This Sunday LIVE on Star TV

Yahaya,

Msijaribu kuwa neutral bali mnalazimika kuwa neutral no matter nyinyi ni wapenzi wa chama gani kwa muda mrefu mmekuwa mkijiharibia mbele ya macho ya watanzania kwa mfano wakati mko karibu na ILEMELA Mlishindwa kabisa kuonyesha hatua kwa hatua zoezi la uchaguzi lilivyokuwa linaendelea, licha ya kujigamba kila wakati kuwa mna waandishi wenu eneo hilo pamoja na Nyamagana, fun enough hata idadi ya kura na "MTU" aliyeshindwa mkashindwa kutangaza, kigugumizi cha nini? Kwa stahili ya habari zenu ni wazi mmekula yamini na STAR TV na niulize tu mtafia hapo?


Mwandishi mmoja mkongwe alipata kunieleza hili.........WANANCHI AMBAO NI WALAJI, WATAZAMAJI NA WASIKILIZAJI WANAJUA ZAIDI KULIKO MNAVYOJUA NYINYI WAANDISHI.....Huo ni ushauri wangu kwenu!

Mchango wangu:

Watu hawa walioteuliwa wana kitu kipya (mawazo mapya) yatakayotusadia kutatua matatizo ya msingi ya watanzania? Je watu wanaoweza kuwa na mawazo huru nje ya mfumo wa kimafia wa CCM?


Ni mimi Mtembezi!

Finally umetoa hoja mtembezi. Being critical siyo kila wakati ukosoe kila jambo.
 
Maoni yangu:

  • Serikali iliyoundwa ni kubwa na kuna wizara ambazo mantiki yake hayajulikani mfano Mahusiano,
  • Wizara nyingi na zisizo na uhuhimu wa manaibu waziri zimewekwa kwa ajiri ya kutoa shukurani na si kuwasaidia wapiga kura
  • Je, sasa wakati muafaka muundo wa serikali ukajadiliwa na ukawa wa kudumu, ukawa kwenye katiba mpya?
  • Serikali iko tayari kuzifanyia kazi sera za upinzani ukizingatia kuwa kuna wapiga kura wengi walioziona zinafaa na wanaamini zitatuoa hapa tulipo kuelekea kule tunakotaka kwenda?
Swali la uzushi na la nyongeza:
  • Tujuzwe ni nini serikali hii itafanya kuhusu masuala tete ya OIC, je ni kweli serikali inagharamia uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi?

Shukrani Ntemi kwa ushiriki wako
 
Kama ww ni Yahaya muendesha kipindi pamoja na yule KULWA naombeni sana mjadala wenu uwe huru, kusema kweli nilikua mshabiki sana wa kipindi hicho lakini mlipoanza biashara za kuwa biased (kuipendelea CCM) MFANO; Slaa alikaribia kususia mjadala wa Star Tv kati yake na Kinana so mi niliona haina maana, pili amueni moja, ondoeni kipindi cha kupiga simu au wekeni muda mrefu kidogo sio mnaruhusu kwa dk 15 TU!! Tuwaeleweje?

Hope ujumbe umefika
 
Mimi nadhani maendeleo nchi hii hayataletwa na kutunga na kutungua wizara. JK tangu aingie madarakani ametunga na kutungua wizara labda kuliko rais mwingine tuliyewahi kuwa naye. Kwa mfano alipoingia akatungua wizara za ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, akaleta miundombinu. Miaka miwili baadaye akaitungua na kuanzisha mawasiliano, sayansi na teknolojia, baada pia ya kuiua ile ya elimu ya juu, sayansi na teknolojia. Huu ni upuuzi na inaonyesha JK alichukua fomu ya kuomba kugombea urais bila kujua alikuwa anataka kufanyia nini nchi hii ndio maana anaonekana kujaribu jaribu.

Angekuwa na lengo angeunda serikali ya wizara kumi na tano tu, hakuna naibu. Kazi nyingi zinafanywa na departments na executive agencies. Angefuta wizara zifuatazo:
  1. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Katibu Mkuu Kiongozi afanye kazi za waziri huyu)
  2. Ofis ya Rais Utawala Bora (PCCB na vyombo vingine vya utawala bora vinaweza kujitegemea)
  3. Ofisi ya Rais Mahusiano (Kurugenzi ya Mawasiliano inaweza kufanya hili, kama kuna haja)
  4. Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano (haina sababu-Makamu wa Rais mwenyewe afanye hili-anaweza akawa na wasaidizi)
  5. Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira (achia NEMC)
  6. Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji (Sijui ina maana gani kwa kweli ila Uwekezaji kwa wageni unashughulikiwa na TIC)
  7. Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Bunge(hakuna sababu)
  8. Wizara ya Sheria na Katiba (Mwanasheria Mkuu anatosha wakati Mahakama inapaswa kujitegemea)
  9. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (Tume ya Mawasilano an Tume ya Sayansi na Teknolojia zinatosha-hawa hawahitaji wanasiasa kuwaingilia)
  10. Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo (Habari ingepelekwa Tume ya Mawasilano, Utamaduni BASATA na michezo BMT)
  11. Wizara ys Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Peleka Mambo ya Nje)
  12. Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Changanya na Kilimo)
  13. Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto (haina sababu kuwa wizara)
  14. Wizara ya Maji (peleka kazi zake kwenye halmashauri na tayari kuna taasisi kila halmashauri zinazosimamia upatikanaji wa maji)
  15. Wizara ya Ujenzi (unganisha na Uchukuzi na ili iwe na maana iitwe Usafirishaji (Transport)).
Halafu majina tu ya Wizara nyingine yamejaa uswahili kama vile wanataka kuweka malengo yote ya wizara:
  1. Kazi na Ajira iitwe Kazi
  2. Elimu na Mafunzo ya Ufundi iitwe Elimu
  3. Kilimo, Chakula na Ushirikia (ingepaswa kuchanganya na mifugo na uvuvi) iitwe Kilimo
  4. Viwanda na Biashara iitwe Biashara.
  5. Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Ardhi na Nyumba)
 
Great responses Yahya,

Tunakuomba uzingatie hayo ili KUREJESHA IMANI KWETU WATAZAMAJI tunaowafatili tena kwa umakini.

USHAURI:

Msiegemee pande yoyote mnapokuwa hewani, uwe unaomba ushauri wa mada (TOPIC) humu ili tukupe dondoo ziwasaidie katika vipindi vyenu ili mrejeshe imani kwa watz iliyoanza kufifia siku za karibuni.
 
Ni kweli mnaonyesha kwamba hamjakomaa kama waandishi wa habari, kwa sababu mnapochambua mambo mbalimbali ya siasa za hapa nchini; mnadhihirisha waziwazi bila kificho mnapenda chama gani na mnataka watu wote waone kuwa hicho chama chenu (CCM) ndio bora.

USHAURI: Ingieni kwenye siasa na muachane na uana habari, au kuweni wana habari.

Siku hizi nikimkuta huyo Baruani (anaechonga o) ktk kipindi naweka station nyingine .... anaudhi kwelikweli, ana ushabiki na unazi uliokithiri!!
 
Asante Yahya kwa taarifa yako, naomba usiegemee upande wowote, uwe neutral ukitusaidia kuwakilisha maoni yetu. Vilevile umekuwa na tabia ya kuipendelea CCM, huku unakatisha mazungumzo ya wapiganaji kwa makusudi.
 
Yahaya angalau kidogo unajitahidi, huyo nanii huyo mwenye O, eti mchambuzi wa mambo ya siasa... Siasa gani anayochambuaga?T ena umefanya vizuri kushirikisha JF ktk kipindi chako.

Kingine huyu Mabuga ndo hafai kabisaaaaaa.... maswali ya wageni anajibu yeye. YAHYA JIREKEBISHE KIDOGO UNAWEZA! Tuko pamoja hiyo siku!
 
Yahya,

Nimeangalia comments za wengi zimeonyesha mawazo chanya mengi japo malalamiko yaliyotolewa kwa upande wenu mnaweza kudhania ni chuki lakini huu ndio ukweli toka kwa jamii inayowaangalia kwenye luninga. Ninyi ni sehemu ya jamii; umri wenu unaruhusu kubadilika na uhakika wa kupata kazi kokote bado mnao!

