WOWOWO. Heshima kwa ko kwa observation yenye muono wa mizani inayojitosheleza.
Kulewa madaraka si katika maneno tu bali hata vitenda. Viongozi wa CDM wameshaanza kulewa hata kabla madaraka makubwa hayajawapata.
Nina mfano mzuri wa kujinyenyekeza kwa viongozi , kwa waliochini yao.
Miaka ya mwishoni mwa ' 60 , baba yangu aliyekuwa afisa wa jeshi tulienda naye mess ya NS Mgulani(National Service), baada ya kutoka kwenye halaiki ya kitaifa Uwanja wa Taifa.
Ndani ya mess tulikuwa na mana yangu mzazi aliyekuwa akimnyonyesha mdogo wagu wa mwaka mmoja.
Ghafla walinzi waliingia ndani ya mess na kututaka tuondoke, wakati tunafikiri kinachoendelea akaingia Mwalimu Nyerere akiwa na tabasamu kubwa usoni.
Aliniuliza kama nilikuwo pale uwanjani nami nikamjibu kuwa nilikuwepo kwenye halaiki ile.
Halafu akamsalimia mama yangu SHIKAMOO MAMA!!!
Baada ya hapo akaendele na shughuli zake na kutokomea na walinzi wake wengi.
Tukio zima lilinipumbaza kwa muda. Nilikuwa nimeongea na R ais!!
Sikuelewa mantiki ya somo lenyewe mpaka nilipoingia sekondari na kufikiria kwa makini tukio lile.
Nikaja kugundua kuwa Mwalimu alikuwa na umri mkubwa kuliko mama yangu kwa wakati ule, lakini alimuamkia shikamoo mama!
Hii ni hekima ya hali ya juu, kwa kiongozi wa kitaifa kujishusha na kujinyenyekeza mbele ya watu wake,na wala hakujipunguzia wadhifa wake.
Leo viongozi wengi wanaenda kwa kujikweza sana na hivyo kutoona kuwa wanawakwaza hata wananchi wao.
Kwa Mbowe kukimbilia kufung u matawi Mbeya na kumwacha Mzee Nyimbo, kwanza its a snub, dharau.
Mtu akidharaulika mbele ya kadamnasi kwa kiongozi wake kukosa unyenyekevu, options kwa watu kama Nyimbo ni chache, hatakiwi CDM.
Makamanda Dr Slaa na Lema wapo honey moon wamewasahau wapiganaji wa mstari wa mbele wanatangatanga.sasa mbona makamanda wanaondoka tenaaa!!!,au hakua kamanda!
Sikufuatilia saana uzi huu, niliuona jana kwa ufupi, ila kama analysis ya lole gwankaja ni kweli, viongoz cdm wanapotoka
Nimepigiwa simu na mkazi mmoja wa njombe,kuwa aliyekuwa mgombea wao wa ubunge mwaka 2010,amejitoa ndani ya Cdm!kama kuna mtu mwenye taarifa zaidi naomba atujuze!
UPDATE:
SUNDAY, OCTOBER 28, 2012
MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za Umangimeza ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za Umangimeza ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]-Awaasa vijana kuwa mabadiliko ndani ya Tanzania si kuiondoa CCM na kuiweka Chadema.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa mbeya na iringa wakimsikiliza mlezi Thomasi Nyimbo katika ukumbi wa hotel yake ya Maunt livingstone jijini mbeya[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]Raymond wa Ebony FM Iringa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu wakiwa makini kumsikiliza mzee Nyimbo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za Umangimeza ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.
Nyimbo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka 10 katika Jimbo la Njombe Magharibi kabla ya kukimbilia Chadema mwaka 2010, amesema hivi sasa atabaki kuwa mwanasiasa huru asiyefungamana na vyama.
Akitoa taarifa ya kuachana na siasa ndani ya vyama jana, Jijini hapa, huku akiwa ameambatana na mkewe Mary Mwenga, alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona siasa za kushabikia vyama hazina tija kwa watanzania walio wengi na badala yake zinawanufaisha viongozi wachahe wanaojineemesha wao wenyewe kwa kutumia jasho la wananchi.
Akifafanua zaidi alisema alichojiuzulu ni siasa za vyama, lakini sio siasa, huku akitamba kuwa yeye alizaliwa akiwa ni mwanasiasa, kiongozi na mtu ambaye mawazo yake yanahitajika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake, hivyo atabaki kuwa mwanasiasa asiyekuwa na chama cha siasa.
Katika taarifa hiyo aliyoitoa kwa vyombo vya habari mithiri ya Mhadhara, Nyimbo alitumia zaidi ya saa moja na nusu kuelezea mustakabali wa taifa na vijana kutokana na vyama vya siasa kuelekea kuwatumbukiza kwenye machafuko.
Nimeachana na Chadema baada ya kubaini kuwa siasa za vyama havina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana ya vyama vya siasa vituandalie sera na tunahitaji sasa itungwe sera ya kitaifa ambayo mgombe inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi alisema Nyimbo.
