Yapi mahusiano ya Adani Group na TICTS huko Bandarini?

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
516
2,881
Serikali na Mamlaka ya Bandari (TPA) iweke wazi kuhusu mahusiano ya Adani Group na TICTS ya Karamagi (Under Hutchinson Port Holding).

Abdul Nondo.

Miezi sita sasa tangu serikali imalize mkataba wake na TICTS Novemba 2022, kutokana na ufanisi mdogo wa uendeshaji wa Magati kadhaa katika Bandari yetu.Tulitarajia mambo haya yawekwe wazi hadi sasa kwamba anayefanya kazi baada ya TICTS Bandarini ni nani na kwa utaratibu gani alipewa kazi hiyo na anafanya kazi gani ,ila hadi sasa hakuna taarifa zozote za wazi kuhusu jambo hili.

Lakini taarifa ambazo tunazo sasa ni kwamba kazi ambayo alikuwa amepewa TICTS (Under Hutchison Port Holding) ya uendeshaji (Operation ) na ukusanyaji wa fedha katika Bandari sasa hivi inafanywa na kampuni ya Adani Group chini ya familia ya Gautam Adani & Rajeshi Adani. Nilimuuliza swali hili katika Clubhouse Msemaji wa
Serikali ndug.Greyson Msigwa Jana tar 01/07/2023 akasema kazi sasa hivi inafanywa na Mamlaka ya Bandari (TPA) na wala Adani Group hayupo .

Moja ya jambo ambalo serikali inapaswa kujiepusha nalo mara zote ni kuficha mambo ambayo baadaye yakishafahamika na umma yanazua mjadala na serikali kutumia nguvu kubwa kutetea na kusafisha . Haya ni mambo ambayo yanahusu Maslahi ya nchi na ufanisi wa kazi inayofanywa katika maeneo kadhaa Bandarini ukilinganisha na kampuni iliyopewa kazi ya Operation sasa na utaratibu uliotumika kutoa hiyo kazi ya Operation.

Kwa taarifa ambazo tunazo sasa ni kwamba Mamlaka ya Bandari sasa hivi inafanya kazi moja tuu ya kukusanya fedha ,ila kazi zote za Operation na uendeshaji zinafanywa na kampuni inayoitwa Adani Group , na Kampuni hii ni ya kidalali haina wafanyakazi wala haina mitambo , kampuni hii inatumia mitambo ya TICTS kufanya kazi na inamlipa TICTS fedha kwa yenyewe kutumia mitambo ya TICTS ,kampuni hii haina wafanyakazi (ManPower ) inatumia wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi chini ya TICTS.Kampuni hii inalipwa na TPA fedha nyingi kwa ajili ya hiyo operation, operation ipi?.Ikiwa kampuni haina vifaa wala wafanyakazi inalipwa kwa kazi gani?.

TICTS alitusumbua kutokana na ufanisi wake mdogo wa ufanyaji kazi tukapiga kelele na kutaka TICTS isiongezewe mkataba , naomba kuuliza hii kampuni ya Adani Group imeleta ufanisi gani kwa miezi hii tangu imeanza kufanya kazi ikiwa inatumia vifaa,mitambo ya TICTS kwa kumlipa TICTS fedha na wafanyakazi wote ni wale waliokuwa chini ya TICTS ni ufanisi gani Taifa na nchi tunaotarajia kuupata kutoka kwa kampuni ya kidalali ya Adani Group? . Kwa jicho la haraka haraka kwanini tusiamini kwamba TICTS ameendelea kufanya kazi Bandarini kwa Mgongo wa Adani Group ? .

Kwa sababu, makubaliano ya mkataba kati ya TICTS ya Karamagi chini ya Hutchison Port Holding na Mamlaka ya Bandari,ni kwamba baada ya TICTS kumaliza mkataba wake vifaa vyote na mitambo vitabaki chini ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa kumlipa TICTS fidia (Compensation) ya fedha .

Ila TICTS hadi sasa haijalipwa fidia yeyote na serikali kupitia Mamlaka ya Bandari kutokana na vifaa na mitambo yake ,alafu wakati huo huo tunaambiwa Adani Group amepewa kazi na TPA kufanya kazi ya Operation kwa kutumia vifaa vya TICTS . Serikali inataka tuamini nini ? . Kwamba TICTS bado anafanya kazi Bandarini kwa mgongo wa dalali Adani Group ? ,au ni Adani Group anamlipa TICTS kwa kutumia mitambo yake ,na fedha ambayo Adani Group anamlipa TICTS anaitoa wapi, ikiwa Adani ni dalali tuu (Broker).Haya mambo yanahitaji uwazi mkubwa ili tujue nini kipo nyuma na kipi kinaendelea.

Utaratibu wa kumpata Adani Group kufanya hiyo kazi ya Operation katika maeneo ambayo TICTS walikuwa wanafanya hiyo kazi ulitumikaje ? , Tenda (Competitive bidding) ya kumpata Adani Group kufanya hiyo operation ilitangazwa lini ? ,walioshindanishwa hadi kumpata Adani Group ni kampuni gani ? . Adani Group anafanya kazi ya Operation kwa muda gani na kwa makubaliano gani? ,kwanini serikali imeficha kuambia umma kuhusu kampuni inayofanya kazi ya Operation baada ya TICTS kumaliza mkataba wake ? .

Ni vyema masuala kama haya serikali iwe inatoa taarifa na kuweka wazi kuliko kuficha,sababu kuficha ficha ndiyo chanzo cha rushwa na ufisadi ,majibu ya serikali katika hili ni muhimu ili watanzania tujue ,tuliokuwa tunapiga kelele juu ya ufanisi mbovu wa TICTS tulitarajia kuambiwa na serikali kwa uwazi juu ya ufanisi wa Kampuni inayofanya kazi sasa baada ya TICTS na kujua makubaliano ya serikali na kampuni hiyo Adani Group ni makubaliano ya namna gani, na kwanini Adani Group anafanya kazi ya Operation kwa vifaa vya TICTS ikiwa tulisema awali vifaa vya TICTS na mitambo havina ufanisi ,huyu Adani Group analipwa na TPA kwa kazi gani hasa anayoifanya ikiwa hana vifaa wala wafanyakazi? .

Haya mambo tuna hoji ni kwa upendo wa dhati kwa nchi yetu ,Kwa Maslahi ya nchi yetu ili rasilimali zetu tuliyojaaliwa na Mungu zinufaishe Taifa letu.Ili Dhamira ya dhati ya kuleta Maendeleo itimie kupitia manufaa ya rasilimali zetu.

Ahsante.

Abdul Omary Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana.
ACT Wazalendo Taifa .
Tar 02/07/2023.
Kilwa-Kivinje (Lindi).
 
Michongo ya kipigaji hii inaendelea. Adani nimedananisha na akina Yogesh maneki hawa ndio wamiliki wa Gapco. Wahindi wote waliokuwepo Tanzania wamekuja kutafuta fedha hakuna mitambo watanunua wala chochote.

Na wengi hawafahamu kwamba Karamagi alikuwa ni frontman mwenye hisa kadhaa lakinj baadae Muajemi wa caspian ndio alikuwa bigmba behind the curtain kwenye hicho kinachoitwa Ticts a franchise of Hutchison of Hongkong.

Hata hii DP world its either Muajemi is behind it, Na juzi juzi ameonekana Joho wa mombasa hapa mjini nadhani anawexekanza ndiye aliye broker hii deal ya DP world kupitia kina wamiliki wa timu ya wananchi.

Kwanini Public procurement principles hazifuatwi. Tunashangaa tunaona ma mercedez g wagon yanajaa mjini kumbe hela zetu za mikopo world bank watu wanazisigina.
 
Serikali na Mamlaka ya Bandari (TPA) iweke wazi kuhusu mahusiano ya Adani Group na TICTS ya Karamagi (Under Hutchinson Port Holding).

Abdul Nondo.

Miezi sita sasa tangu serikali imalize mkataba wake na TICTS Novemba 2022, kutokana na ufanisi mdogo wa uendeshaji wa Magati kadhaa katika Bandari yetu.Tulitarajia mambo haya yawekwe wazi hadi sasa kwamba anayefanya kazi baada ya TICTS Bandarini ni nani na kwa utaratibu gani alipewa kazi hiyo na anafanya kazi gani ,ila hadi sasa hakuna taarifa zozote za wazi kuhusu jambo hili.

Lakini taarifa ambazo tunazo sasa ni kwamba kazi ambayo alikuwa amepewa TICTS (Under Hutchison Port Holding) ya uendeshaji (Operation ) na ukusanyaji wa fedha katika Bandari sasa hivi inafanywa na kampuni ya Adani Group chini ya familia ya Gautam Adani & Rajeshi Adani. Nilimuuliza swali hili katika Clubhouse Msemaji wa
Serikali ndug.Greyson Msigwa Jana tar 01/07/2023 akasema kazi sasa hivi inafanywa na Mamlaka ya Bandari (TPA) na wala Adani Group hayupo .

Moja ya jambo ambalo serikali inapaswa kujiepusha nalo mara zote ni kuficha mambo ambayo baadaye yakishafahamika na umma yanazua mjadala na serikali kutumia nguvu kubwa kutetea na kusafisha . Haya ni mambo ambayo yanahusu Maslahi ya nchi na ufanisi wa kazi inayofanywa katika maeneo kadhaa Bandarini ukilinganisha na kampuni iliyopewa kazi ya Operation sasa na utaratibu uliotumika kutoa hiyo kazi ya Operation.