Ushauri wangu: Najua mazingira magumu ya kazi mnayofanyia kazi, natambua forces nyuma yenu lakini ningesisitiza kuwa jaribuni kusimama kwenye tasnia yenu ya habari, mna haki kuwa na mapenzi na vyama vya siasa kama wengi tulivyo lakini mnapokuwa hewani jitahidini kuelewa kuwa watazamaji wenu wanawaangalia wakiwa na mitizamo tofauti, wale wanaopenda chama tawala na wasiokipenda na hata wale wasio na vyama.

Pili: Kipindi chenu ni kizuri sana na kipo wakati mzuri sana, mkirekebisha mnakoona watu wanalalamikia mnaweza kukifanya kiwe unique, kumbuka kipindi hiki kilisababisha kile cha TBC1 kuanza kukosa watazamaji!

MAONI YANGU:

  1. Baraza ni kubwa sana na endapo issue ya kutumia mashangingi itaendelea basi taifa linaelekea kubaya ukizingatia kuwa wahisani wameanza kukata misaada kwa Tanzania! Rais amechemsha big time, Wizara nyingi sana, hazina tija zipo kisiasa sana kama walivyotangulia kusema wenzangu.
  2. Mawaziri wengine wanashangaza kwanini JK kaendelea kuwakumbatia; Mkulo ni mzigo ambao sielewi kwanini anataka kutubebesha watanzania. Sielewi KABISA kwanini aendelee kumweka Membe Mambo ya Nchi za nje, ni kitu kilichonifanya nianze kuwaza kuwa huenda zile tetesi zinazozagaa sana zina ukweli ndani yake. Sophia Simba si tayari yupo UWT, Mbunge, Mbunge SADC, sasa pia uwaziri? Why?
  3. Baraza limekosa sura za vijana, vijana wamemkosea nini JK? Au wapo vijana wa rika lake?
  4. Umefika wakati wa Tanzania kuacha kuendesha taifa kisiasa sana, CCM ikubali hoja za wapinzani (si CHADEMA pekee) kwani zikipitiwa kwa umakini au hata serikali ikienda kuongea na wapinzani siamini kama watakataa kuwapa mawazo namna ya kulipeleka taifa LETU tunapohitaji.
  5. Mawaziri WAWE NA UKOMO maana inashangaza kina Masha walikuwa bado mawaziri hata baada ya uchaguzi, wakaendelea kulitia taifa hasara kwa matumizi yasiyo na tija kwa taifa. Mawaziri ni viongozi wa kisiasa tu, Wizara zinakuwa na makatibu ambao kwangu ndio watendaji wakuu, bunge linapovunjwa basi na hii mizigo ituliwe!
Aidha, nadhani umefika wakati ambapo tunatakiwa sasa kuangalia kinachosababisha mawaziri LAZIMA wawe toka chama tawala ilhali kuna watanzania wazalendo wengi toka vyama aidha vya upinzani au hata wananchi ambao wana uwezo mkubwa zaidi ya vilaza kadhaa tunaowapa uongozi unaohitaji maamuzi mazito sana lakini wakaamua kisiasa. Nadhani itatakiwa aidha mawaziri WAAJIRIWE na wakichemka wawajibishwe kisawasawa kwa mujibu wa sheria itakayowekwa.

Mwisho, nasikitika kuona Magufuli na Mwakyembe wamewekwa kwenye Wizara moja ya Ujenzi... Ni wizara ngumu kuanzia 2011; ujenzi wa barabara nyingi hivyo vunjavunja inakuja, uamuzi mgumu utalazimika kuchukuliwa maeneo MENGI na si Dar pekee; ni wazi watagombana sana na kina A1 Outdoor et all + wananchi endapo serikali haijawalipa fidia au walilipwa kidogo. Ningependa Magufuli atusaidie MABANGO mengi yaliyosambaa jiji la Dar es Salaam na kulifanya chafu sana, mabango haya yamewekwa aidha kisiasa (kiushkaji) au bila kufuata ushauri wa wataalam. Yanaweza kuwa chanzo cha ajali nyingi maana yamezagaa ovyo.

