Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,610
- 4,782
ikiutawala mchezo kwa muda wote wa dakika 90 klabu yenye mafanikio zaidi ulimwenguni yaani AC Milan wameweza kuwa kuikanyaga na kuitimbatimba timu ya Soka ya Biaconelli timu ilioanzishwa na Bibi kizee La Vecchia Signora mwaka 1888 kwa jumla ya goli moja kwa bila.
Bao pekee la Milan lilifungwa na mbrazil Robinho na kufanikiwa kuipatia Milan jumla ya point 3 zinazowavuta mpaka nafasi ya 8.
Milan ikiongozwa na nahodha Ricardo Montolivo waliweza kukitawala kiungo cha Juve na hata kumficha mkuu wa Ndevu Kiungo Andrea Pirlo.
Mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa katika dimba la Sansiro ambapo miongoni mwa watazamaji waliohudhuria katika uwanja huu alikuwa ni Rais mwenye mafanikio ya soka yaani Silvio Berlusconi akiwa sambamba na mshambuliaji ambaye alipata kuifungia Milan magoli manne katika siku kama ya leo Milan wameibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.
nikilipoti kutoka hapa Mahuta Newala ni mimi Gang Chomba.
Forza Milan.