Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,610
- 4,782
UWANJA - Sansiro
MAHALI - Milan
WATAZAMAJI - 85,700
ULIANZA KUJENGWA - 1925
KUFUNGULIWA RASMI - 19 SEP: 1926
BARABARA YA KUINGILIA - PICCOLONINI.
Siku chache zimebaki kabla ulimwengu kushuhudia tena mtanange ambao miaka kadhaa iliyopita tulishuhudia timu moja ikitupwa nje ya mashindano na nyingine kupeta kama ilivyo ada.
Huu ni mpambano kati ya AC Milan na klabu ya Manchester UTD.
Mpambano huu unazidi kuvuta hisia za watu wengi ukizingatia kuwa Man UTD wanataka talaka yao kwa lazima ili wakaanzishe maisha mapya yasiyo na vipigo vya kila msimu, huku AC nao wakijipanga kuendeleza ubabe kwa wanyonge wao.
Leo niko hapa kwa ajili ya kuizungumizia timu yangu kipenzi AC Milan.
Milan kama Milan ilipoanza ligi ilionekana wazi kuwa isingemudu mikiki ya mashindano yoyote yale.
Lakini kuwa fit kwa wachezaji wake kulipelekea haraka kuaminiwa kuwa ni timu ambayo kwa msimu huu yaweza nyakuwa baadhi ya vikombe.
Hofu ya wapinzani wetu ilipanda maradufu pale AC walipotua ktk uwanja wa el Santiago Bernabeu na kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu iliyopewa nafasi ya kufanya vizuri kutokana na usajili waliofanya.
Hali hii imepelekea kuanzia kocha wa Man UTD mpk mshabiki aliye hapo Tanzania kujawa hofu huku wakiwa hawapati usingizi.
Milan ina wachezaji wenye vipaji kama uncle Seeldorf, pirlo, Beckham, Pato, nesta, Ambrosini, silva, dinho, Pippo na wengine weengi ambao mara kwa mara wamekuwa wakielewana sana wawapo uwanjani.
IVAN ''RHINO'' GENNARO GATTUSO...
huyu ni mtumishi wa klabu.
Mara kadhaa Gattuso amekuwa akiwashikisha adabu wachezaji wanaopambwa na sifa za mashabiki.
Siku hiyo Gattuso atakabidhiwa Rooney huku akipokea msaada toka kwa Beki bora wa kati Duniani Alesandro Nesta.
ANDREAS PIRLO...
hii ni Injini ya Milan.
Anasifika kwa kupoza mpira ili kuendana sawa na spidi ya Milan.
Ana pasi zenye akili na uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa.
DAVID JOSEPH ROBERT BECKHAM...
Ttumemtaka asihangaike na kukaba siku hiyo. Bali amimine majalo yenye upako yatakayofika kwa Hitman Pato.
UNCLE SEERDOLF...
kila mtu anafahamu kuwa kadri siku zinapozidi kwenda, basi nae anazidi kuwa imara.
Kizazi chake amebaki kwenye Ramani yeye pmj na kipa Van Der Sir.
SUPER PIPPO...
Ktk washambuliaji ambao sir Alex anawachukia basi Inzaghi anaongoza.
Na kama atapewa muda wa kucheza ni wazi ukuta wa Man UTD utakuwa busy kwa kipindi choote mpk filimbi ya mwisho.
PATO & BORIELLO
Ni double snipers.
ni wauaji hatari na wenye mbinu kali.
RONALDO ''ASSIS'' de MOREIRRA...
sina cha kumzungumzia.
Ila nauliza je ni wachezaji wangapi wa Man UTD watakaojitolea kudhalilishwa na mchezaji huyu anayefananishwa kiuchezaji na wachezaji wa ligi za mbinguni?
FRANCO BARRESI, ALESANDRO COSTACURTA NA PAOLO MALDINI...
Hawa watakuwepo jukwaa kuu wakihamasisha.
Hakika Milan tuna kila sababu za ushindi, kwani tupo ktk ari na pia tuna uzoefu mkubwa ktk mashindano haya kuliko wapinzani wetu.
Milan imebeba kombe hili mara 7, wakati wagosi wao wana mara 3.
Forza Milan.