This is too much.. Wazee nao warusha mawe Hazina!

Sijui ni Mwanzo wa mwisho au ni mwisho mwishoni?!

Mwanzo wa Mwisho wa Muungwana....Hiyo haitafutika katika historia ya Tz kuwa msafara wa Rais ulirushiwa mawe. Msije kushangaa siku moja mtu akatoka na kumtandika na yai bovu wala sio siku nyingi sana....watu wamechoka na utawala wa kisanii.........
 
Tunasubili kuandaa maandamano ya kumpongeza Rais kwa kumaliza siara yake MBY salama.
 
Tunasubili kuandaa maandamano ya kumpongeza Rais kwa kumaliza siara yake MBY salama.
...Usishangae akitoka Mbeya kesho anaruka zake US au UK kwenda kusafisha macho maana vumbi nyingi sana alikumbana nayo kwenye ziara ya Mbeya....
 
I doubt if anxiety to see someone can turn into stonning the same person you were eager to see.

Kikwete and your buddies, stop pretending that you don't see what is going on. The people are angry. Your obedient servants are tired of your incompetence and corrupt leadership. If you dont change, you shouldn't be supprised to continue losing elections, even to idiots.

Jamani kama unamsubiri mtu, mawe unayakusanya ya nini?!!!. Unakusanya mawee tu kama unasubiri umpe mtu mkong'oto.

Kubwa Jinga nakubaliana na wewe kabisa!
 
I doubt if anxiety to see someone can turn into stonning the same person you were eager to see.

Kikwete and your buddies, stop pretending that you don't see what is going on. The people are angry. Your obedient servants are tired of your incompetence and corrupt leadership. If you dont change, you shouldn't be supprised to continue losing elections, even to idiots.

I am glad other people are seeing through the spin. These are the unprecedented signs of the times indicating the colossal failures and monumental negligence on the part of Kikwete's administration.

Wanasema ukila na kipofu usimshike mkono, sasa naona Kikwete kala mpaka kajisahau kamshika mkono kipofu, kipofu anashtuka.
 
Huyu rahisi wetu ataingia katika vitabu vya rekodi kwa kufanyiwa vituko na wananchi wake. Is he a worthless president? Just wondering.
 
Duh kweli Rweyemamu msanii, anashangaa nini sasa, anadhani kwa yeye kuwa na uhakika wa mshahara wake wa mwezi + marupurupu + ulinzi akiwa na sehemu nzuri ya kulala ndiyo kila mtanzania? a wapi na kwa wadanganyika wengine sivyo hivyo mambo ni tofauti can you immagine fedha hakuna za kununulia madawati lakini za kumfadhili TOSS kusimamia wizi wa kura Tarime zipo halafu eti Kurugenzi ya mawasiliano haijalisemea hili KUGUSWA TU kakutana na wanahabari, naamini hii ni rasharasha tu, mvua bado wajipange maana hali si nzuri kwa wananchi kama wanavyodhania wao.
Natoa hoja.
 
HATARI..

Lazima tukubali swala la kumshambuli mtu yoyote na hasa Rais halilubaliki.Kama kuna kitu au tatizo lolote kuna njiaa nyingi za kufikisha ujumbe na kuhoji

Lakini pia kuna maswali na mambo mengi ya kuhoji hapo kingozi aliyotangazwa kushinda uchanguzi kwa kile kilichoitwa ushindi wa kishindo na wapambe wake inakuaaje rai wake wanamchukia mpaka kifika umbali wa kumshambuli
 
Duh kweli Rweyemamu msanii, anashangaa nini sasa, anadhani kwa yeye kuwa na uhakika wa mshahara wake wa mwezi + marupurupu + ulinzi akiwa na sehemu nzuri ya kulala ndiyo kila mtanzania? a wapi na kwa wadanganyika wengine sivyo hivyo mambo ni tofauti can you immagine fedha hakuna za kununulia madawati lakini za kumfadhili TOSS kusimamia wizi wa kura Tarime zipo halafu eti Kurugenzi ya mawasiliano haijalisemea hili KUGUSWA TU kakutana na wanahabari, naamini hii ni rasharasha tu, mvua bado wajipange maana hali si nzuri kwa wananchi kama wanavyodhania wao.
Natoa hoja.

