This Sunday LIVE on Star TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This Sunday LIVE on Star TV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Nov 25, 2010.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mjadala wa Kipindi cha Tuongee asubuhi utaangazia muundo na taswira ya serikali mpya kwa maendeleo na ustawi wa Taifa.

  WaJF tumeni maoni, mitazamo na ushauri wenu katika mada hiyo na tutayasoma mawazo yenu hewani.

  Ahsante
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  baraza bado kubwa, ambapo bado litakuwa gharama kubwa kwa serkali
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Saa ngapi?

  Kuna garantii yoyote umeme hautakatwa? Mgao umekweisha kwani?

  Maoni yangu mimi: Ninamuomba Mungu afanye maajabu yake ili miaka mitano itimie kesho JK atupishe Watz.

  Amen.
   
 4. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mjadala utaanza saa 1 na nusu asubuhi mpaka saa 3 kamili asubuhi. LIVE calls pia zinaruhusiwa japo huwa ni kazi kupata line.

  Huu umeme tuendelee kutazama kama utakuwepo ama la! Ni nje ya uwezo wetu wadau
   
 5. Joyum

  Joyum Senior Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nauliza uhalali wa sofia simba kuwepo kwenye baraza hili, na pia kuwakilasha bunge la SADC bila hata kuhojiwa kuna nini kimejificha hapa kwa huyu mama!?!!!!!!!!!!
   
 6. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ahsante Yahya kwa taarifa,

  Mimi ni miongoni mwa wanajamii tunaowafatilieni sana, ila last Sunday uliahidi kuendeleza mada iliyokuwa moto na kwamba mngeirejea tena wiki hii.

  Haaya tena wageni mliowaalika this week watatushibisha tukianza mapema kutoa maoni yetu?
   
 7. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yahya M.

  Usiwe biased sana, kipindi cha uchaguzi ilibidi niache kuangalia vipindi vyako hasa wewe na Yule jamaa mwenzako Mabuga or something like that na kuna yule jamaa mwingine ana O, mnaegemea Chama Chenu Mpaka mnajisahau, nyinyi ni waandishi wa habari inabidi msi-pick sides, mnakera sana na kama mkiendelea hivyo sidhani kama mtafikia level za kuwa watangazaji mahiri.

  Last weekend ulikuwa na jamaa wa NCCR na Jamaa wa CDM duu rangi zako zilikuwa zinawakawaka, baada ya kuona unashtukiwa ukaanza kumpa support ya kufa mtu jamaa wa NCCR ili jamaa wa CDM aonekane hana maana, huku ukimkatisha kila mara na kupinga kila anachoongea, mlivyo watu wa ajabu na Dar kulikuwa na jamaa mwingine wa CDM na Bunsen Bana, kwa kifupi mlikuwa wanne against one na jamaa aliwamudu vizuri sana.

  Masako wa ITV ni SiSiEm lakini akifanya interview huwezi jua yuko chama gani, ni juzi tu ndiyo nimegundua kuwa ni mwanachama wa SiSieM.

  Badilika umri unakuruhusu!
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Maoni yangu:

  • Serikali iliyoundwa ni kubwa na kuna wizara ambazo mantiki yake hayajulikani mfano Mahusiano,
  • Wizara nyingi na zisizo na uhuhimu wa manaibu waziri zimewekwa kwa ajiri ya kutoa shukurani na si kuwasaidia wapiga kura
  • Je, sasa wakati muafaka muundo wa serikali ukajadiliwa na ukawa wa kudumu, ukawa kwenye katiba mpya?
  • Serikali iko tayari kuzifanyia kazi sera za upinzani ukizingatia kuwa kuna wapiga kura wengi walioziona zinafaa na wanaamini zitatuoa hapa tulipo kuelekea kule tunakotaka kwenda?
  Swali la uzushi na la nyongeza:
  • Tujuzwe ni nini serikali hii itafanya kuhusu masuala tete ya OIC, je ni kweli serikali inagharamia uanzishwaji wa mahakama ya Kadhi?
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Maswali yangu pokea kabisa sasa hivi maana Jumapili bado nitakua Kijijini na wala sitoona TV huko:

  1. Je, Mama Celina Kombani anayo CV ya kutosha kutuletea mabadiliko ya kweli kuandika KATIBA MPYA na Kuwapata VIONGOZI wetu halisi tuliowachagua sisi Vijana?

