Tibaijuka: Muleba hawana shida ya mafuta ya taa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaujuka amefunguka na kusema kuwa watu wa jimbo lake la Muleba hawana matatizo ya mafuta ya taa bali matatizo makubwa walionayo wao ni magari yao kuharibika kutokana na mafuta aina ya diesel kuchakachuliwa.
Tibaijuka.jpg

Tibaijuka alisema hayo bungeni baada ya kupewa taarifa na Mbunge wa Mbozi (CHADEMA), Pascal Haonga ambaye alikuwa anamwambia Tibaijuka kuwa hata wananchi wake Muleba hawataweza kununua mafuta ya taa kutokana na bei hiyo mpya kwamba itakuwa kubwa sana na kumtaka kurekebisha kauli yake, jambo ambalo Tibaijuka alilikataa na kusema jimboni kwake yeye anapigania magari ya watu yasiharibike.

"Taarifa nimeikataa kwa sababu kule kwangu sisi shida yetu ni magari yasiharibike, engine zisiharibike, kwa hiyo ngoja niwaambie mimi ndiyo nawakilisha watu wangu wa Muleba, matatizo yetu ni disel hata viwanda kama Kagera Sugar karibu kisimame kwa sababu disel inakuwa imechakachuliwa, hivyo uchakachuaji ni mkubwa. Kwa hiyo mafuta ya petroleum ilivyokaa kwenye bajeti ni sawa kabisa" alisema Tibaijuka
 

kiduni

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
256
250
Wanatukataza tusitumie kuni na mkaa gesi inauzwa bei kubwa na bei ya unit za umeme iko juu mafuta ya taa nayo wanataka yapande bei aisee acha tuharibu misitu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom