This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 16, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wazee wastaafu wa EAC wazuia magari ofisi za Hazina Dar
  *Wapiga mawe gari la serikali mbele ya polisi

  Na Fidelis Butahe

  MIGOMO na harakati za kudai haki ambazo zimekuwa zikitapakaa kwa sura tofauti nchini, jana iligeukia kwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati walipozuia magari kutoka na kuingia majengo ya Wizara ya Fedha na kulipasua kioo gari moja lililokaidi.

  Wazee hao ambao wamekuwa wakidai malipo hayo kwa muda mrefu, jana walionekana kupandwa na hasira zaidi na kufanya kitendo hicho cha aina yake.

  Baada ya kusababisha usumbufu kwa kuzuia magari kuingia au kutoka kwenye maeneo ya Wizara ya Fedha, Polisi waliitwa eneo hilo na kujaribu kuwatoa kwa nguvu, lakini ilishindikana.

  Baadaye Polisi waliamua kumwambia dereva wa gari moja aina ya Land Rover Defender kuwa apitishe gari bila ya kujali kama kuna watu barabarani. Lakini wakati dereva huyo wa gari lenye namba za usajili, STJ 6157 akijiandaa kutekeleza amri hiyo, alistukia kioo cha mbele kikiwa kimepigwa mawe na kupasuka.

  Baada ya tafrani hiyo dereva huyo alishuka kusubiri maelekezo zaidi, huku Polisi wakionekana kujirudi na kuacha kutumia nguvu.

  Tukio hilo ni mwendelezo wa wimbi la matukio kadhaa ya kudai haki ambayo yamekuwa yakifanywa kwa njia ya migomo kote nchini, ikiwemo migomo iliyotikisa nchi kama ule wa wafanyakazi wa benki ya NMB na mgomo unaoendelea wa walimu.

  "Tumechukua hatua hii kupinga kauli iliyotolewa juzi na Naibu Waziri wa Fedha, Omary Yusuph Mzee kuwa baadhi ya wastaafu ni vibarua na kwamba malipo yatakayofanyika ni kwa wale waliokuwa waajiriwa wa Jumuiya ya `Afrika Mashariki." alisema Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki.

  "Sisi hatukuja hapa kwa shari, la hasha. Tulikuja hapa kutaka maelekezo kutoka kwa Waziri kwamba atatulipaje fedha tunazodai.

  "Hizi fedha ni haki yetu kulipwa na tunachokitaka ni tume tuliyoiunda ihusishwe na wizara katika kuhakiki malipo yetu. Tukiwaacha wenyewe wanaweza kutulipa hata Sh 200 hawa".

  "Na hili tulimwambia Naibu Waziri, lakini mpaka sasa hataki kuelewa maombi haya... eti serikali inasema tumeshalipwa, labda waeleze walitulipa wapi na lini."

  Alisema kama kuna wastaafu ambao wameonekana kuwa hawastahili kulipwa basi ufanyike utaratibu wa kuwapa barua ambazo zitaeleza sababu za kutolipwa mafao yao, lakini si kama waziri alivyowatamkia kuwa vibarua hawatalipwa.

  "Unajua nashindwa kumwelewa huyu waziri. Kwanza hapa hakuna kibarua. Vibarua wa enzi zile walikuwa wakifanya kazi miezi sita sita. Hawa wote unaowaona hapa wamefanya kazi zaidi ya mwaka mmoja na nusu... huoni hii kama ni dharau," alihoji Mlaki.

  Jana wazee hao walikuwa wamekaa katikati ya barabara na kuendelea na mikakati ya jinsi ya kuendeleza harakati zao za kudai haki, ikiwa ni pamoja na kupeana karatasi ambazo zina vielelezo vinavyoeleza kiasi wanachostahili kulipwa.

  Wakiongozwa na Mwenyekiti wa vikundi vya wastaafu wa Jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki, wazee hao walitanda nje ya majengo ya Wizara ya Fedha na Uchumi, huku wengine wakiwa wamekaa katikati ya barabara na kusababisha magari yaliyokuwa yakitoka na kuingia wizarani humo kushindwa kupita.

  Naibu Waziri Omary Yusuph Mzee alishatoa tamko kuwa majina ya watakaolipwa na wasiostahili kulipwa yataanza kubandikwa leo kwenye ukumbi wa Karimjee.

  Afisa itifaki wa wizara hiyo, Cyprian Kuyava alisema wizara itaanza kubandika majina ya wanaostahili na wasiostahili kulipwa leo kwenye ukumbi wa Karimjee.

  Akizungumzia kuhusu wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, afisa huyo alisema kazi ya wizara si kukaa na wazee hao na kujadili kwa pamoja malipo yao bali ni kuwalipa pesa walizohakiki na kama kutakuwa na mapungufu katika ulipaji basi taratibu nyingine zitafuatwa.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Oct 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hii imekaa vibaya! Ni dalili ya kitu flani... What's it?
   
 3. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Isije ikawa sasa ndio fasheni, watu wakiudhika jambo wanarusha mawe!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  is somebody losing control of this nation? Kwa sababu matokeo yake ni watawala kuanza a system of suppression.... inanikumbusha kisa cha Mugabe na Matebele....
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  It is obvious, isnt it? The system is broken and there is nobody to fix it. Much more will follow unless the big joker wakes up. Pray that happens soon.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Oct 16, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,415
  Trophy Points: 280
  Duh! yaani bado hawajawalipa tu mafao yao? What is the problem?
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..sehemu nyingine huwa wanarusha kinyesi!!

  ..wanaonifurahisha ni wale wanapiga watu na keki!! kama mtakumbuka lile tukio la Bill Gates kushambuliwa.
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I hope it wont get to a situation tunakuwa termed as a failed state!
   
 9. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu,Wanazuoni husema:'When the preassure on the inside exceeds the one on the outside the end is near'
   
 10. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2008
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sasa imekuwa kwa Taifa zima na baadhi ya nyanja kandamizwa...maana zamani ilizoeleka kwa wanafunzi wa vyuo hususana Mlimani
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ....kwa kweli namuonea huruma sana kikwete..ameshashindwa kutawala......watu walikuwa wana m rate mwinyi down but ukweli ni kuwa mwinyi is far much better than kikwete.....kikwete WILL BE THE WORST PRESIDENT EVER....IN TANZANIA...

  PIA namshauri kaka yangu kikwete kuwa kwa hali ya mambo ilivyo ASISAFIRI KWENDA NJE HADI HUU UPEPO UPUNGUE.....KWA HALI ILIYOPO SASA HATA MWENDAWAZIMU ANAWEZA KUMPINDUA KIKWETE NA AKAPATA UUNGWAJI MKONO....TUTATUPUKIZA NCHI KWENYE MAAFA MAKUBWA....NA LAWAMA ZOTE TUTAMPA YEYE ALIYEKABIDHIWA JUKUMU LA KULINDA NA KUHIFADHI HILI TAIFA.....

  TUNAOMBA KIKWETE ATUFIKISHE SALAMA ...KAMA ANAONA MIAKA KUMI NI MINGI ....AISHIE MIAKA MITANO...HATUTAMCHEKA KWA HILO....KWANI KUSHINDWA NI SEHEMU YA MAISHA!!!
   
 12. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Phil usiogope sana, kwa bahati nzuri miongoni mwa watu wenye uwezo huo wa kumpindua Kikwete hakuna mwenda wazimu, na kwanza ni watu wake damdam, kwa hiyo halitatokea hilo. Mkuu wa majeshi Gen Davis Adolf Mwamunyange ni mshikaji wake tangu wakiwa jeshi. IGP Saidi Ali Mwema ni shemeji yake. DG wa TISS Rashid Othman wametoka nae mbali, tangu kabla ya enzi zake pale MOFA ambako kamtunza sana. Kwa ujumla hakuna wa kumpindua JK, uwe na amani.

  Hii ya kwake ni tofauti sana na Obote ambae aliweka mtu asiyetabirika, Idd Amin kuwa mkuu wa majeshi, amnaye hatimaye alimgeuka. JK ni mjanja zaidi, hana watu dizaini hiyo. Tatizo lililoko ni kuwa jinsi watu wanavyozidi kupungukiwa uvumilivu na kufanya fujo, ndivyo watawala wanavyozidi kupata visababu vya kutenda dhuluma kwa visingizio vya "law and order", na kama busara haitatumika hali itazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.
   