Unajuwa ukiwa raisi wa watu...Then movement yako ni rather from down up na si top down.

Halafu eti walisubiri kumwambia kuhusu mawe hadi alipofika huko anakokwenda.

Kwanini hawakumpigia simu? Ama alikuwa amelala ndani ya gari yake?

Sasa huko anakopita ni wananchi anatembelea ama miti?

Huyu Rais inakuwa vipi anafanya ziara kama Bush?

Ama hata Rais wa nje?

Kwasababu hizo haraka haraka ambazo wanazifanya kwenye ratiba yake ni kumwonyesha hali ambazo si halisi..Sasa waligunduwa anaweza kuona kwenye gazeti na angewauliza ni vipi hawakumwambia...MPENI REALITY..NA YEYE NI MUHIMU ATAFUTE REALITY KWA KUJUWA HALI HALISI YA WANANCHI HUKO MITAANI.....MAMBO NI MBAYA NA HUKU MAFISADI WANA MABILIONI WANAYAITA "VIJISENTI" NA HUKU KUKIWA NA RUMOURS KWAMBA WANAJITAPA KUWA WAO NDIYO WENYE NCHI.

Kwani JK hachungulii humu?

Kwanza alitakiwa alale hapo kijijini kwa mwananchi mmojawapo watakayemchaguwa ama popote penye ulinzi wa kutosha na si kusema mambo ya ratiba...Ratiba gani isiyokuwa ya kukutana na wapiga kura ziarani?

Nyie washauri wa JK mwelezeni ukweli na mumwonee huruma huyu mtu jamani.

Nilishawahi kusema huko nyuma urais wa Tanzania ni kazi ngumu..Wengine wanadhani ni urahisi..Mwalimu mwenyewe kama si mambo ya chama kimoja angekumbana na mengi tu...Na bado pia alikumbana na mambo mengi lakini usalama wa Taifa ulikuwa ni usalama wa chama tawala....Hivyo unawekwa kizuizini ukileta za kuleta....This is now a new era.

Watu hawajifunzi kutokana na historia...Hamkumbuki hata chini ya chama kimoja bado kulikuwa na vugu vugu la uasi na kupinduliwa kwa serikali?
Wakati huu wa vyama vingi wananchi ni wazi wataonyesha frustrations zao kwa namna nyingi ambazo hazijawahi kutokea chini ya fikra "Sahihi" za mwenyekiti wa chama chenye kushika hatamu
 
Hili la hawa Wazee aliyezembea sio Kikwete ni Mwalimu. Limekaa muda mrefu, rekodi nyingi zimepotea, waliokwisha lipwa wanadai walipwe tena kutokana mkanganyiko huu wa kumbukumbu, wengine wala hawakuwahi kuwa waajiriwa wa EAC, watumishi wa hazina nao wanatumia vurugu hii kujineemesha,.....

Bila shaka ama husomi maelezo yanayotolewa ama ni mgumu kuelewa. Jumuiya ilikufa mwaka 1977 na zoezi la ugawaji mali ulichukua miaka saba na fedha za wastaafu zililipwa benki kuu ya Tanzania mwaka 1984. Zoezi la kuwalipa wahusika lilitakiwa lianze mwaka 1985 wakati Mwalimu hayuko madarakani. Wazee walipoanza kupiga kelele kwa mara ya kwanza, Mwalimu siyo tu hakuwa Raisi bali alikwisha kustaafu kama Mwenyekiti wa CCM na serikali wakati huo iliongozwa na Mwinyi na makamu wake akiwa Malecela na waziri wa fedha akiwa Cleopa Msuya. Hili ndilo genge linalohusika na wizi wa fedha za Wastaafu. Kuna wakati Mwalimu alishtuka sana aliposikia kilio cha hawa wazee.

Mahesabu kama haya ya milioni 60, milioni 100,.... za mwaka 1977 ndio yanayofanya zoezi la ulipaji kuwa utata mtupu!Unajua nini MamaParoko, hata tunaostafu sasa hivi, hakuna anayelipwa kiasi hicho!