  2. Mhe Sitta kupewa IDARA ya Afrika Mashari ambayo ni meza ndogo sana ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje, ina maana JK anatutukana sisi wananchi na kusema adui wake namba moja ni sisi ambao jamaa alikua anafanya kazi kubwa ya kututetea au tumwelewe vipi na hicho kitendo cha kejeli?

  3. Je, wizara hizo zilizoongezeka zaidi zitakua kwa gharama ya nani, au ni sisi sisi huku ambao bado tuna machungu ya kufa mtu kuporwa ushindi wetu halali?

  4. Je, ni nini malengo ya baraza hili hasa, KULETA MABADILIKO tunayotaka sisi au kutupinga na kuleta mapambano kwa mara ya kwanza nchini? Endapo dira ya kuundwa kwa baraza hili litakua linapingana na mahitaji ya sasa ya taifa (MABADILIKO YA KWELI) basi itakua ni makosa ya miaka yote mitano hii!!!

  NB: Nashukuru safari hii haujatukurupusha kwa hilo. Maswali mengine wataongeza Wana-JF ambao wametanda ulimwengu mzima.
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hivi, naomba kujua huyu mtoa mada ni nani?

  Isijekuwa anatufanya sisi mazuzu.

  Kucheza na akili za wanaJF. Anataka kujua wanaJF wana maoni gani na serikali ya mkwere.

  tuwe waangalifu kidogo au tutafute thead nyingine.
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Umeona eeh! hawa jamaa kipindi chao ni kizuri sana na mimi binafsi ninakipenda sana hasa siku za weekend huwa sikikosi. Tatizo lao kwa upande wa siasa ni ushabiki wao kwa CCM. Yani jamaa ni watetezi wa CCM utadhani wao ndio Makamba. Na kwa staili hii watu wanaanza kukipotezea kipindi chao. Bora kumwangalia Dotto Bulendu Jumamosi na Angelo Mwoleka inatosha lakini hawa akina Yahya, Mabuga na Baruan yani wameharibu kipindi kabisa. Lakini bado muda upo wanaweza kubadilika na kipindi kikawa na mvuto kama zamani.
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ukweli kaka Yahya M. umenikuna,

  Upele umepata mkunaji sasa...

  Tunawapenda sana STAR TV hasa ninyi watangazaji ni mahiri sana kwa uchambuzi, ila kama alivyosema BADO NIPONIPO ni kwamba kipindi cha uchaguzi mliegemea upande fulani wa chama tawala.

  Ninyi ni watangazaji vijana na mna hekima & busara mnapokuwa mnaongoza vipindi ila msiegemee pande fulani, sisi ni watazamaji vijana lakini ni wasomi na tunafatilia kwa kina mambo mnayoendesha...tunawashauri mtazame vema na mjirekebishe kwani mlishajijengea sifa nzuri kwenu BARUANI, SYMPHROSE, YAHYA M, PAUL MABUGA pamoja na mzee SAMADU aka jungu kuu..!!
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa ni mtangazaji wa star tv(naambiwa sasahivi ananoa bongo SAUT) ila bado anaendelea kukamua startv kama kawaida. Huwa anaendesha kipindi cha tuongee asubuhi, wakati mwingine kwa ushirikiano na paul mabuga na baruan muhuza. wakati mwingine anachambua hotuba na peter omari. pia alikuwa anashirikiana na daktari isack ndodi, siku hizi namuona eatv chanel five. Ni kijana mzuri anaonekana ana uelewa mzuri wa mambo ila tatizo lake kubwa kama walivyo wenzake wengi wa startv ni ushabiki wa ccm usiokuwa na ulazima(sijui kama kuna mkono wa daktari anthony diallo?)hata kama ni haki yao kuwa na wanachama au washabiki wa chama chochote lakini mapenzi hayo yasiingilie au kuathiri vipindi vyao.Wakijirekebisha kwa hilo tu kipndi kitaendelea kuwa juu.
   