Wawili hawa ningependa wachukue maamuzi magumu; kampuni zilizopewa tenda za kuweka mataa barabarani na kuweka barabara sawa ziangaliwe upya; nguzo ni zaidi hata ya za kichina, ushkaji umetawala, taa ni fake sana, ufyekaji wa barabara MUHIMU ya Nyerere ambayo huleta wageni wengi wa kimataifa hufanyika kwa slasher (mafyekeo) na wafyekaji wamejichokea si mchezo; nina wasiwasi ajali ya fyekeo kuchomoka siku moja na kuua mtu. Teknolojia ya sasa inatakiwa kufutilia mbali huu upuuzi wa kulindana tu.

Mengine najua watu wataongeza
 
MAONI YANGU,

1. SERIKALI HII IANZE MARA MOJA MCHAKATO WA KATIBA MPYA UZANDIKI WOTE UNANZIA HAPO
2. SERIKALI HII IRUHUSU KUUNDWA KWA TUME HURU YA UCHAGUZI UNAFIKI WOTE UNAENDELEZWA HAPO KUANZIA KWENYE KATIBA
3. SERIKALI HII IPUNGUZE PAYE FROM 14% TO 10%
4. SERIKALI HII IFUTE WAKUU WA WILAYA BADALA YAKE WABAKI WAKURUGENZI
5. SERIKALI HII IFUTE LOAN BOARD NA KULIPIA ADA VIJANA WOTE WANAOCHAGULIWA VYOU VIKUU
6. SERIKALI HII IAGIZE MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII KUJENGEA NYUMBA WANACHAMA WAKE NA KUWAKATA RIBA NDOGONDOGO BADALA YA KUWAPITIA WANASIASA NA WAFANYABIASHARA MICHANGO YETU (GPF,NSSF,PPF,PSPF, LTF ect)
7. SERIKALI HII ISINUNUE MASHINGINGI TENA YA ANASA
8. SERIKALI HII IJENGE BARABARA ZENYE FLY OVER MIJI MIKUU DAR, MWANZA, ARUSHA, MBEYA NA BARABARA MPYA MIKOA MINGINE
9. SERIKALI HII IWEKE BIMA YA AFYA KWA KILA RAIA KUTIBIWA BURE!
 
NOTE this;-
1.Kuna umuhimu gani wa kuwa na wizara ya Africa Mashariki, wakati tunayo wizara ya mambo ya Nje?
ANGALAU;
A.Tungekuwa na wizara ya mambo ya nje, alafu ikawekwa IDARA, ambayo ingeshughulikia Masuala ya Africa Mashariki au hata manaibu wawili..

B.Wizara ya MAHUSIANO na Uratibu ingeunganizhwa na MUUNGANO.

C.Wizara ya Nyumba, Ardhi na makazi Ingeunganishwa na MAZINGIRA.

D.Kungekuwa na wizara moja tu ya MALIASILI ambayo ingebeba MADINI,MAJI alafu NISHATI ingeenda kwenye SAYANSI NA TECHNOLOGIA.

E.UCHUKUZI na UJENZI zingebaki kama awali MIUNDOMBINU.

F.KILIMO NA CHAKULA ingeunganishwa na MIFUGO NA UVUVI

Kwa misingi hiyo hapo jii simaanishi majina yaendelee kuwa kama hivyo, bali ingetafutwa jina linaloweza kucover viunganishi hivyo, na kuweka idara husika ndani ya wizara ambazo zingekuwa effective.

Pili Rais anaposema kuwa WATU WANACHOKA, haina maana ndo ugawanye gawanye wizara HOVYO HOVYO IVYO, cha msingi ni kuwa na watu ambao wanaweza kujidedicate katika kazi BASI, maana wanalipwa vizuri sio kuwa na wizara zenye majukumu YALEYALE ila MAJINA TOFAUTI
 