Kwa taarifa ambazo tunazo sasa ni kwamba Mamlaka ya Bandari sasa hivi inafanya kazi moja tuu ya kukusanya fedha ,ila kazi zote za Operation na uendeshaji zinafanywa na kampuni inayoitwa Adani Group , na Kampuni hii ni ya kidalali haina wafanyakazi wala haina mitambo , kampuni hii inatumia mitambo ya TICTS kufanya kazi na inamlipa TICTS fedha kwa yenyewe kutumia mitambo ya TICTS ,kampuni hii haina wafanyakazi (ManPower ) inatumia wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi chini ya TICTS.Kampuni hii inalipwa na TPA fedha nyingi kwa ajili ya hiyo operation, operation ipi?.Ikiwa kampuni haina vifaa wala wafanyakazi inalipwa kwa kazi gani?.

TICTS alitusumbua kutokana na ufanisi wake mdogo wa ufanyaji kazi tukapiga kelele na kutaka TICTS isiongezewe mkataba , naomba kuuliza hii kampuni ya Adani Group imeleta ufanisi gani kwa miezi hii tangu imeanza kufanya kazi ikiwa inatumia vifaa,mitambo ya TICTS kwa kumlipa TICTS fedha na wafanyakazi wote ni wale waliokuwa chini ya TICTS ni ufanisi gani Taifa na nchi tunaotarajia kuupata kutoka kwa kampuni ya kidalali ya Adani Group? . Kwa jicho la haraka haraka kwanini tusiamini kwamba TICTS ameendelea kufanya kazi Bandarini kwa Mgongo wa Adani Group ? .

Kwa sababu, makubaliano ya mkataba kati ya TICTS ya Karamagi chini ya Hutchison Port Holding na Mamlaka ya Bandari,ni kwamba baada ya TICTS kumaliza mkataba wake vifaa vyote na mitambo vitabaki chini ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa kumlipa TICTS fidia (Compensation) ya fedha .

Ila TICTS hadi sasa haijalipwa fidia yeyote na serikali kupitia Mamlaka ya Bandari kutokana na vifaa na mitambo yake ,alafu wakati huo huo tunaambiwa Adani Group amepewa kazi na TPA kufanya kazi ya Operation kwa kutumia vifaa vya TICTS . Serikali inataka tuamini nini ? . Kwamba TICTS bado anafanya kazi Bandarini kwa mgongo wa dalali Adani Group ? ,au ni Adani Group anamlipa TICTS kwa kutumia mitambo yake ,na fedha ambayo Adani Group anamlipa TICTS anaitoa wapi, ikiwa Adani ni dalali tuu (Broker).Haya mambo yanahitaji uwazi mkubwa ili tujue nini kipo nyuma na kipi kinaendelea.

Utaratibu wa kumpata Adani Group kufanya hiyo kazi ya Operation katika maeneo ambayo TICTS walikuwa wanafanya hiyo kazi ulitumikaje ? , Tenda (Competitive bidding) ya kumpata Adani Group kufanya hiyo operation ilitangazwa lini ? ,walioshindanishwa hadi kumpata Adani Group ni kampuni gani ? . Adani Group anafanya kazi ya Operation kwa muda gani na kwa makubaliano gani? ,kwanini serikali imeficha kuambia umma kuhusu kampuni inayofanya kazi ya Operation baada ya TICTS kumaliza mkataba wake ? .

Ni vyema masuala kama haya serikali iwe inatoa taarifa na kuweka wazi kuliko kuficha,sababu kuficha ficha ndiyo chanzo cha rushwa na ufisadi ,majibu ya serikali katika hili ni muhimu ili watanzania tujue ,tuliokuwa tunapiga kelele juu ya ufanisi mbovu wa TICTS tulitarajia kuambiwa na serikali kwa uwazi juu ya ufanisi wa Kampuni inayofanya kazi sasa baada ya TICTS na kujua makubaliano ya serikali na kampuni hiyo Adani Group ni makubaliano ya namna gani, na kwanini Adani Group anafanya kazi ya Operation kwa vifaa vya TICTS ikiwa tulisema awali vifaa vya TICTS na mitambo havina ufanisi ,huyu Adani Group analipwa na TPA kwa kazi gani hasa anayoifanya ikiwa hana vifaa wala wafanyakazi? .

Haya mambo tuna hoji ni kwa upendo wa dhati kwa nchi yetu ,Kwa Maslahi ya nchi yetu ili rasilimali zetu tuliyojaaliwa na Mungu zinufaishe Taifa letu.Ili Dhamira ya dhati ya kuleta Maendeleo itimie kupitia manufaa ya rasilimali zetu.

Ahsante.

Abdul Omary Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana.
ACT Wazalendo Taifa .
Tar 02/07/2023.
Kilwa-Kivinje (Lindi).
Kwani bro Zzk anasemaje .?
 
Back
Top Bottom