 14. M

  Mtembezi Member

  #14
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yahaya,

  Msijaribu kuwa neutral bali mnalazimika kuwa neutral no matter nyinyi ni wapenzi wa chama gani kwa muda mrefu mmekuwa mkijiharibia mbele ya macho ya watanzania kwa mfano wakati mko karibu na ILEMELA Mlishindwa kabisa kuonyesha hatua kwa hatua zoezi la uchaguzi lilivyokuwa linaendelea, licha ya kujigamba kila wakati kuwa mna waandishi wenu eneo hilo pamoja na Nyamagana, fun enough hata idadi ya kura na "MTU" aliyeshindwa mkashindwa kutangaza, kigugumizi cha nini? Kwa stahili ya habari zenu ni wazi mmekula yamini na STAR TV na niulize tu mtafia hapo?


  Mwandishi mmoja mkongwe alipata kunieleza hili.........WANANCHI AMBAO NI WALAJI, WATAZAMAJI NA WASIKILIZAJI WANAJUA ZAIDI KULIKO MNAVYOJUA NYINYI WAANDISHI.....Huo ni ushauri wangu kwenu!

  Mchango wangu:

  Watu hawa walioteuliwa wana kitu kipya (mawazo mapya) yatakayotusadia kutatua matatizo ya msingi ya watanzania? Je watu wanaoweza kuwa na mawazo huru nje ya mfumo wa kimafia wa CCM?


  Ni mimi Mtembezi!
   
 15. T

  The Biggest IQ Member

  #15
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mm naomba nijue sababu ya sophia simba,jumanne maghembe na mahanga kubaki katika baraza hilo kwani kwangu mm utendaji wao ulikuwa ni hafifu sana na sikuona sababu ya kubakizwa.
  watu kama prof.mwakyusa alikuwa na afadhali sana japo nae apumzike pia.
  naomba muwalete watu wa ukweli kuchambua hili sio makanjanja na mtangazaji aache kuwa bias
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  na bado lima majitu ambayo yamedanganya juu ya elimu zao...mkulo, nchimbi, nagu, lukuvi, mahanga etc hawapaswi kuwemo. we need to see watu wasio waongo kwa kiasi hicho ndipo tutawaamini.

  Nina wasiwasi na aliyepewa wizara ya mambo ya ndani, alipaswa kuwa Africa ya Mashariki na aliyewekwa Africa ya mashariki awe mambo ya ndani. Mahesabu yamekosewa hapo.
   
 17. k

  kibunda JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Note swali hili Yahya:

  Je, ni sahihi kwa JK kumteua Makongoro kuwa naibu huku ana kesi ya kujibu High Court? Pia, Sophia alifaa kurudi tena kwenye baraza?
   
 18. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #18
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shukrani wanaJF wote ambao bado mnaendelea kutoa hoja za msingi hasa kuhusiana na kipindi kijacho jumapili. Tusi-deal na individual tu-deal na hoja iliyopo mezani.

  Kila upande ulilalamika wakati wa uchaguzi inawezekana unatolea mfano kipindi ambacho ulikuwa tayari na mtazamo. Msimamo wetu ni kuwa neutral daima kama unatufuatilia vema na si kishabiki.
   
 19. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #19
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumezinagatia ushauri wenu wa wiki iliyopita. Shukrani kwa mchango wako mwanaJF
   
 20. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #20
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Point noted; shukran kwa ushiriki wako
   
Loading...