TIB Develpoment Bank Yawa ya Kibiashara

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,630
1,943
Kwa muda mrefu hii benki ilikuwa inafanya kazi kama taasisi ya serikali ya kukopesha kwa ajili ya maendeleo. Ilivyokuwa inafanya kazi kwa staili hiyo watumishi wake walikuwa wanajifanyia kama taasisi nyingine za serikali ambapo urasimu na rushwa vilitamalaki. Hatimaye badala ya kutopa mikopo kwa maendeleo walikuwa wanakwamisha maendeleo yenyewe.

Sasa wameingia sokoni kibiashara kupambana na commercial banks nyingine. Swali langu ni moja je wameshawandaa hao stafu wao kufanya kazi kibiashara? Hizo rushwa na urasimu wa kupata hiyo mikopo hata kama unastahili wameacha? Wale dada zangu kwenye kitengo cha mikopo na miradi hapo milmani city wenye nyodo utadhani hiyo benk ya hawara zao wamejirekebisha?

Biashara sio mchezo, ndio maana wateja wengi waliwakimbia. Sasa tuone kama watabadilika otherwise haistahili kuwa commercial bank.
 
Back
Top Bottom