Tiba ya malumbano yote ni Katiba

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MALUMBANO YOTE MSINGI WAKE MKUU NI KATIBA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kumekuwa na majibizano na hoja nyingi zinazoibuliwa na baadhi ya watu Mashuhuri. Majibizano haya yamezua mijadala mikubwa mitandaoni.Kila mtu anaibuka na umahiri wake mkubwa katika kutetea hoja yake anayoiamini. Hoja za watu mahiri na mashuhuri zimetugawa na ukizitaza Kwa jicho la tatu ni za kila mtu kujipendekeza kwenye upande anaouamini.

Hakuna hoja wala haja ya mjadala unaotafuta ufumbuzi na suluhu ya minyukano hii. Ni Jambo la kawaida kutofautiana lakini lazima kutafuta chimbuko.

Bahati mbaya sana wengi wamekuwa wanashindana Kwa kunyosheana vidole na kuwagawa wafuasi lakini binafsi ninadhani hatuzungunzii tatizo lenyewe. Tutaendelea kunyosheana vidole kuwa huyu hafai na huyu anafaa. Huyu msaliti wa serikali na Chama na huyu anajipendekeza kwenye serikali na Chama. Ningepewa nafasi ya kutafuta mwafaka, Kwanza wote ningesema mpo sawa sawa sawa. Lakini ningesema tuwe na katiba inayomfanya mtu asiwe na vitu moyoni na kusubiria mda wa kuvilipua.

Mimi kwa mtazamo wangu ninaona msingi wa mikinzano yote ya kunyosheana vidole msingi wake ni "KATIBA". Bahati mbaya linapokuja swala la Katiba WanaCCM wenzangu wengi huwa hawapendi kulisikia. Hasa vijana. Ukizungumza katiba wanakutazama mara mbili mbili kuwa huyu vipi? Leo ninatamani kuwapa Elimu makada wenzangu pengine ninaweza kuvuna Wanachama wengine wapya wanaoweza kuona hitaji la katiba kuelekea 2030.

Mwaka 2012 kama siyo 2013 Mzee Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Rais alisema "Watanzania wanahitaji Katiba Mpya itakayo KIDHI MATARAJIO YA SASA". Mimi ninakiri kuwa Katiba tuliyonayo ni nzuri ndiyo maana imetuhudunia Kwa miaka karibia 60. Lakini ubora wake wa nyuma hauwezi kuwa bora Kwa sasa ukizingatia kuna mabadiliko makubwa ya kidunia.

Wapo unapogusa hili wanakwambia katiba hii imetupatia maendeleo makubwa hivyo tuendelee nayo. Yaani tunataka pamoja na mabadiliko makubwa tuendelee kuwa na mawazo yaleyale. Katiba yetu ni kweli ni Bora, ila tunahitaji kuiboresha zaidi.

Katiba yetu tuliyonayo ndiyo wengine wanamuona Mhe Polepole Msaliti. Wengine wanamuona Mhe Nape Msaliti. Wengine wanawaona wazee wetu wengine kama Bulembo, Mhe Werema na Waheshimiwa wengine kama wamepotoka. Si kweli. Tunahitaji kuwa na katiba itakayotibu kunyosheana vidole.

Leo inebuka suala la madeni wengine wakiona Mhe Ndugai amekosea kusema kwa kuwa yeye ni Spika na kama kiongozi wa Bunge alikuwa na nafasi nyingine. Mhe Selukamba akaenda mbali kuwa kwa nini kipindi hicho hakusema anayosema Leo? Kwa hoja hii unaendelea kuona bado katiba ni hitaji la mhimu. Lakini Mhe Ndugai wakati CAG anasoma ripoti, ninamzungumzia CAG kabla ya huyu wote tunakumbuka alivyokuwa.

Watu wanahoji Kwa nini tulikopa trillion 29 na wakati huo tuliambiwa ni fedha zetu? Wanasema Mbona Mhe Rais leo Kila anachokopa anatueleza na tunajua kinafanya kazi gani?

Kukiwa na Katiba mahususi, inayokidhi matarajio ya kizazi hiki ninadhani maneno ya kunyosheana vidole yataisha. Mihimili yote itafanya kazi zao independently. Hakuna mhimili utakiwa juu ya mwingine kwenye ku check and balance.

Wanaohoji kwa nini kipindi chuma haya hayakuongelewa? Niwakumbushe kuwa Hayati Mwalimu Nyerere katika moja ya nukuu zake aliwahi kusema nchi hii ikipata kiongozi........anaweza....... Hivyo kwa nukuu ya Mwalimu mara nyingi viongozi wanatumia zaidi Hekima, Busara na Vipawa vingine kutuongoza. Lakini kuna Twitter alishawahi kuandika Ridhiwani Kikwete sikumbuki ni mwaka gani ninaamini atanikumbusha akisoma makala hii, aliwahi kusema "nilikuwa ninaongea na Baba/Rais mstaafu ameniambia nikiongoza Kwa kufuata katiba yetu tu hata kwa 50% mnaweza kuniona DIKITETA.

Hivyo mnapowachambua mnaodhani wanaongea sasa mnapaswa kujua kuwa pengine hawakuona upenyo wa Busara, Hekima n.k kuzungumza wakati mwingine.

Ninawashangaa vijana ambao hawaini umhimu wa katiba. Mimi ninadhani Katiba hii imetusaidia sana kufika hapa, lakini tunatakiwa kupata katiba nyingine itakayotuvusha Kwa miongo mingine zaidi.

Vijana ambao kibiolojia tuna mda mrefu wa kuishi tunapaswa kuwa mstali wa mbele kuhakikisha Katiba inapatikana ambayo itatuongoza bila kuwa na mivutano na kunyosheana vidole. Kunahitaji katiba ambayo itasaidia kutoa dira ya Taifa badala ya kutegemea mawazo ya kiongozi mmoja.

Na tukubali kuwa CCM haitaongoza milele, hivyo tunahitaji kupata Katiba ambayo hata tusipokuwa madarakani tutaendelea Kula keki ya Taifa bila Damu na Jasho bali jasho na Amani. Tunahitaji kushauri upatikanaji wa katiba ambayo hata ukiwa upinzani huoni kutengwa au kuumizwa. Tunahitaji katiba ambayo Upinzani utakuwa kama utani wa mpira na siyo uadui.

Kuendelea kutokuona mapungufu ya Katiba yetu ni kuendelea kuwaaminisha watu kuwa bila katiba mpya hatuwezi kushinda. CCM inashinda Kwa sera na itikadi zake, haishindi chaguzi Kwa katiba.

Tudai katiba ambayo itatupa nguvu ya kushauri Mambo makubwa ukiwa sehemu ya Mhimili wa Mahakama, Serikali au Bunge na Si katiba ya Leo ambayo watu wanavizia kukosoa wakisha staafu.
 
Tumbo kaka ndyo kila kitu now

Back
Top Bottom