Tiba mbadala ni bomu linalokaribia kulipuka

Tiba mbadala ni bomu linalokaribia kulipuka

Kama alivyosema mmoja wetu hapa jamaa wamatumia firsa iliyopo. Mimi nilimzuia mzazi wangu kwenda kufanya vipimo kwa hawa jamaa wa tiba mbadala tena walikuja kanisani eti wanatumia computer then magonjwa yako yote yanaonekana nikamwambia mzee hivi kama hicho kipimo kweli kingekuwa kinafanya kazi hiyo pale muhimbili si wangekuwa wamenunua hizo mashine nyingi tu kupunguza msongamano? Hivyo hawa jamaa wnajua matatizo watu waliyonayo wengi ni vidonda vya tumbo ambavyo hata muhimbili watakupa dawa za kutuliza na ukifuta masharti unapona lakini wao wanasema havitibiki hospitali za kawaida. Pia maswala ya uzazi wasichana wengi wnapokosa kwatoto wanakilbilia kwenye tiba mbadala lakini hakuna jipya huko.

Umesema ukweli kabisa mkuu, ubarikiwe sana. Kuna ndugu yangu mmoja, tena msomi, alishindwa kutibiwa infertility hospitalini, akazunguka kwa hao makanjanja sana tu. Walimlia fedha nyingi sana lakini mpaka leo hajapata solution ya tatizo lake. Chezea makanjanja wewe!
 
Mkuu ujue "Kwenye msafara wa mamba na kenge pia wamo"

Ni kweli kuna makanjanja wengi ila pia kuna walioponywa na tiba mbadala..

So usi- generalize tafadhali..
 
Nahisi dhana za utandawazi na soko huru zimepokelewa "vibaya" huku kwetu afrika,au zimepokelewa "vizuri" kwa mtizamo wa wale waliozileta.nasikitika matokeo ya dhana hizi itachukua miaka mingi kueleweka na madhara yake kuonekana.
 
mkuu, kuna UTANDAWAZI na utandawizi. hiki wanachokifanya hawa waganga wa kienyeji ni UTANDAWIZI. wao kila ugonjwa wanajidai kwamba wanajua kuutibu---hadi UKIMWI! wewe uliona wapi tiba ya ukimwi? hawa waganga ni wahalifu kama wahalifu wengine, inafaa wachukuliwe hatua zinazofaa.
 
hawana tofauti na babu wa samunge huko loliondo

ni kweli kabisa mkuu. Hata babu wa samunge aliwadanganya wengi lakini hawakupona, hadi leo wamebakia na magonjwa yao sawia!
kikombe.jpg
 
Hii nchi bhana❗➖elimu,afya tumeuachia utandawazi.
 
Mliokuwa ngazi za juu fanyeni mpango muwazuie hao makanjanja
Mimi nashangaa Sana, kuna jamaa fulani wanawapima watu kwa kushika sehemu ya mashine na computer kuanza kuprinti magonjwa, hii kitu niliidhalau Sana, lakini bado wapo wanawatapeli wananchi na serikali iko kimya Sana, hii kitu ni hatari, wengine wakaenda mbali wanasema hivi vidoge vya kisasa wazungu wameweka chip kama za simu ili wamfahamu kila mtu, kitu ambacho ni uongo, na haya makitu watu wanakuwa wameyasikia Sana, lakini serikali kimya.
Kuna siku nilikuwa pale babati stendi kuu nilikwenda kucheki ile technologia yao nikagundua ni matapeli kabisa, huwezi ukagusa tu mashine uambiwe moyo unashida, mapafu yana upele, damu yako chafu, ubongo umesinyaa, utumbo mdogo umevimba, huu ni utapeli wa dhahiri, wanakuja Sana hapa Tanzania kwa sababu hatuna elimu ya kutosha na watanzania ni lahisi kuwadanganya. Mambo mengine yanafanyika utadhani hakuna serikali? Inasikitisha.
 
Kama alivyosema mmoja wetu hapa jamaa wamatumia firsa iliyopo. Mimi nilimzuia mzazi wangu kwenda kufanya vipimo kwa hawa jamaa wa tiba mbadala tena walikuja kanisani eti wanatumia computer then magonjwa yako yote yanaonekana nikamwambia mzee hivi kama hicho kipimo kweli kingekuwa kinafanya kazi hiyo pale muhimbili si wangekuwa wamenunua hizo mashine nyingi tu kupunguza msongamano? Hivyo hawa jamaa wnajua matatizo watu waliyonayo wengi ni vidonda vya tumbo ambavyo hata muhimbili watakupa dawa za kutuliza na ukifuta masharti unapona lakini wao wanasema havitibiki hospitali za kawaida. Pia maswala ya uzazi wasichana wengi wnapokosa kwatoto wanakilbilia kwenye tiba mbadala lakini hakuna jipya huko.
Unachosema ni kweli kabisa.
Kuna sehemu niliona wameweka hema stendi ya daladala wanatangaza huduma na hicho kimashine.
Wateja wao wakubwa ni wanawake.
 
Punguzen wivu acheni watu wapone, kweny mahospital yenu tumewachoka wengi mnakariri dawa
 
Umesema ukweli kabisa mkuu, ubarikiwe sana. Kuna ndugu yangu mmoja, tena msomi, alishindwa kutibiwa infertility hospitalini, akazunguka kwa hao makanjanja sana tu. Walimlia fedha nyingi sana lakini mpaka leo hajapata solution ya tatizo lake. Chezea makanjanja wewe!
Utasa dawa hauna mtapoteza pesa bureee
 
Tuwe wa kweli. Dawa yoyoye inaweza kuwa tiba na pia inaweza kuwa sumu. Kuna watu wameshakuwa vipofu,wamebabuka miili, wamepooza na mengineyo kwa kupewa tiba ya kisasa hoapitalini. Tusibeze tiba za asili, kuna watu zimewasaidia na wakawa mashuhuda kwa wengine. Tiba ni hiari ya mtu na kupona ni Majaliwa. Si kila anayetibiwa lazima apone, ndo mana hata hospitali kuna mochwari za kuhifadhia maiti ambao madaktari wamejitahidi kuokoa uhai wao lakini imeshindikana.
 
Tiba mbadala ni wezi tu,na wanawaibia sana dada zetu
 
Back
Top Bottom