Alisema hata nchi zenye wigo mpana wa Demokrasia kama Marekani ambao hivi sasa wapo kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu huwezi kuwasikia wagombea wake wakisifia vyama vyao, bali wanawaeleza wananchi wa Marekani watatekeleza vipi sera ya nchi yao .
Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.
Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa katiba mpya, inabidi itungwe sera ya Taifa itakayolindwa kisheria, ambayo kila chama kitakachofanikiwa kuingia madarakani kilazimike kuifuata badala ya ilivyo sasa vyama vinaogelea hovyo.
Alisema kuwa ndoto za kuwa mwanasiasa huru alikuwa nazo tangu zamani, na ndiyo sababu katika mabango yake ya kuhamasisha achaguliwe wakati akigombea ubunge kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikuwa na kauli mbiu ya Mtu kwanza, chama baadaye.
Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.
Nitapenda kushauriana na watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa letu nje ya mlolongo wa vyama, hivyo hata kama naipenda vipi Chadema, nalazimika kuresighn (kujiuzulu) uanachama ili niweze kutimiza azma hiyo, alisema Nyimbo.
Kilichomkimbiza Chadema.
Alisema ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho baada ya kubaini kuwa kinaenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambanua mbele za watu.
Alisema licha ya kuwaaminisha wananchi, hususani vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli,lakini viongozi wake wa daraja la juu akiwataja Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa wamekuwa wakijinufaisha binafsi.
Alisema viongozi hao pia wamekuwa si watu wa kushaurika ndani ya chama hicho, lakini kibaya zaidi ni kuendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi na kuaminisha bila kuwa na suluhisho (Mob Politics).
Alisema siasa za namna hiyo ni hatari kwa taifa kwa kuwa baada ya kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale watakapofanikiwa kuingia madarakani na kushindwa kuwatimizia kutazua vurugu.
Kuhusu CCM.
Nyimbo alidai kuwa chama hicho kinajimaliza chenyewe kutokana na kuacha suala la rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha kuwapata viongozi wake.
Hata hivyo alisema ili tatizo hilo limalizike ni wananchi wenyewe kuamua kuikataa rushwa kwa kupokea rushwa isiyoleta matunda kwani wakifanya hivyo watakuwa wamemaliza tatizo hilo .
Mfano wewe ukipokea rushwa na kuamua kufanya tofauti na aliyekuhonga kwa kuwa baadaye atakuwa hajapata kile alichotaka kukinunua toka kwako, unafikiri kesho atarudia.
Vijana.
Amewataka vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo hasi wenye kuleta mstakabali mzuri wa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani na kuiweka Chadema.
Alisema kuna mambo mengi ya msingi ambayo kama vinana wanapaswa kuwahoji viongozi waliowachagua kama wameyatekeleeza , ikiwemo kupigania katiba mpya kuwa na sera ya inayoweza kuruhusu mgombea binafsi kwa kuwa huko wanaweza kupata viongozi bora.
Kujiengua kwa Nyimbo linaweza kuwa ni pigo kubwa kwa Chadema, kwani baada ya kujiunga na chama hicho mwaka 2010, alikuwa ni mlezi wa Chadema kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, huku pia akiwa ni miongoni mwa wanasiasa wenye mvuto na wahamasishaji wazuri wa Chadema katika mkoa mpya wa Njombe.
Habari kwa hisani ya Moses Ngwat,Mbeya. picha na Mbeya yetu
[TD="align: center"][/TD]
[/TABLE
Mkuu Lole Gwakisa, nadhani humfahamu Thomas Nyimbo, amasivyo usingepoteza muda kutoa maelezo marefu haya. Nyimbo hafai kuwa kiongozi hata kidogo, aliingia CHADEMA baada ya kuwekewa zengwe na CCM na kwa ujinga wake alidhani angepata ubunge kupitia CDM, hakuingia huko kwa mapenzi mema. Nyimbo ni mlafi, mbinafsi na mwenye hila, anapenda kunyenyekewa na kuabudiwa kama nini! aliwahi kuwatisha watu walioonesha nia ya kugombea ubunge katika jimbo alilodhani ni miliki yake. Bora ameondoka mapema kwani naamini angebaki angewanyanyasa sana watu ambao angedhani ni wapinzani wake. Kumbuka akiwa CCM aliwahi adhibiwa kwa utovu wa nidhamu. Hafai mtu huyu.WOWOWO. Heshima kwa ko kwa observation yenye muono wa mizani inayojitosheleza.
Kulewa madaraka si katika maneno tu bali hata vitenda. Viongozi wa CDM wameshaanza kulewa hata kabla madaraka makubwa hayajawapata.
Nina mfano mzuri wa kujinyenyekeza kwa viongozi , kwa waliochini yao.
Miaka ya mwishoni mwa ' 60 , baba yangu aliyekuwa afisa wa jeshi tulienda naye mess ya NS Mgulani(National Service), baada ya kutoka kwenye halaiki ya kitaifa Uwanja wa Taifa.
Ndani ya mess tulikuwa na mana yangu mzazi aliyekuwa akimnyonyesha mdogo wagu wa mwaka mmoja.
