Tiba hiyo hapo

Tiba hiyo hapo

Ishanitokea hii, kipindi niko bachela nyumba za kupanga, mtoto wa watu kanitembelea, usiku mvua inanyesha balaa yupo kibarazani anasonga ugali ndani mboga teyari tena kuku wa kupaka, akapita mama wa jirani akatupia macho sufuriani, weweee ugali haukuiva milele, ilibidi tule mboga tulale.
Duu,huyo mama ni jipu
 
Duu hii ilitokea kwenye harusi moja hivi yani nyama ya kuku ilikuwa kama kuku waliokufa kibudu na haikuwa na Ladha kabisa...aisee watu waliharisha ile harusi sitakaa nisahau
Hahahaha. Hii noma mkuu
 
Duu hii ilitokea kwenye harusi moja hivi yani nyama ya kuku ilikuwa kama kuku waliokufa kibudu na haikuwa na Ladha kabisa...aisee watu waliharisha ile harusi sitakaa nisahau
Mshana kwani ww hukushtukia mchezo, ilikuwaje ukala wakati hizi mambo unazijua sana
 
6a268bad58ed6c48fd78982e0765f1f2.jpg
Mkuu vipi juu ya zongo la shambani maana nalima Sana ekari nyingi mazao yaiva vizuri lakin nikija kuvuna napata kiduchu hii cyo zongo kweli
 
Kutabana zongo nkuhumpunta na haghio mwe cheni
Shida ya tiba ya ufagio anayetibu pia anapata mateso ya kugoka kama vile anatapika!!! Mi namshukuru Mwenyezi MUNGU kukaa kwangu sambaani kote alinilinda sikuwahi fikiwa na zongo hata siku moja
 
Mganga wakati anatabana ili kutoa zongo anaweza kutapika mpaka ukamuonea huruma. Osiee, zongo ni noma, usiombe kutupiwa, utahangaika na kila dawa halafu unaweza usiaamini tiba yake ni ufagio ili ndio utumikao kutabana. We wacha kabisa na hiyo makitu.
 
Shida ya tiba ya ufagio anayetibu pia anapata mateso ya kugoka kama vile anatapika!!! Mi namshukuru Mwenyezi MUNGU kukaa kwangu sambaani kote alinilinda sikuwahi fikiwa na zongo hata siku moja
Yeah anakuwa kama anacheuwa
 
Tumbo linauma, linajaa gesi, huendi choo, hujisikii kula, wakati mwingine kuharisha kunakuwepo, wanasema ukinywa maji ya magadi inasaidia na wale wenye imani za kihivyo ndo huwa wana fagia tumbo. Ajabu kuna watu wanamacho ya zongo lakini wenyewe hawajui.
Duh..!! Ndio naifahamu leo hii.
 
Back
Top Bottom