kitambulisho nikawa nimepewa regardless of my Education level,,,swali langu ni kwamba je Kibarua HAPASWI KUJUA MSHAHARA WAKE?, WEWE Unaona mm kutimuliwa kwa kuuliza mshahara ni HAKI???, Saidia kujibu hayo
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,852
  Likes Received: 23,468
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo ndipo unapokosea.....kukonkludi bila kuwa na uhakika. Sina maslahi yoyote na wala sihusiki kwa namna yoyote ile na kampuni hiyo. Nilichofanya ni kukusaidia kukufahamisha hali halisi. Nina ndugu zangu wawili ambao Elimu kwao ililazimika kuishia kidato cha nne ambao wanafanya kazi kwenye hiyo kampuni ndio walionipa habari hizi.

  Kama elimu yako ni zaidi ya kidato cha nne nakushauri tena, ile kazi siyo size yako. Wale wenye size yake, mpaka sasa wako kwenye foleni ya kuomba kuajiriwa japo hawajui mshahara ni kiasi gani. Mkuu ulikosea kuingia kwenye choo cha jinsia tofauti kama una elimu yako ambayo inakuwezesha kufanya kazi nyingine na wala si hii ya tallying..... ile tu kuomba kazi ya tallying inaelekea uko katika msako mkubwa wa kazi.....ile kazi mkuu, hata vijana wa darasa la saba wanaifanya, na wako vijana ambao wako happy kuifanya kwa mshahara kiduchu.

  Kukutimua kwa kuulizia mshahara, wamekosea sana.....si haki kabisa. Labda nikuulize, kupewa sare za kufanya kazi na kitambulisho cha muda mfupi ndio tayari ulmeajiriwa? Walikupa barua yoyote au mkataba wa ajira?....Kama walikupa niambie ili nami niwaambie vijana wangu wakaidai....Otherwise mkuu, ulikuwa hujaajiriwa, bali ulichukuliwa kama kibarua.

  Samahani kama nimekukwaza mkuu, lakini habari ndio hiyo....
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,852
  Likes Received: 23,468
  Trophy Points: 280


  Mkuu....interview kwa maana ya interview haikufanyika pale! Unaweza kuinterview watu 400 ili kupata nafasi 180 kwa siku moja? Kilichofanyika pale ilikuwa ni kuwasilisha fotokopi ya vyeti. Wengi, akiwemo ndugu yangu mmoja ameajiriwa kwa cheti cha rafiki yake!! Huwezi kusema ile ilikuwa intavyuu, manake huyu ndugu yangu navyomjua angefanyiwa interview na kuajiriwa, ningeshangaa sana......navyomjua hawezi kufaulu interview ya kazi yoyote ile.....
   
 17. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Miye yangu macho tu hapa hadi kieleweke. Kaka mkubwa nasikia harufu ya manufaa kwa upande wako hapa
   
 18. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure!!!
   
Loading...