Yahya,
Nimeangalia comments za wengi zimeonyesha mawazo chanya mengi japo malalamiko yaliyotolewa kwa upande wenu mnaweza kudhania ni chuki lakini huu ndio ukweli toka kwa jamii inayowaangalia kwenye luninga. Ninyi ni sehemu ya jamii; umri wenu unaruhusu kubadilika na uhakika wa kupata kazi kokote bado mnao!
Ushauri wangu: Najua mazingira magumu ya kazi mnayofanyia kazi, natambua forces nyuma yenu lakini ningesisitiza kuwa jaribuni kusimama kwenye tasnia yenu ya habari, mna haki kuwa na mapenzi na vyama vya siasa kama wengi tulivyo lakini mnapokuwa hewani jitahidini kuelewa kuwa watazamaji wenu wanawaangalia wakiwa na mitizamo tofauti, wale wanaopenda chama tawala na wasiokipenda na hata wale wasio na vyama.
Pili: Kipindi chenu ni kizuri sana na kipo wakati mzuri sana, mkirekebisha mnakoona watu wanalalamikia mnaweza kukifanya kiwe unique, kumbuka kipindi hiki kilisababisha kile cha TBC1 kuanza kukosa watazamaji!
MAONI YANGU:
- Baraza ni kubwa sana na endapo issue ya kutumia mashangingi itaendelea basi taifa linaelekea kubaya ukizingatia kuwa wahisani wameanza kukata misaada kwa Tanzania! Rais amechemsha big time, Wizara nyingi sana, hazina tija zipo kisiasa sana kama walivyotangulia kusema wenzangu.
- Mawaziri wengine wanashangaza kwanini JK kaendelea kuwakumbatia; Mkulo ni mzigo ambao sielewi kwanini anataka kutubebesha watanzania. Sielewi KABISA kwanini aendelee kumweka Membe Mambo ya Nchi za nje, ni kitu kilichonifanya nianze kuwaza kuwa huenda zile tetesi zinazozagaa sana zina ukweli ndani yake. Sophia Simba si tayari yupo UWT, Mbunge, Mbunge SADC, sasa pia uwaziri? Why?
- Baraza limekosa sura za vijana, vijana wamemkosea nini JK? Au wapo vijana wa rika lake?
- Umefika wakati wa Tanzania kuacha kuendesha taifa kisiasa sana, CCM ikubali hoja za wapinzani (si CHADEMA pekee) kwani zikipitiwa kwa umakini au hata serikali ikienda kuongea na wapinzani siamini kama watakataa kuwapa mawazo namna ya kulipeleka taifa LETU tunapohitaji.
- Mawaziri WAWE NA UKOMO maana inashangaza kina Masha walikuwa bado mawaziri hata baada ya uchaguzi, wakaendelea kulitia taifa hasara kwa matumizi yasiyo na tija kwa taifa. Mawaziri ni viongozi wa kisiasa tu, Wizara zinakuwa na makatibu ambao kwangu ndio watendaji wakuu, bunge linapovunjwa basi na hii mizigo ituliwe!
Aidha, nadhani umefika wakati ambapo tunatakiwa sasa kuangalia kinachosababisha mawaziri LAZIMA wawe toka chama tawala ilhali kuna watanzania wazalendo wengi toka vyama aidha vya upinzani au hata wananchi ambao wana uwezo mkubwa zaidi ya vilaza kadhaa tunaowapa uongozi unaohitaji maamuzi mazito sana lakini wakaamua kisiasa. Nadhani itatakiwa aidha mawaziri WAAJIRIWE na wakichemka wawajibishwe kisawasawa kwa mujibu wa sheria itakayowekwa.
Mwisho, nasikitika kuona Magufuli na Mwakyembe wamewekwa kwenye Wizara moja ya Ujenzi... Ni wizara ngumu kuanzia 2011; ujenzi wa barabara nyingi hivyo vunjavunja inakuja, uamuzi mgumu utalazimika kuchukuliwa maeneo MENGI na si Dar pekee; ni wazi watagombana sana na kina A1 Outdoor et all + wananchi endapo serikali haijawalipa fidia au walilipwa kidogo. Ningependa Magufuli atusaidie MABANGO mengi yaliyosambaa jiji la Dar es Salaam na kulifanya chafu sana, mabango haya yamewekwa aidha kisiasa (kiushkaji) au bila kufuata ushauri wa wataalam. Yanaweza kuwa chanzo cha ajali nyingi maana yamezagaa ovyo.
Wawili hawa ningependa wachukue maamuzi magumu; kampuni zilizopewa tenda za kuweka mataa barabarani na kuweka barabara sawa ziangaliwe upya; nguzo ni zaidi hata ya za kichina, ushkaji umetawala, taa ni fake sana, ufyekaji wa barabara MUHIMU ya Nyerere ambayo huleta wageni wengi wa kimataifa hufanyika kwa slasher (mafyekeo) na wafyekaji wamejichokea si mchezo; nina wasiwasi ajali ya fyekeo kuchomoka siku moja na kuua mtu. Teknolojia ya sasa inatakiwa kufutilia mbali huu upuuzi wa kulindana tu.
Mengine najua watu wataongeza