Ghafla walinzi waliingia ndani ya mess na kututaka tuondoke, wakati tunafikiri kinachoendelea akaingia Mwalimu Nyerere akiwa na tabasamu kubwa usoni.
Aliniuliza kama nilikuwo pale uwanjani nami nikamjibu kuwa nilikuwepo kwenye halaiki ile.
Halafu akamsalimia mama yangu SHIKAMOO MAMA!!!
Baada ya hapo akaendele na shughuli zake na kutokomea na walinzi wake wengi.
Tukio zima lilinipumbaza kwa muda. Nilikuwa nimeongea na R ais!!
Sikuelewa mantiki ya somo lenyewe mpaka nilipoingia sekondari na kufikiria kwa makini tukio lile.
Nikaja kugundua kuwa Mwalimu alikuwa na umri mkubwa kuliko mama yangu kwa wakati ule, lakini alimuamkia shikamoo mama!
Hii ni hekima ya hali ya juu, kwa kiongozi wa kitaifa kujishusha na kujinyenyekeza mbele ya watu wake,na wala hakujipunguzia wadhifa wake.
Leo viongozi wengi wanaenda kwa kujikweza sana na hivyo kutoona kuwa wanawakwaza hata wananchi wao.
Kwa Mbowe kukimbilia kufung u matawi Mbeya na kumwacha Mzee Nyimbo, kwanza its a snub, dharau.
Mtu akidharaulika mbele ya kadamnasi kwa kiongozi wake kukosa unyenyekevu, options kwa watu kama Nyimbo ni chache, hatakiwi CDM.
MI NAONA BORA MAGAMBA YAMEANZA KUJIONYESHA MAPEMA ,HUYU MZEE UKIWA NJE YA SIASA UNAWEZA UKAONA KUWA NI MWASIASA MZURI NA MPAMBANAJI WA UKWELI LKN KIUKWELI HUYU MZEE NI MBINAFSI SANA,KWA SISI VIONGOZI WA JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI TULIOFANYA NAYE SIASA KWA HII MIAKA 2 TUNAONA AFADHARI ALIVYOAMUA KUACHANA NA SIASA ZA CDM MAANA NI MBINAFSI SANA HUYU MZEE ,ushahidi wa haya ni jinsi alivyokiendesha chama kule njombe magharibi kama mali yake na si chama cha wanachadema ,kumbuka kule njombe magharibi kuna viongozi wa jimbo lakn hawakuwa na sauti na hata kuitisha mkutano wa wananchi ama wanachama kama viongozi walikuwa hawawezi bila idhini yake,hivyo basi jimbo lile linaviongozi wasiona mvuto wa wananchi zaidi ya yeye nyimbo ,lkn angalia majimbo mengine yaliyo kwenye mkoa huu wa njombe ambayo hayakumuegemea yeye kwa kila kitu yanajiendesha na viongozi wana mvuto hata mbele ya wananchi na wanachama kitu kinachopelekea kuwa chama haikiwezi kuyumba kwa sababu ya mtu mmoja,mwezi wa sita aliyekuwa katibu wa cdm jimbo la njombe kaskazini alisimamishwa kufanya shughuli za chama lkn hatukuweza kuyumba zaidi ya kuongeza wanachama zaidi na zaidi.amini nikuambiayo cdm iliyojengwa kwenye mioyo wa watu haiwezi kuyumba sababu ya mtu mmoja lkn kama imejengwa kwa mtu mmoja itayumba hata upepo mdogo ukipita.
Mkuu Lole Gwakisa, nadhani humfahamu Thomas Nyimbo, amasivyo usingepoteza muda kutoa maelezo marefu haya. Nyimbo hafai kuwa kiongozi hata kidogo, aliingia CHADEMA baada ya kuwekewa zengwe na CCM na kwa ujinga wake alidhani angepata ubunge kupitia CDM, hakuingia huko kwa mapenzi mema. Nyimbo ni mlafi, mbinafsi na mwenye hila, anapenda kunyenyekewa na kuabudiwa kama nini! aliwahi kuwatisha watu walioonesha nia ya kugombea ubunge katika jimbo alilodhani ni miliki yake. Bora ameondoka mapema kwani naamini angebaki angewanyanyasa sana watu ambao angedhani ni wapinzani wake. Kumbuka akiwa CCM aliwahi adhibiwa kwa utovu wa nidhamu. Hafai mtu huyu.
Ameona chadema ni chama cha fujo.kusini hawapendi kabisa fujo
Chama cha Kikanda, chama cha Kikabila,Kikoo na sasa chama cha Kimangimeza...
Unajuwa principle ama unaropoka tu.Aliyebanwa ni nani?Asiyekuwa na mfano ama mwenye kutoa reference ya mchangiaji kipuuzi?Mifano ipo mingi,nipe mmoja tu.
Ni watu wa aina hii ambao wakibanwa on a matter of principle wanaji side track na kutaka mifano.
Mifano ipo mingi tu na ipo humu JF.
Cha msingi ni wanachama wa CDM kukubali kuwa chama chao kina mapungufu, hata kama anayesema hivyo ana mapungufu.
Mh! haya mkuu Ritz, Vipi umeogopa nini kupongeza!Kakosa cheo huyo.