Tibaijuka awatisha Malecela, Sumaye; AONYA MUDA WAO KUHODHI ARDHI KUBWA UMEKWISHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tibaijuka awatisha Malecela, Sumaye; AONYA MUDA WAO KUHODHI ARDHI KUBWA UMEKWISHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 16 August 2011 23:34

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]AONYA MUDA WAO KUHODHI ARDHI KUBWA UMEKWISHA

  Waandishi wetu, Dodoma, Dar

  LICHA ya kupata wakati mgumu Bungeni, Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imepitishwa jana huku Waziri wake, Profesa Anna Tibaijuka akitoa onyo kwa wanaohodhi ardhi kwa muda mrefu bila kuiendeleza akisema: "Fungate yao imekwisha."

  Kauli hiyo ya Profesa Tibaijuka imekuja siku moja baada ya kambi ya upinzani bungeni kupitia Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kutaja orodha ndefu ya vigogo hao wa CCM wakiwamo Marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Mawaziri Wakuu wastaafu, John Malecela na Frederick Sumaye.

  Wengine waliotajwa ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula na aliyekuwa Naibu wake (Bara), Hassan Ngwilizi akisema kwamba wamehodhi ardhi kubwa mkoani Morogoro bila kuiendeleza. Hata hivyo, alisema ni Mkapa pekee aliyeendeleza eneo lake.

  Mwingine aliyetajwa na Mdee ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mulla.Akijibu hoja hiyo na nyingine bungeni jana Profesa Tibaijuka, kwa kifupi alisema kwa wamiliki wote wa ardhi ambayo haijaendelezwa: "Honeymoon is over" (fungate imekwisha) na kwamba wizara yake itapitia miliki za mashamba na maeneo mengine yasiyoendelezwa kisha kuchukua hatua stahili.

  "Wizara yangu itafanyia ukaguzi maeneo haya ya ardhi, hivyo wanaomiliki mashamba ambayo bado hayajaendelezwa basi wajue kwamba "honeymoon is over."

  Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema) katika hoja hiyo, alisema vigogo hao wanahodhi maeneo makubwa ya ardhi huku wananchi hasa wale waishio jirani nayo wakikosa ardhi hali ambayo aliita ni hatari kwa amani ya nchi.

  Bila kuwataja kwa majina vigogo hao kwa majina kama alivyofanya waziri kivuli, Profesa Tibaijuka pia alisema kwamba hata wale ambao wamemilikishwa ardhi na kuamua kuikodisha kwa wananchi na kuwatoza kodi, watashughulikiwa.

  Pinda aingilia kati
  Kabla ya Waziri Tibaijuka kujibu hoja za wabunge, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alizungumza na kueleza kuwa mgogoro wa ardhi ambao umekuwa ukipigiwa kelele na Watanzania kuhusu shamba la Katumba, anaufahamu na kwamba upo kwa maslahi ya wananchi wa maeneo hayo.

  Alisema Shamba la Katumba halina mgogoro, bali wanaopiga kelele ni watu wanaotoka mbali na maeneo kwani hawajui msingi wa mkataba huo.

  "Waheshimiwa wabunge, eneo la Katumba liko jimboni mwangu na mara nyingi watu wanapopiga kelele hapa siwaelewi na siko tayari kukubaliana nao, nitaufia msimamo wangu kuhusu eneo lile,'' alisema na kuongeza:

  "Kama kuna kitu ambacho lazima wenzetu wakubali ni pamoja na kuwa mikoa ya pembezoni ilikuwa nyumba sana licha ya kuwa sisi ndiyo tunaolisha Tanzania nzima. Sasa hatukubali."

  Alisema bado mwekezaji hajapewa idhini ya kumiliki kama ambavyo wengi wamekuwa wakieneza na badala akasema ni makubaliano ya awali tu ndiyo yaliyofanyika ambayo yatakwenda hatua nyingine tena kwa kushirikisha vyombo husika.

  Alieleza kusikitishwa kwake na jinsi baadhi ya watu wanavyojia juu hatua hiyo ya kuwekeza katika shamba hilo na maeneo ya pembezoni jambo ambalo pia linafanyika katika maeneo mengine ya nchi.Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, Pinda alikiri kuwa ipo kutokana na wananchi wengi kuhitaji ardhi na akasema jambo hilo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini.

  Hata hivyo, licha ya kumsifia Profesa Tibaijuka, aliwataka mawaziri pia kuwa na meno kwa watendaji wao kuliko kuendelea kulalamika kila siku.

  "Nataka kuwaambia mawaziri wote kuwa acheni kunung'unika juu ya watendaji wabovu, nendeni mkafoke ikibidi watimueni halafu mambo mengine yatafuata ili mradi mfuate taratibu na sheria za kutomuonea mtu,'' alisema.

  Michango ya wabunge
  Wabunge wengi waliochangia mjadala wa hotuba hiyo walituhumu baadhi ya mambo ikiwamo rushwa katika sekta ya ardhi nchini na kuonyesha kuchukizwa kwao na ufisadi unaotikisa sekta hiyo kwa kuhusisha maofisa ardhi, kuchelewa kesi mahakamani zinazohusu migogoro ya ardhi na bajeti finyu ambayo ya Sh47.89 bilioni ambayo walisema haiwezi kuleta tija katika mabaraza ya ardhi.
  Mdee aonya machafuko kugombea ardhi

  Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliitahadharisha Serikali kuwa kuipuuza sekta ya ardhi kutasababisha watu wa taifa hili kuchinjana."Sekta ya ardhi ndiyo uhai wa nchi hii. Sekta hii tukiipuuza... na ninaiambia Serikali tukiipuuza watoto wetu, wajukuu wetu watakuja kuchinjana na hatutaki kutengeneza Tanzania ya kuchinjana katika kipindi," alisema Mdee.

  Akizungumzia kuhusiana na Kampuni ya Agri Soil ambayo imepewa eneo la uwekezaji katika Wilaya ya Mpanda, Mdee alisema mbali na upungufu wake imekiuka sheria."Imekiuka sheria ya nchi, sheria zetu zote ziko wazi na hili namwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu asiposhughulikia vizuri anaweza akaanguka nalo kabisa kwa sababu kuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa ofisi yake ilihusika tutumie busara tuokoe nchi," alisema.

  Mdee alisema sheria inasema kama kuna ushirikiano unamhusu raia na kwamba sheria ya uraia haijatambua halmashauri na kuhoji kuwa Serikali iwaambie wabunge ni raia gani anamiliki hekta zaidi ya 200?

  Mgogoro wa shamba hilo uliibukia kwa mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Pudenciana Kikwembe ambaye aliitaka serikali kutoa asilimia 25 ya hisa katika shamba hilo kwa wazawa na kwa sababu madiwani walishirikishwa katika suala la Agro Soil basi waamue gawio la faida litakwenda katika mradi gani.

  Mbunge wa Nkenge (CCM), Assumpta Mshama alilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwachukulia hatua watu waliojilimbikizia ardhi pasipo kufanyia shughuli za maendeleo.

  "Naiomba wizara ichukue maoni kwa wananchi kujua ni kwa namna gani wanafaidika na hao wanaojiita wawekezaji waliopewa sehemu kubwa ya ardhi kuliko kuwaachia watu wasiowanufaisha wananchi husika."

  Mshama aliwataka mahakimu wasiendeshe kesi za migogoro ya ardhi kwa muda mrefu ili kuwapatia hati stahiki walalamikaji kwa muda muafaka kwa ajili ya kujiletea maendeleo kiuchumi.

  Mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Jitu Soni alisema jimbo lake limekumbwa na mgogoro wa Bonde la Mto Kilwa kwa zaidi ya miaka 25 bila usuluhishi wowote."Tume mbalimbali zimekuwa zikiundwa kujadili tatizo hili, lakini kwa kipindi chote hicho zinakuja na majibu yasiyo na muafaka wa tatizo," alisema.

  Mbunge huyo alitoa pendekezo kwamba, ili kupunguza matabaka na umaskini uliokithiri kwa wananchi wengi ni vizuri kila mwananchi anayemiliki ardhi apimiwe eneo lake na apewe hati miliki."Endapo suluhisho la matatizo haya ya ardhi litafanikiwa, utabaka utatoweka na hali ya umaskini itapungua. Watu wanahitaji ardhi kwa ajili ya kujijenga kiuchumi ili waishi vizuri kwa amani hivyo basi, ni vizuri kama kutakuwa na ardhi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo na makazi."

  Mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Philipo alisema asilimia 90 ya kero za wananchi wa jimboni kwake ni migogoro ya ardhi ambayo imesababishwa na wawekezaji wakubwa ambao mikataba yao ilishakwisha malizika siku nyingi bila kufanyiwa ufuatiliaji.

  "Naomba wizara ishughulikie mikataba iliyoweka na wawekezaji wakubwa ambayo mingi imeonekana kuisha siku zake, lakini maeneo hayarudishwi kwa wananchi kwa ajili ya kuwanufaisha badala yake wamekuwa wakinyanyasika."

  Alipendekeza kwamba halmashauri ziwezeshwe kwa kupewa vifaa vya upimaji jambo ambalo litawasaidia wananchi kutumia ardhi zao kuchukua mikopo itakayowasaidia kujiletea maendeleo.

