Star TV tuongee asubuhi mnapinga sensa?

Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,961
3,592
Leo kipindi cha star tv tuongee asubuhi, amealikwa mwandishi Odelo charles Odelo kuzungumzia habari ya sensa. Dooh jamaa ameipinga sensa vibaya. Hoja zake ni hizi..

1. Kama tuna taasisi ya nbs kazi yake ni ipi kiasi mpaka ifanyike sensa baada ya miaka kumi.

2. Maafisa takwimu wilaya wanaolipwa na serikali kazi yao nini??

Sijui kama star tv wamepanga mjadala uwe hivi maana swali mezani ni upi mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha sensa lakini jamaa anavyochana chana hili jambo ni hatari.
 
Yuko sahihi kabisa kwa hoja hizo.Sensa haiwezi kukuletea maendelele kama tunavyoaminisha na hawa viongozi feki.

Kila sehemu ya nchi hii kuna changamoto nyingi tu ambazo hazihitaji uwepo wa sensa kuzijua.

Kipindi hiki sensa imeongeza gharama kwa kuwalipa hao wafanyakazi ambapo imepelekea kuanzishwa kwa tozo za miamala za benk

Sent using jamii forums mobile app
 
Leo kipindi cha star tv tuongee asubuhi, amealikwa mwandishi Odelo charles Odelo kuzungumzia habari ya sensa. Dooh jamaa ameipinga sensa vibaya. Hoja zake ni hizi...
Hii ndo madhara ya kualika watu wenye ufahamu mdogo kwenye mijadala. Utaratibu huu unafanana duniani kote.

Kuna baadhi ya taarifa zinaweza kukusanywa na maafisa takwimu lakini hili la kuhesabu watu hufanywa kwa staili hii duniani kote.

Kama kuna tofauti ni ndogo lakini lazima census workers wapite majumbani kuhesabu watu.
 
Hiyo pesa ya Sensa .......ni Bora ipunguze bei za mafuta Tu......maana yashapanda mpaka kero...Ila bado yameshupaza shingo na kutaka mi Sensa Yao isiyoeleweka pumbavu
 
Hii ndo madhara ya kualika watu wenye ufahamu mdogo kwenye mijadala. Utaratibu huu unafanana duniani kote...
Wewe uliishi ulaya ya wapi ukakuta watu wanapanda na kushuka maskaiskrepa kwenda kuhesabu watu!

Ungesema wao huchukua taarifa mara unapozaliwa na kufariki na kuzihifadhi, pia kila mtu anayeingia na kutoka anajulikana kutokana na matumizi ya anuani za makazi.
 
Wewe uliishi ulaya ya wapi ukakuta watu wanapanda na kushuka maskaiskrepa kwenda kuhesabu watu! Ungesema wao huchukua taarifa mara unapozaliwa na kufariki na kuzihifadhi, pia kila mtu anayeingia na kutoka anajulikana kutokana na matumizi ya anuani za makazi.
Hata huko UK wanatumia questionnaire kupata data kutoka kwa kila household kila miaka 10. Households ndio hujaza hizo questionnaires.
 
Hii ndo madhara ya kualika watu wenye ufahamu mdogo kwenye mijadala. Utaratibu huu unafanana duniani kote. Kuna baadhi ya taarifa zinaweza kukusanywa na maafisa takwimu lakini hili la kuhesabu watu hufanywa kwa staili hii duniani kote. Km kuna tofauti ni ndogo lakini lazima census workers wapite majumbani kuhesabu watu.
Ha ha ha
 
Katika familia kama umeenda kutembeza bakuli sababu ya njaa, anaetaka kukusaidia atakuuliza mpo wangapi katika familia? Ili ajue namna ya kutoa msaada. Sensa ni muhimu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maeneo Idadi na taarifa za watu wanazo ila hakuna mabadiliko ya wazi Zaid sera za kishamba na utekelezaji sifuri .
Sijui kwa level ya taifa itakuwaje
UNFPA wanaaangalia fiction movie hii.
 
Back
Top Bottom