Thread ya AC Milan kutua JF hivi punde...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,490
4,774
[''maandalizi yoote yamekamilika, data za uhakika zimepatikana, history na mambo muhimu yoote yameshakusanywa, hivyo tunasubiri muda uliopangwa ili tuweze kuirusha hewani na wadau mpate kuifahamu timu hii yenye mafanikio zaidi Duniani'']

Hiyo ni kauli ya shabiki nguli wa AC Milan Gang Chomba alipokuwa anajibu maswali na kutoa maelezo kwa wachangiaji wa maswala ya michezo hapa JF ndugu Belo, Abdulhalim, Barantanda na Acid.

Gang Chomba ameahidi kuwa thread ya AC Milan itakuwa hewani hivi punde.

wapenzi wa soka mara kadhaa wamekuwa wakitaka kuanzishwa kwa thread inayoihusu timu hii ili kuweza kupata habari za nyota kama Robinho, Ibracadabra, Nesta, Pippo, Seedorf, Pato na kiungo anayeaminika kucheza soka la Mbinguni Ronaldo de Assis Morreira ama Dinho Gaucho....

Forza Milan
 
Acheni sera za kununua Zilipendwa wengi kupita kiasi, nasikia sasa mnamtaka Allesandro Del Pierro!
 
Naona AC MILAN inafufuka msimu huu tangu kuondoka kwa Sheva
 
companero ishu ni kuwa wachezaji weengi huamini kuwa ili uwe umekamilika basi ni lazima ukipute AC Milan.
Ndo maana kuna wakongwe kama Rivaldo, Ledondo na De Lima wamepita pale ili kukamilika.
 
Acheni sera za kununua Zilipendwa wengi kupita kiasi, nasikia sasa mnamtaka Allesandro Del Pierro!

Alesandro Del Pierro ama Alexander Peter ni Mungu mtu hapo Torino.
Umaarufu wake ni zaidi ya ule wa Hayati bibi Lavecchia Signorra.
So kama atatuwa Milanelo itakuwa ni rrrraha isiyo kifani.
Yaani itakuwa sawa na asali kumwagikia kwenye ftari.
 
I just know and watch English premier League! wasnt even touched to watch inter vs Ac. I like the way Gang Chomba Expresses his feelings on AC milan. Hope this may make me start watching Italian League.
Welcome to Old trafford Gang. We call it theater of Dreams!
 
Gang timu inahitaji balance. Kwa muda mrefu balance iliyoletwa na aliyekua kinda mwenye kasi, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka', ilikuwa imepotea maana mlikuwa mmebakisha majeba wengi. Walau sasa madogo Pato na Robinho wakisaidiana na mzee wa makamo Ibra wanaanza kutukumbusha enzi za kweli za Milan. Na napozungumzia enzi za kweli usidhani namaanisha zile za kina Manuel Rui Costa na Andriy 'Sheva' Shevchenko. La hasha. Naongelea zile zama za wapiga kabumbu ambao kila mtangazaji wa Serie A akitaja majina yao ilikuwa ni kama muziki wa ala ama santuri - Albertini, Maldini, Lentini!
 
Alesandro Del Pierro ama Alexander Peter ni Mungu mtu hapo Torino.
Umaarufu wake ni zaidi ya ule wa Hayati bibi Lavecchia Signorra.
So kama atatuwa Milanelo itakuwa ni rrrraha isiyo kifani.
Yaani itakuwa sawa na asali kumwagikia kwenye ftari.

Ina maana umaarufu wake umemzidi hata yule mchezaji mtanashati waliyembatiza jina la 'mkia mtukufu wa farasi ndama', yaani 'the divine ponytail'?
 
companero ishu ni kuwa wachezaji weengi huamini kuwa ili uwe umekamilika basi ni lazima ukipute AC Milan.
Ndo maana kuna wakongwe kama Rivaldo, Ledondo na De Lima wamepita pale ili kukamilika.

Mtake radhi kiungo maridhawa Fernando Redondo ambaye kamwe manazi wa theater of daydreams kama mlachake hawatamsahau kwa kumpiga tobo la kufa mtu beki wao na kutoa pande lililoleta maafa old toughroad katika mpambano murua wa ECL! Huyu alikuwa bado ni dogo tu alipohamia San Siro. Na yeye alifanyiwa majungu kama aliyofanyiwa Dinho na kocha wa taifa kwenye kombe la dunia ilhali walikuwa wanajua kuwatosa hawa ni kosa lisilosameheka! Itachukua miongo kama sio karne kadhaa Argentina kupata kiungo mtesaji kama Redondo!
 
ingawa mimi ni mpenzi wa ligi ya uingereza watoto wa emarates, ila unapoongelea AC-,milan unaikumbusha my all time fev. Filippo inzaghi a.k.a "super pippo" ukisikia uzee dawa basi cheki hii super sup ikiwa uwanjani.

much respect broda
Forza Milan

P.S onyo! zungukeni mnako zunguuka msiombe mkaja kukutana na Gunners ligi ya mabigwa any year, any day, any time Mtapata TABUU
 
Ina maana umaarufu wake umemzidi hata yule mchezaji mtanashati waliyembatiza jina la 'mkia mtukufu wa farasi ndama', yaani 'the divine ponytail'?

Mkongwe ukitaka kujua balaa la Del Piero basi pita ktkt ya mitaa ya Torino kisha paza sauti huku ukitoa maneno ya kumdhihaki...
Cha moto utakiona.
Au la subiri aende kupiga kona halafu jitahidi umzomee.
Kisha moto wake utauona
 
Mtake radhi kiungo maridhawa Fernando Redondo ambaye kamwe manazi wa theater of daydreams kama mlachake hawatamsahau kwa kumpiga tobo la kufa mtu beki wao na kutoa pande lililoleta maafa old toughroad katika mpambano murua wa ECL! Huyu alikuwa bado ni dogo tu alipohamia San Siro. Na yeye alifanyiwa majungu kama aliyofanyiwa Dinho na kocha wa taifa kwenye kombe la dunia ilhali walikuwa wanajua kuwatosa hawa ni kosa lisilosameheka! Itachukua miongo kama sio karne kadhaa Argentina kupata kiungo mtesaji kama Redondo!

Angenyoa nywele ndugu yangu huyu yoote yasingemkuta
 
Gang na Tusker, hivi nywele zina uhusiano gani na uwezo wa kusakata kabumbu? Ile ilikuwa ni chuki binafsi tu! Chuki hiyo mashabiki wa Man U wanayo dhidi ya huyu jamaa maana aliwanyanyasa sana akiwa Madrid - nahisi Tusker ni nazi mmojawapo wa Man!
 
Companero ishu ni kuwa Paselella alisema kwenye timu yake hataki watu wavae hereni, wavae kamba mkononi, wavae hereni, hataki wachole tatoo, wala wawe na nywele ndefu....
Na ndio maana Veron alivua hereni, bartgoo akanyoa nywele, na wengine wakavua kamba mikononi na kufuta tatoo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom