Thomas Mashari kufuta zama za utawala wa Francis Cheka leo?

obwato

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2012
Posts
1,188
Reaction score
365
Kwa wale wapenzi wa Ngumi leo kuna pambano la kukata na shoka kwenye ukumbi wa PTA 77. Mashari ni kijana mtukutu anayeishi maeneo ya Tandale anajukumu zito la kufuta ngebe na tambo za muda mrefu za Francis Cheka anayeishi maeneo ya Ujenzi Kilimahewa Morogoro na ambaye ameshawatwanga karibu wababe wote wa DAR na hivyo kuifanya Dar yote kuwa nyuma ya Mashari. Kiufundi hawa ni mabondia wanaotumia style tofauti za upiganaji, wakati Cheka akiwa ni mzuri sana kwa "Straight Punch" mpinzani wake ni mtaalamu wa "Uper Cuts" na "Hucks" na ni mwepesi wa kuhamahama ulingoni. Kiujumla Mashari analindwa na uwezo wake wa kukwepa na kutumia aina nyingi za kushambulia kuliko mpinzani wake lakini hana pumzi za kumshinda Cheka, kama atoweza kushinda kwa "knock out" ndani ya raundi tano za mwanzo basi uwezekano wake kushinda kwa point ni mdogo sana hivyo kuruhusu gari aina ya Noah ambayo ni zawadi kwa mshindi iende mji kasoro bahari na kuwaacha midomo wazi watemi wa Dar.
 
Ngumi saa ngapi nataka nitimbe huko
 
kutoka pta vipi Jamani ?

Mpaka sasa pambano kuu bado halijaanza mechi za utangulizi ni nyingi, na kwa jinsi watu walivyo wengi na wapenzi wa mchezo huu hawachelewi kuacha kilichowaleta na kurudia kazi zao ntatoa matokeo ya jumla ili kunusuru kimeo changu.
 
Mkuu wattaka jua id watokea pemba nini
 
Mpaka sasa pambano kuu bado halijaanza mechi za utangulizi ni nyingi, na kwa jinsi watu walivyo wengi na wapenzi wa mchezo huu hawachelewi kuacha kilichowaleta na kurudia kazi zao ntatoa matokeo ya jumla ili kunusuru kimeo changu.

ni kweli mkuu mashabiki wa ngumi ni kama wapenzi wa yanga awakawii kubadili mada. Tunasubiri matokeo
 
Una uhusiano na twite twite usiogope atukuletei watu wa immigration
 
Mlioko PTA nasikia Mashari kakaa chini round ya kumi baada ya kupelekewa ngumi za kutosha za mbavu.

Tupeni matokeo, barca huku kashachezea 3-0 mpaka sasa jumla ni 7-0.
 
Pambano vipi?

Pambano ndio limekwisha sasa hivi, Cheka ameshinda kwa Knock out raundi ya kumi, Mashari amezimika kabisa, alijitahidi kuonesha upinzani lakini uzoefu na pumzi vimemuangusha.
 
poa wakuu tunashukuru taharifa hii kwa hiyo noha imehenda moro
 
Back
Top Bottom