  Kwa upande wake Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere kutokana na ufinyu wa bajeti katika wizara hiyo, alimtaka waziri Tibaijuka ajiuzulu wadhifa wake kwa kumwambia Rais ameshindwa kufanya kazi.

  "Siungi mkono hoja na naomba Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi uende kwa Rais kumwambia umeshindwa kazi kutokana na fungu kuwa dogo, kama huwezi mimi nitakusaidia," alisema.

  Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse aliitaka Serikali ijilize migogoro ya ardhi inasababishwa na nini? Kwa mtazamo wake, tatizo hilo linatokana na mfumo mbovu uwekezaji na mamlaka iliyopewa dhamana haitendi kazi ipasavyo.

  Alizitaka Wizara za Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Kilimo, Chakula na Ushirika na Maliasili na Utalii kukutana kwa ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya ardhi kwa wakulima, wafugaji na wananchi wa kawaida.

  Mbunge wa Ilemela kwa tiketi ya Chadema, Ezekia Wenje aliwashutumu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza kwa kujimilikisha eneo kubwa la ardhi maeneo ya Luchelele kutoka kwa wananchi wa hali ya chini bila kuwapa fidia stahili.

  Naye Susan Kiwanga (Viti maalumu, Chadema), alimshutumu Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akisema amejimilikisha eneo la ardhi linalofikia hekari 300 huko Morogoro huku akijisifia kuwa amewalipa kiasi kidogo cha fedha.

  "Inasikitisha sana kuona watu tuliopewa dhamana kutetea haki za wananchi ndiyo tunaongoza kwa kuwanyanyasa. Kwa mfano, Mbunge wa Kisesa ameamua kuja kujimilikisha hekari 300 kutoka kwa wananchi wa hali ya chini huku akijisifia. Ina maana ardhi huko Mwanza imekwisha?''

  Mbali na hilo, Kiwanga alisema migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na rushwa iliyotawala miongoni mwa watendaji lakini pia huku akielezea kushangazwa kwake na kauli ya wizara kwamba ni asilimia moja tu ya ardhi nchi nzima iliyopimwa.

  Imeandikwa na Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma na Furaha Maugo, Dar.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Kwanini Sasa Marais Wanajilimbikizia Ardhi -- Wakati wa Nyerere hakufanya ulafi huo?


  1. Mzee Mwinyi! Ana Mtoto Waziri kwa zaidi ya Miaka 10
  Ana Mtoto Mbunge wa Afrika ya Mashariki kwa Miaka 6
  Pesa ya Walipa kodi wa Tanganyika na Zanzibar inamtunza mpaka Afe, Ulinzi anao Usafiri wa Uhakika anao hadi kwenda nchi za nje kwa Fedha za Serikali Ana Wake Wawili na watoto wote wamefanikiwa kimaisha.
  WHEN R THEY GOING 2 SAY ENOUGH IS ENOUGH? HIZO ARDHI NI NYINGI HADI WANASHINDWA KUZIENDELEZA.
  YEYE NI MZANZIBARI NA ANAJUA WABARA HAWAWEZI KUPATA ARDHI ZANZIBAR.


  2. MZEE MKAPA! UZURI watoto wake hawako kwenye Ulafi wa Serikali
  Alijipa KIWIRA COAL MINES, Mkewe ana vitega uchumi kibao; Pesa za kodi zinawatunza mpaka wafe
  BADO ana KAZI NZURI UNCTAD; Unapokea $$$, Bado kukimbilia Mashamba na ulafi unashindwa kuyaendeleza yote tamaa Ardhi mmejigawia wananchi wa maeneo hayo wanalia njaa.


  3. MZEE MALECELA! Umeshika Uongozi wewe na Kaka yako toka Uhuru; Madaraka Mbalimbali, watoto kibao wote Wamesomeshwa na serikali ya nchi hii hadi Elimu ya Juu; Watoto wanakazi nzuri ndani na nje ya nchi, Mikataba mingi na miradi mingi 10% na bado serikali na walipa kodi wa nchi wanakutunza kuangalia Afya yako ukapelekwa India na UK n.k

  Bado kuparamia Ardhi za Wananchi na unajilimbikizia hauna hata uwezo wa kuendeleza HAYO MASHAMBA.Ni ULAFI WAKATI WA NYERERE HAKUNA ALIKUFURU KAMA SASA. NA WOTE MLIJIFANYA VIONGOZI MAIRI MSIOTAKA KUJILIMBIKIZIA MALI TOKA KWA WANANCHI!!