1. Hivi hao vijana ambao JK ali promise wako wapi?
2. Kwa nini kuna wengine hawajachaguliwa kwa namna halali lakini unakuta wanachaguliwa kua waziri huku bado wana kesi mahakamani?
3. Je, serikali inapanga vipi kurekebisha hiyo mikataba mibovu ambayo inaendelea kutunasa kwenye mtego wa kukosa full advantage ya resources za nchi?
4. Katiba mpya vipi?
5. Shangingi mwisho jamani pamoja na maanasa ya mandazi na mbuzi kwenye minada ya Dodoma wakati wa bunge n.k...
6. Wastaafu kweli watashughulikiwa jamani? - HII IMENIGUSA KWELI
 
Naomba sana sana mzungumzie swala la uwezekano wa utekelezaji wa ahadi alizotoa mkwere, kuna mtu mmoja alilist ahadi na kufikia trilion tisini hapa hapa jamvini! mjulishe Baruani asiharibu kipindi kama vipi ahamie clouds akasaidiane na Kibonde!! muda wa kupiga simu uongezwe!!!
 
maoni yangu: kuachwa kwa pro. mwakyusa, pro. kapuya na pro. msola, maprofesa wa3 kunaashiria kwamba kuwa na elimu kubwa(pro) sio kuwa na uwezo wa mafanikio ktk siasa, bali dhamira uliyo nayo ndio inayokuwezesha kupata mafanikio ya kuwaletea watu maendeleo. pia ninaushauri kwa managment ya startv kuwa background yenu iko busy saana yaani hata watu unapata shida kuwaona, hapa kuna ndizi, mahindi, miti nk. nashauri kuwe na plain au picha zipunguzwe kidogo kuleta muonekano mzuri, nategemea mabadiliko jpil
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91256-this-sunday-live-on-star-tv.html
 
Shukrani wanaJF wote ambao bado mnaendelea kutoa hoja za msingi hasa kuhusiana na kipindi kijacho jumapili. Tusi-deal na individual tu-deal na hoja iliyopo mezani.

Kila upande ulilalamika wakati wa uchaguzi inawezekana unatolea mfano kipindi ambacho ulikuwa tayari na mtazamo. Msimamo wetu ni kuwa neutral daima kama unatufuatilia vema na si kishabiki.

NONONONONP; YAHYA NIKO MWANZA ila kwa ufupi mko biased sana wewe na MABUGA; heri Baruani huwa yuko makini kujizuia na kuondoa uashabiki; hakuna mwenye mtazamo kuna watu wasomi wanapima kwa mizania na kumbuka watazamaji ndio wanaona kuliko nyie mliopewa rungu kuendesha vipindi; narudia mnajiabishaga sana kushabikia upande wowote hasa CCM, hata kama mabosi wenu ni CCM lakini mna taaluma lazima mzitumie vema ziweze kuwa na manufaa kwa wote na mimi niliacha kabisa kuwaangalia sababu ya ushabiki wenu; mnaanza kuwa watu uchaguzi ukiisha ndio maisha gani hayo kwa kusifia chama hicho hicho CCM. Tumieni vema taaluma zenu au la mtaondoka duniani wazima wazima hamtaacha chochote cha kukumbuka kwa jamii zenu ambazo kwazo mmesoma na kufikia mlipo sasa; kama nimeongea kwa ukali samahani ila nilitaka ujue hisia zangu seriously huwa mnakera sana

Kuhusu Baraza; naona kubwa kuliko makusanyo yetu ndio maana hata awemo magufuli au nani; ila naamini ya kuwa hakutakuwa na jipya ndani ya miaka mitano; 61==>47==>50; huenda likivunjwa sasa litakuwa 64 by a returning factor; rais wetu hana uchungu na nchi yake hata baraza liwe kubwa yeye haimhusu maana maisha bora kabisa kuna wasi wasi gani kwa walala hoi. Niseme huenda akawa miongoni wa marais ambao wataondoka na kuiacha nchi wala hamna watakachomkumbuka nacho; atapotea kama majivu, siku inakuja tutapata mtu serious no matter from which party

Mtuletee wachambuzi mahiri kama akina mwesiga/lwaitama sio mnatueletea makada wa CCM tu useless
 
Yahya unajitahidi lkn huyo mwenzio barwani yuko biased kinoma anajifanya mchambuzi wa siasa wkt haelewi kitu,amepotosha sana umma juu ya walk out ya cdm
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom