Tiba za viongozi wa kitaifa ng'ambo sasa ni mzigo mkubwa kwa wavuja jasho................

inauma sana kwakweli.nilimsikia chami kwenye kipindi cha dk 45 itv akisema alienda india kwa 'medical chek-up' tu na kwamba hakuwa na serious problem hata wenzake wizarani wanajua yuko fit kwani anachapa kazi kama kawa!!!
Nani wa kuwauliza watu kama hawa?nani wa kuwakumbusha wajibu wao kwa nchi hii na wananchi wake?kwa mtindo huu kuna atakayekuwa na urgency ya kuboresha hospitali zetu kwa maana ya miundo mbinu,vitendea kazi,na wafanyakazi kwenye hizi hospitali?

hawa viongozi wetu ni majambazi tu.......................hawana uchungu na kero zetu zikiwemo kuwa na tiba bora hapa nchini kwa sababu wao wenyewe wala hawazitumii.......
 
Unachomaanisha ni kwamba umefika wakati tukubali kwamba tuwaache wafu wafe badala ya kutumia fedha nyingi wakati haitasaidia kurudisha uhai wao badala yake fedha hizo zielekezwe kwenye mahitaji ya walio hai.

Nadhani nakubaliana na wewe, sababu tunachokifanya ni sawa sawa na mzazi mfu kutumia mapema mengi kusogeza siku alafu akishafariki anaacha ufukara mkubwa kwa kizazi chake.

jingine gharam,a za matibabu nje ni kubwa na siyo kila mtanzania mwenye matatizo yanayofanana na ya hao majambazi atapewa kipaumbele kwenda kutibiwa huko...................kwa hiyo kuna ubaguzi.........ni vyema yeyote anayetaka kwenda nje atumiye mfuko wake na wala siyo hazina
 
tuwaombe madaktari wa huko majuu viongozi wetu wakienda huko wasirudi wakiwa hai. uone kama watarusha mguu huko

hili wala siyo la muhimu kwa sababu m,agonjwa yao kwanza hayana tiba.................watarudi aidha kwenye majeneza yao au watarudi kufia hapa nchini...............tatizo ni ubadhirifu wa mali za umma ndicho tunapaswa kukemea.....
 
Haiwezekani kwa wabunge kupitisha sheria itakayowataka wajilipie matibabu ya nje ya nchi kwasababu hao hao wabunge ndio wanaofaidika na mpango wa kwenda kutibiwa Apollo; wengine hata wanawapeleka wake zao kulea mimba zao [be-rest] huko kwa fedha za wavuja jasho!

kwa hiyo una maana nguvu ya umma haiwezi kuwawajibisha hawa majambazi wa mali za umma?
 
Viongozi wetu si wazalendo na hawapendi wanchi wao,nitakuja kumwaga picha za hospitali zetu zilivyo hoi huko vijijini watu wanakufa sio kwa sababu siku zao zimefika ila kwa sababu ya kukosa matibabu haki ya msingi ya kila binadamu.

viongozi wakiendelea kujitafutia wao wenyewe tiba nje ya nchi ujue ya kuwa tiba hapa nchini kamwe hazipewa kipaumbele...........
 
rasimu ya katiba inakuja ni wakati mzuri sasa wa kuyaweka mambo haya vizuri.pendekezeni hakuna wakubwa kupelekwa nje kwa matibabu labda kwa fedha zao ili nao wapate adha tunazozipata sisi walalahoi ndipo watakapotambua umuhimu wa madaktari wetu wa hapa bongo

kwenye mapendekezo ya marekebisho ya katiba tudai kuwa tiba zote nje ya nchi serikali isigharimie na wahusika wajigharimie mwenyewe kwa sababu ni ghali, zimekithiri kwa ubaguzi wa kipato na vyeo, zina harufu ya ufisadi na zinahamisha fungu la wengi la tiba hapa nchini kwenda kwa wachache ambao kwanza ndiyo chanzo cha kudorora kwa huduma za afya hapa nchini kwa kubuni sera na utekelezaji wake mbovu..............
 
Tuchague viongozi vijana, lakini hata zitto alipelekwa India. Basi tuwashauri viongozi wafanye mazoezi huko dodoma, wapunguze viti moto, red meat na matumizi ya alcohol.
 
Tuchague viongozi vijana, lakini hata zitto alipelekwa India. Basi tuwashauri viongozi wafanye mazoezi huko dodoma, wapunguze viti moto, red meat na matumizi ya alcohol.

hawa tulionao wamekubuhu hawashauriki na hata kama wakishaurika ujue hawawezi kurudisha nyuma wakati.........makosa yao hayarekebishiki.......na usisahau ya kuwa wengi wao ni hiv ndiyo inawasumbua................kwa hiyo ngono now is a killer disease.............................hayo yote yanhitaji sheria kuwabana.................watoe mfukoni hizi gharama...........lol
 
Back
Top Bottom