  PLEASE OUR LEADERS DON'T GAIN THE WORLD and LOSE YOUR SOUL, WISDOM is BETTER THAN SILVER or GOLD!!!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwa bahati mbaya sio anachoweza kufanya mama tibaijuka

  kama anaweza aanze na yule burushi mwenye eka laki moja na ushee kigamboni wakati wanachi hawana pa kuhamia kupisha upanuzi wa mji
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watu toka Tanzania Bara hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar, lakini wao Wanzanzibari wanamiliki ardhi huku Tanzania bara. Pengine si vizuri hili swali likaulizwa bungeni ili kuweka mambo hadharani.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  NI porojo tu for sure hakuna kitakachofanyika
   
 6. R

  Raila Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tumpe muda, ametuahidi mwenyewe
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Hatutaki vitisho nchi hii tunataka vitendo zaidi kwani ndio vinatisha kuliko haya maneno ya kimipasho ya mawaziri.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  hizi ni toi toi geresha tu.....................
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Open space vipi.... muda haujaanza?
   
 10. Suip

  Suip JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,039
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Haya ndio matokeo ya kukataa AZIMIO LA ARUSHA sasa mnalalamika nini,
   
 11. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  huyo alikuwa anapiga kelele tu hakuna lolote atalifanya
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  gamba halivuk uchafu mwing had kinyaa,kila mtawala ccmagamba mkimguza ananuka wizi wa mali za umma.oh Tz mabomu haya yalipuka usalama je?hv baada humu JF yana ushabik na ccmagamba du aibu yao!
   
 13. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ataweza wapi huyu binti. Kwanza Tanzania yenyewe haijui ipasavyo. Muda mwingi alikuwa nje ya nchi !
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  hizi ni poorojo tuu
  kuna alilolifanya toka aingie madarakani
  nchi hii ahadi ni nyingi kuliko vitendo
  ataahidi na budget ijayo bado ataahidi tena na tena
   
 15. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  propaganda tu hizo hawezi kuwafanya chochote jamani
   
 16. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu tujaribu kuwa wakweli,huyu mama haiwezi hii wizara atabaki kupiga porojo tu then muda utakwisha.
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  ................Nilijaribu kuangalia hotuba ya huyu mama kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake,pamoja na kumsikiliza hakijumuisha hotuba yake na zaidi wakati akijibu hoja za wabunge wakati bunge limekaa kama kamati ya matumizi..Niwe wazi na nadhani kama kuna mtu alitazama anaweza kuniunga mkono..
  1. Huyu mama anaonekana haijui hii wizara vyema na hana majibu sahihi kwa hoja zenye mshiko
  2. Huyu mama pamoja na U-prof wake na uzoefu wa kazi katika nyanja ya makazi tena kimataifa hajui kujenga hoja na kujipanga kutengeneza hoja zenye tija.
  3. Huyu mama anaongea bila kuwa na taarifa za kuhusu hali ya nchi yetu...hajui mafisadi wameishika na bosi wake ni mmoja anaewalinda...
  4. Huyu mama nahisi ni mtendaji na sio kiongozi...anafaa sana kazi kama katibu mkuu nk..na sio uwaziri....
  Otherwise...sitegemei jipya kutoka kwake,zaidi nategemea hii wizara kufa kabisa...
   
 18. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Mzee umesahau ma-hecta ya ardhi anayomiliki MKAPA huko LUSHOTO. Kwa uzoefu wangu binafsi hakuna sehemu zenye uhaba wa ardhi kama maeneo ya milima ya USAMBARA na maeneo ya kuzunguka mlima KILIMANJARO. Kitendo cha MKAPA kujimilikisha sehemu kubwa ya ardhi ya WASAMBAA tena akiwa angali rais ni aibu kubwa mno kwa kiongozi wa nchi changa kama Tanzania.
   
 19. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hii, "Wizara yangu itafanyia ukaguzi maeneo haya ya ardhi, hivyo wanaomiliki mashamba ambayo bado hayajaendelezwa basi wajue kwamba "honeymoon is over."
  Basi tumpe muda huyu mama, kama atashindwa tutamuomba akalime Muleba, ila na yeye ana eneo kubwa sana huko Kyamyorwa Muleba anapakana na Msitu wa Hifadhi wa Biharamulo alikuwa hajaliendeleza by 2007 nilipokuwa huko wanaofhamu juu ya hilo eneo watufahamishe zaidi.
   
 20. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hii, “Wizara yangu itafanyia ukaguzi maeneo haya ya ardhi, hivyo wanaomiliki mashamba ambayo bado hayajaendelezwa basi wajue kwamba “honeymoon is over."
  Basi tumpe muda huyu mama, kama atashindwa tutamuomba akalime Muleba, ila na yeye ana eneo kubwa sana huko Kyamyorwa Muleba anapakana na Msitu wa Hifadhi wa Biharamulo alikuwa hajaliendeleza by 2007 nilipokuwa huko wanaofhamu juu ya hilo eneo watufahamishe zaidi.
   
Loading...