Tiba hiyo hapo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,550
729,428
6a268bad58ed6c48fd78982e0765f1f2.jpg
 
Uchawi wa kisambaa huwekwa machoni mwa mrogaji akikuangalia tu au akiangalia unachokula tayari umenasa utaumwa tumbo mwanzo mwisho
Tiba ya ni fagio inaitwa kuhumputa yani kupepewa na ufagio usoni na tumboni
Tumbo linauma, linajaa gesi, huendi choo, hujisikii kula, wakati mwingine kuharisha kunakuwepo, wanasema ukinywa maji ya magadi inasaidia na wale wenye imani za kihivyo ndo huwa wana fagia tumbo. Ajabu kuna watu wanamacho ya zongo lakini wenyewe hawajui.
 
Aisee umelichambua zongo vizuri sana pia kuna dawa ya makata ni tiba ya zongo
 
sie udogoni tulishalizoea hilo ila tulikuwa tunaondolewa kwa maombi tu, huwa tulikuwa tukienda korogwe kumsalimia bibi, tukiondoka huwa hatuagi watu twaondoka usiku usiku. Tanga wanapiga zongo mpaka gari, utawasha gari mpaka unachoka.

wamasai wana zongo la ngombe, kama ngombe wako anatoa maziwa sana, akipita mtu mwenye zongo kwisha habari yake, maziwa yanakuwa maji hata ndama hawezi nyonya.
 
Na zongo la chakula hakiivi na kikiiva hakina Ladha kabisa hasa nyama
 
Uchawi wa kisambaa huwekwa machoni mwa mrogaji akikuangalia tu au akiangalia unachokula tayari umenasa utaumwa tumbo mwanzo mwisho
Tiba ya ni fagio inaitwa kuhumputa yani kupepewa na ufagio usoni na tumboni
Mshana utaniuaaaaa. Mie tumbo sina tena sababu ya kucheka au ndo zongo tayari. We acha tu!!!!!!
 
Na zongo la chakula hakiivi na kikiiva hakina Ladha kabisa hasa nyama
Ishanitokea hii, kipindi niko bachela nyumba za kupanga, mtoto wa watu kanitembelea, usiku mvua inanyesha balaa yupo kibarazani anasonga ugali ndani mboga teyari tena kuku wa kupaka, akapita mama wa jirani akatupia macho sufuriani, weweee ugali haukuiva milele, ilibidi tule mboga tulale.
 
Duu hii ilitokea kwenye harusi moja hivi yani nyama ya kuku ilikuwa kama kuku waliokufa kibudu na haikuwa na Ladha kabisa...aisee watu waliharisha ile harusi sitakaa nisahau
 
Back
Top Bottom