Tiba za viongozi wa kitaifa ng'ambo sasa ni mzigo mkubwa kwa wavuja jasho................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba za viongozi wa kitaifa ng'ambo sasa ni mzigo mkubwa kwa wavuja jasho................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Mar 5, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Nionavyo mimi afya za viongozi wengi hapa nchini zina mushkeli mkubwa na matokeo yake mabwanyenye hawa hukimbizwa nje ya nchi badala ya kutibiwa hapa nchini. Gharama za kutibu viongozi hawa sasa ni mzigo mkubwa kwa taifa na sioni dalili ya kupungua bali kuongezeka. Sehemu kubwa ya matumizi haya wala hayana kibali cha bunge. pendekezo langu ni kuwa kuna uhaja wa kuwashinikiza wabunge kufuta kabisa kasma ya matibabu nje na yeyote anayetaka kutibiwa nje atoe pesa mfukoni kwake. Hii pia itaongeza kasi kwa watunga sera kuimarisha huduma za afya hapa nchini badala ya kuimarisha mfuko wa kuwapeleka nje kwa matibabu..............

  Viongozi wengi magonjwa yao hayana tiba lakini kwa sababu ya ubinafsi wao hawako tayari kukubali ya kuwa safari zao hapa duniani zimefikia ukingoni na hivyo kuendelea kutubebesha mzigo wa kuwahudumia nje ya nchi. Mimi huwasifu Cuba ya kuwa pamoja na umasikini wao ni marufuku kwa serikali kugharimia matibabu ya kiongozi au raia yoyote nje ya nchi matokeo yake Cuba ina huduma bora za tiba hapa duniani ambazo hazina ubaguzi wowote huhusani wa kipato au cheo............
   
 2. K

  Kiraka Timothy Peter Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli wazo hili lina kila sababu ya kuungwa mkono na yeyote mwenye upeo wa kupambanua mambo..Viongozi wetu wanafahamu fika uduni wa huduma zetu za afya hapa nchini.,wanafahamu mazingira mabovu ya wodi tulizo nazo,upungufu wa vitendea kazi na uhaba wa wahudumu.Lakini badala ya kutumia nafasi na ushawishi walio nao kupandisha hadhi ya sekta ya afya,wanangoja waanze kukohoa wapande ndege kwenda ulaya,tena wao na wakati mwingine familia zao na watu wao wa karibu..Tunakifahamu bayana kisingizio chao.,daima wanatumia utaratibu uleule kuwa mfanyakazi anapougua anapaswa kuhudumiwa na mwajiri wake.Nakubaliana na hili kwa zaidi ya 100%,lakini nawakumbusha tu kuwa wao ni waajiriwa wa serikali,na serikali ni wananchi.,kumbe sisi ndio waajiri wao,ama wakubali kwa busara zao ama wapinge kwa ufinyu wa fikra walizo nazo..Rai zangu ni tatu.,
  Mosi,kila kiongozi atumie gharama binafsi katika safari za matibabu yake nje ya nchi kama kwa utashi na mtazamo wake,ndugu zake au majirani na marafiki wanaona na wamethibitisha kuwa huduma za anapokwenda zina tija kuliko za hapa nchini..
  Pili,bunge liwe na sauti ya kupinga au kuruhusu safari za kila kiongozi au viongozi kwenda nje ya nchi wakitathmini tija ya safari hizo..
  Tatu,sisi wananchi tulio waajiri wa viongozi wetu tuwe na utaratibu wa kuhoji na kupinga matumizi ya kodi tunazotoa kwa kutaka ama kutokutaka ili zitumike vema kutuletea maendeleo,sio kunufaisha wachache wasio na nia kweli ya kutusaidia..Kodi zetu ziboreshe sekta za elimu,afya,miundombinu na kilimo ili tusonge mbele..
   
 3. kiagata

  kiagata Senior Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  madaktari wa Tanzania wajifunze uzalendo kutoka Cuba,Iraq,Somalia kwa hiari ya kufanya kazi bila kipato kikubwa kwa nia ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huwezi kuwa mzalendo wakati unanyonywa,kukiwa na usawa mtu anaweza kuwa mzalendo.
  Mtu anapewa mshahara ambao haukidhi ata mahitaji ya msingi na mbaya zaidi wakati unaishi maisha duni wenzio wanaishi kama Mbinguni.Dont expect true patriotism apo from the exploited citizen.
  Na hawa viongozi wanaenda nje bse hawataki boresha hospital za ndani ili kuokoa hela
   
 5. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nafikiri UZALENDO wangeanza WANASIASA..!!

   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Tujifunze kutoka kwa wacuba........hata comandoo Chavez Hugo naye amekiri kwa kwenda kutibiwa kule badala ya majuu...........
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  hayo mabilioni yanayotumika kutibu viongoziu ulaya yatumike kwa kulipa madaktari na kuimarisha huduma za afya hapa nchini kama kujenga zahanati vijijini na hospitali za rufaa kila mkoa ambazo kweli zinaweza kutoa huduma zote bila zengwe.........................acha kutetea ubadhirifu weye..........
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Njowepo
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,090
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  marazi wanayapata kwenye anasa zao,
  kodi zetu ndizo zinawatibia, lol.
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  viongozi wanapaswa kuonyesha njia badala ya kumungunya maneno matamu ya kuwashawishi wavuja jasho wakaza mkanda kumbe wao ni kuku kwa mrija............
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  na hili linasikitisha sana mtu anaendekeza ngono na kula kupita kiasi bila ya kipimo khalafu sisi kazi yetu ni kumtibu ng'ambo badala ya kutumia vijisenti vyetu kuimarisha huduma za afya hapa nchini.......lol.........kweli sisi ndiyo wajinga tuliwao..........
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Serikali ya Cuba inagharamia vifaa, Je Serikali ya Majua itaweza kununua vifaa. Kodi yetu wanaochukuwa kwenda kujitibia wao ni bora wangeitumia kununulia vifaa ili tukanufaika sote kuliko kutunyonya. Mimi huwa naomba kila siku Kiongozi au viongozi wowote wanokwenda kutibiwa nje wafie huko huko wakirudishwa wazikwe. Pumbavu zao wanafuja tu Kodi zetu kwa upumbavu wao
   
 13. k

  katitu JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  rasimu ya katiba inakuja ni wakati mzuri sasa wa kuyaweka mambo haya vizuri.pendekezeni hakuna wakubwa kupelekwa nje kwa matibabu labda kwa fedha zao ili nao wapate adha tunazozipata sisi walalahoi ndipo watakapotambua umuhimu wa madaktari wetu wa hapa bongo
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Haiwezekani kwa wabunge kupitisha sheria itakayowataka wajilipie matibabu ya nje ya nchi kwasababu hao hao wabunge ndio wanaofaidika na mpango wa kwenda kutibiwa Apollo; wengine hata wanawapeleka wake zao kulea mimba zao [be-rest] huko kwa fedha za wavuja jasho!
   
 15. vimon

  vimon Senior Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Viongozi wetu si wazalendo na hawapendi wanchi wao,nitakuja kumwaga picha za hospitali zetu zilivyo hoi huko vijijini watu wanakufa sio kwa sababu siku zao zimefika ila kwa sababu ya kukosa matibabu haki ya msingi ya kila binadamu.
   
 16. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  tuwaombe madaktari wa huko majuu viongozi wetu wakienda huko wasirudi wakiwa hai. uone kama watarusha mguu huko
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Unachomaanisha ni kwamba umefika wakati tukubali kwamba tuwaache wafu wafe badala ya kutumia fedha nyingi wakati haitasaidia kurudisha uhai wao badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye mahitaji ya walio hai.

  Nadhani nakubaliana na wewe, sababu tunachokifanya ni sawa sawa na mzazi mfu kutumia mapema mengi kusogeza siku alafu akishafariki anaacha ufukara mkubwa kwa kizazi chake.
   
 18. 4

  4change JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 535
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  inauma sana kwakweli.nilimsikia chami kwenye kipindi cha dk 45 itv akisema alienda india kwa 'medical chek-up' tu na kwamba hakuwa na serious problem hata wenzake wizarani wanajua yuko fit kwani anachapa kazi kama kawa!!!
  Nani wa kuwauliza watu kama hawa?nani wa kuwakumbusha wajibu wao kwa nchi hii na wananchi wake?kwa mtindo huu kuna atakayekuwa na urgency ya kuboresha hospitali zetu kwa maana ya miundo mbinu,vitendea kazi,na wafanyakazi kwenye hizi hospitali?
   
 19. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Viongozi wako wa kisiasa mbona wanakimbilia KIPATO KIKUBWA. Ama kweli wewe ni kipofu na punguani.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Bila ya sheria katika katiba ya kukataza matumizi ya matibabu nje kwa fedha za serikali bado hawa majambazi wataendelea kulipora taifa hili kwa kinamnanamna tu............
   
Loading...