 13. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu mbona safari bado ndefu sana, kama watatumia utaratibu wao wa miaka 10 tuesabu miaka 7 ijayo ndo safari itafika mwisho.

  Bado tuna safari ndefu sana.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "Kama kungekuwa na njama hizo mtu wa kwanza kujua angekuwa ni rais mwenyewe, kwani rais ana vyombo vya ulinzi na usalama."

  Usiniulize kwa nini alikuwa wa mwisho kujua mpango wa "walevi" kujificha kichakani kumsubiri barabarani na mawe, kumuonyesha Salva Rweyemamu kwamba, badala ya mawe, wangeweza kurusha miguu ya kuku!
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Oct 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Sijui nimekuwa dhaifu ama vipi,

  Wakuu, kuna matukio ninayoyaona, kuyasikia ama kuhisi ndani ya nchi yetu yanasababisha machozi kunitiririka. Masikini Tanzania... Tunaelekea pabaya, tunahitaji msaada... I will offer my hand when needed, something MUST happen, very soon. WEWE unaweza kusaidia!

  Mheshimiwa rais anatakiwa asipuuzie mambo haya, yana maana yake... Kwa wale wenye imani nadhani wanaweza kuhisi hizi ni alama za nyakati flani. Tuliombee taifa! JK kama yuko serious asipitishe Nov 3, bila kutekeleza ahadi aliyoitoa BALAA linaweza kulikumba taifa. Watanzania wamechoka, they can't hold this anymore.

  Usanii (sijui nani mhimili wake) umekuwa mwingi sana kila idara. Kila anayejichomoza kutaka kusaidia aidha kwa kalamu ama kwa kinywa chake anafuatiliwa kama gaidi au mhaini vile wakitaka kumjua kwa undani... Mnaotumwa kufanya hivi iweni macho, mnawalinda wachache kwa maslahi ya kisiasa, yana muda mfupi... Ipo siku tu!

  Masikini Tanzania...
   
 16. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapa Salva atakujibu kuwa waliorusha mawe ni walevi, na ushahidi ameupata kwa mkuu wa mkoa ambaye pia ana "vyombo vya usalama". Kama "vyombo vya usalama" vinazidiwa ujanja hadi na "walevi" basi ni kwamba ama hivyo vyombo vimelewa kuliko yale mateja ya kinondoni, au huo ulevi wa watu wa huko Chunya ni mzuri, inabidi wakuu wa vyombo hivyo wautafute ulevi huo wawagawie vijana wao kwenye ration zao!
   
 17. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hiyo Nov 3 ina nini mkuu hebu nisaidie nielewe.

  Hata mtawala wa dola ya Roma ya kale Pater Patriae (father of the fatherland) Julius Caesar alionywa na mtabiri wake kuhusu ides of March (tarehe 15 March) akapuuza, lakini ilipofika tarehe hiyo kweli akauawa na rafiki yake wa karibu Marcus Junius Brutus.

  Hiyo tarehe kuna nini dhidi ya mkulu wetu Mwankupili II ?
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Definitely it wont come to this or anything close !! God forbid !!

  November 3rd, 2007 - President Pervez Musharraf of Pakistan declared emergency rule across Pakistan. He suspended the Constitution, imposed State of Emergency, and fired the chief justice of the Supreme Court.
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hhahahahhha I love JF, ukipata frastrustion na kazi jump into JF will sort you out
   
 20. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naona tunaelekea Ukanda wa Gaza sasa. Wapalestina wenyewe miaka nenda miaka rudi hiyo ndiyo silaha yao kuu. Israel mbali na kuwa mwandani mkubwa wa marekani na vifaa vyote vya kijeshi lakini pale Kigoma "Mwisho wa reli". Sasa 'Usalama wa Taifa' wasije wakajiona carpet mkong'oto itasaidia. Wamuulize Israel anashindwaje kumtia maganjani Palestina....?
   
Loading...