Tiba ya kikombe haitibu - SERIKALI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya kikombe haitibu - SERIKALI

Discussion in 'JF Doctor' started by vivian, Jul 26, 2011.

 1. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Elvan Stambuli na Makongoro Oging'
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (pichani) amepasua jipu na kusema hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliothibitisha kuwa dawa za asili zina uwezo wa kutibu Ukimwi.

  Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Waziri Mponda ameyasema hayo huku maelfu ya watu wakiwa tayari wamekunywa tiba ya mitishamba ya vikombe inayotolewa na watu mbalimbali akiwemo mwanzilishi wake, Mchungaji Ambilikile Masapile, maarufu ‘Babu’ wa Kijiji cha Samunge, Loliondo aliyedai kuoteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.

  Magonjwa mengine aliyotaja kuwa yanatibika kwa mitishamba kwa dozi ya kikombe kimoja ni kisukari, shinikizo la damu, kifafa pamoja na magonjwa mengine yanayosumbua katika tiba za kisayansi.

  DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA
  Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) na akawataka waende kwenye vituo vya afya kupewa.

  Aliongeza kuwa vituo vyote vya afya vinatoa dawa za ARV lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania mwenye tatizo la Ukimwi anapata dawa hizo mahali alipo.
  Alisema kuna vituo 50 vya afya ambapo 30 ni vya serikali na 20 ni vya watu binafsi ambavyo vinatoa msaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.

  “Wagonjwa wanaokwenda kupata tiba asili waache kwa kuwa bado zinafanyiwa utafiti,” alisisitiza waziri na kuzua minong’ono kutoka kwa watu waliokuwa wakimsikiliza wakisema ina maana waliokunywa wamejisumbua.

  Akifafanua zaidi, Waziri Mponda alisema dawa hizo za mitishamba zinafanyiwa utafiti katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

  Aliongeza kuwa kuna waathirika 110,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi na kati yao 72,000, wanaendelea kutumia dawa za ARV na kwamba hayo ni maendeleo katika kupambana na ugonjwa huo.

  TAHARUKI
  Tamko hilo la Waziri Mponda limesababisha taharuki kubwa kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakipiga simu katika ofizi za gazeti hili wakidai kuwa serikali imechelewa mno kutoa tamko hilo.

  “Watu wengi wameuza mali zao ili waweze kutibiwa kwa mitishamba inayotolewa kwa kikombe sehemu mbalimbali nchini, serikali inapojitokeza sasa na kusema haitibu, inatushangaza, wengi wameumia tayari,” alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la John, mkazi wa Arusha.

  Mara baada ya tiba hiyo ya Babu kutangazwa, mawaziri, baadhi ya wakuu wa mikoa, makamanda wa jeshi na wananchi walifurika kwa mzee huyo na watoa tiba wengine wa vikombe huko Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa kupata dawa.

  Baadhi ya mawaziri, waliokunywa dawa hiyo ya mitishamba ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira na wabunge Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) na Augustine Mrema (Vunjo), Rose Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yohana Balele na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.

  ASILI YA DAWA YA BABU
  Mchungaji Masapile aliwahi kuulizwa kuhusu asili ya tiba yake, akasema : “Asili ya dawa hii ni Mungu mwenyewe, mti ni wa kawaida kama miti mingine ila Mungu ameweka neno lake ndani ya mti, hivyo neno ndilo linaloponya.”

  Hakuishia hapo, alisisitiza kuwa Mungu akitoa neno lake ndani ya mti huo, basi mti hautakuwa na nguvu hiyo ya uponyaji. Hata hivyo, hadi sasa Babu hajatoa tamko kuueleza umma kuwa Mungu ametoa neno lake ndani ya mti huo au la na wananchi wachache wanaendelea kwenda kupata kikombe licha ya vifo kuongezeka kila kukicha.

  WAZEE WA SAMUNGE
  Aidha, baadhi ya wazee wa Samunge waliowahi kuzungumza na wanahabari kwa nyakati tofauti walidai kuwa mti huo anaotumia Babu kutibu watu una majina mawili ambayo ni Mgamryaga na Mbaghayo na walisema unapatikana kwa wingi katika Mlima Mwegari kijijini hapo.

  Walidai kuwa mti huo ulikuwa ukitumika kama kinga ya kansa kwa kuuchemsha na kunywa supu yake na pia ulikuwa ukitibu baadhi ya magonjwa ya wanyama.

  Lakini walitoa angalizo kuwa hapo kwao hakuna waganga wa kienyeji pengine katika jitihada ya kusititiza kwamba yanayotokea huko siyo masuala ya kishirikina kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodai.

  Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakipinga tiba hiyo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe alimuambia mwandishi wa habari hii kuwa dawa za vikombe vyote inayotolewa sasa kama tiba ni mambo ya shetani.

  Alinukuu aya ya Biblia Wakorintho 1;10 msitari wa 14-22 ambayo inasema Wakristo wanaoshiriki meza ya Bwana na kukinywea kikombe cha Bwana kamwe wasishiriki kikombe cha mashetani.
  “Kwa hiyo kinachofanyika Loliondo ni ushirikina na ni kazi ya pepo wa uaguzi,” alisisitiza Askofu Kakobe.
   
 2. A

  Aine JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Too late, watu wamekunywa sana hicho kikombe, leo ndio wanasema? i knew it before!!!!!!
   
 3. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua suala la tiba bwana ni suala la kibinafsi..sasa wewe kama unaumwa utakuwa unasubiri serikali ndo ikuambie katibiwe pale..kwa hiyo waliokwenda kwa babu mimi siwalaumu ni matakwa yao binafsi..After all kama umeenda na umepona hivi hata serikali ikisema haitambui hiyo tiba wewe unaathirika nini??..Nadhani imefikia sasa watanzani wenyewe kuwa wadadisi sio tu kufuata mkumbo..oh mbona waziri fulani kafanya..oh mbona mbunge flani kafanya..''fanya unaloona lina manufaa kwako na iga pale unapoona juhudi zako zimeshindwa''
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Nonsense,kinaponya hakiponyi ni wangapiwameshaaenda na wamekufa au wako hai?? hatuna serikali tuna genge la majambazi.....
   
 5. elimumali

  elimumali Senior Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unapopewa tiba ya dawa hosp. zisipokusaidia unarudi kubadilishiwa dawa zingine, lakini kwa mtu mwingine hizo hizo zilizoshindwa kukutibia wewe humtibu yeye. Vivyo hivyo kwa dawa za mitishamba, huwatibu baadhi ya watu na wengine haziwasaidii. Hizo dawa za babu zimewasaidia wengi japo sio wote kwa baadhi ya maradhi. Kuhusu UKIMWI uhakika haupo, japo inawezekana kuwa inasaidia tu kurefusha maisha (kwa baadhi ya watu).
   
 6. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Salute you mkuu...mwenye maskio na asikie..mbona kuna waliopona? Pia wapo ambao hawajapona hivyo serikali haiwezi kukuambia wewe uufanyie nini mwili wako..
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Rafikiayangu Kigeugeu... konda naye kigeugeu.....mchungaji naye kigeugeu...serikali yangu nayo kigeugeu,.....hati miliki nao kigeu geu..

  please feel free to add more kigeugeuz....
   
 8. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mkuu do me a favour and Change your ID. you are really doing injustice to your constructive points here.
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  ndio tumeona haitibu baada ya mkuu wa kaya kwenda kupima sauzi na kukuta ngoma iko pale pale na alikunywa kikombe cha babu- waziri wa afya.
   
 10. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nichagulie basi ID unajua nyie wajinsia hiyo kwa kuchagua ID maashallah...nakusubiria..
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  hahahahaaaaa loool
   
 12. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  PakaJimmy njoo utetee hapa
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  thumb up for u,well say! Tena majambazi sugu loool
   
 14. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tatizo kikombe cha babu kilichukuliwa kisiasa zaidi kulik kiuponyaji
   
 15. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wengine mnaguna wakati wengine wanasewa Naam!! Uko wapi Babu???? Kaeni na Imani dhabiti,Mbona hicho kitengo cha utafiti hapo Muhimbili kilishatoaga majibu ya kwamba dawa ya Babu inafaa? Ama ile THREAD haikuwa na ukweli wowote?
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Fine. binafsi sijaenda kwakuwa sikuwa na tatizo la kunifanya niende huko... ushuhuda upo watu wangu wa karibu waliokwenda huko wakiwa hoooi kwa kisukari sasa wapo fiti hata fanta wanakunywa. Kwa aliyekuwa mgonjwa sasa kapona hata mngepinga namna gani hawezi kukuelewa. It is too personal!
   
 17. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Tupate na data za wanaodai kupona na walioshindwa....
   
 18. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Niambie kwanza ID ya PUMBATUPU umeipendea nini? n what is the reason Behind.
   
 19. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii ID ya pumbatupu kwa sababu 'maranyingi' binadamu huwa tuna-judge mtu kwa kumwangalia sura..yaan hatuendagi in-deep..sasa mie nimepienda hii kwa sbb at first people might ignore what i am saying coz ya ID..but if they read my thread they can see the difference..kiufupi 'ajishushae atakwezwa' na 'ajikwezae' atashushwa' umeskia bidada..
   
 20. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  He he he!!
   
Loading...