Mwaka 1977 dola moja ya kimarekani ilikuwa sawa na Tshs. 8.00 (nane) na makubaliano kwenye mkataba wa EAC ulisema wazi wastaafu walipwe kulingana na thamani halisi ya dola. Thamani ya dola hivi sasa ni Tshs. 1,200.00 sasa kwa aliyekuwa anadai dola mathalani $100,000.00 kwa wakati huo ungeweza ukamlipa Tshs.800,000.00 na akaridhika lakini kwa wakati huu ni wazi kuwa hata bila riba huwezi ukamlipa chini ya Tshs, 90,000,000.00.. Kweli unafikiri ni haki kumlipa Tshs. 800,000 sawa na dola $660.00. - hii ni kama unamwadhibu aliyeibiwa kwa sababu fedha zilitumiwa bila ya idhini ya mwenyewe. Kumbu kumbu zote zipo na hakuna hata moja iliyopotea, kinachofanywa ni ujanja wa wezi kukwepa uwajibikaji.

Unajua nini MamaParoko, hata tunaostaafu sasa hivi, hakuna anayelipwa kiasi hicho!

WildCard ndugu yangu, hawa hawakuwa wafanyakazi wa serikali na hizo fedha hazikuwa za serikali. Ni kama vile wewe unaaminiwa unapewa fedha umfikishie mag3, halafu wewe unaamua kuzitumia bila idhini yangu je, wewe siyo mwizi ? Kwa mfano mwingine karani wa fedha anapewa mshahara awalipe wafanyakazi, yeye anaamua kuzitumia je, si atakuwa ameiba ? Sasa kama wizi unafanywa na serikali na hata mahakama ilikwisha amua hao wastaafu walipwe kulingana na hesabu zilizokubaliwa, serikali inawajibika iwe ya Mwinyi, Mkapa au Kikwete si hoja.
 
mag3,

..kama ni mwaka 1985, basi walikuwepo Mwinyi,Warioba,na Msuya.

..Mzee Cigwiyemwisi John Malecela alikuwa benchi wakati huo.

..lakini kipindi hicho taifa lilikuwa na matatizo makubwa sana ya kifedha.

..utakumbuka ile habari ya nchi kushindwa hata kugomboa meli moja ya mafuta toka bandarini.

..kitu cha kujiuliza ni kwanini hali ya kifedha ilipotengemaa wastaafu hawa hawakulipwa?
 
mag3,

..kama ni mwaka 1985, basi walikuwepo Mwinyi,Warioba,na Msuya.
..Mzee Cigwiyemwisi John Malecela alikuwa benchi wakati huo.
..lakini kipindi hicho taifa lilikuwa na matatizo makubwa sana ya kifedha.
..utakumbuka ile habari ya nchi kushindwa hata kugomboa meli moja ya mafuta toka bandarini.
..kitu cha kujiuliza ni kwanini hali ya kifedha ilipotengemaa wastaafu hawa hawakulipwa?

Kati ya mwaka 1985 mpaka 1990 ilikuwa ni vigumu sana kulalamika na ukasikika kwa sababu ya monopoly ya vyombo vya habari. Hata hivyo mwaka 1991 ndio vilio vya hawa wazee vilianza kusikika kupitia magazeti binafsi kama Family Mirror na kiongozi wa kwanza wa serikali kutamka kwa mbwembwe kuwa serikali haitawalipa hata wakipiga kelele nama gani alikuwa ni Mzee Cigwiyemwisi John Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais. Ni yeye pia aliyekuwa kwenye ubalozi Uingereza mwaka 1985 wakati "crown Agents" wanatoa hundi ya malipo haya kwa serikali ya Tanzania.

Hata kama kulikuwepo na matatizo ya kifedha nchini je serikali ilikuwa na haki gani kutumia fedha ambazo hazikuwa za serikali na kama walikopa ni kwa makubaliano yapi. Ukweli ni kuwa huu ulikuwa wizi wa kiwango cha kutisha kinachozidi hata hiki cha EPA.
 
mag3,

..ungekuwa specific na timeline tungeweza kujua wahusika wa suala hili.

..i didnt know kwamba Cigwiyemwisi Malecela alitamka kwamba serikali haina mpango wa kuwalipa!!

..the impression i had ni kwamba probably serikali had some pressing needs, wakaamua kutumia fedha hizo, wakiamini kwamba baadaye watakuja kuwalipa wastaafu wa EAC.

..nashukuru kwa kutupa habari hii. imenifungua macho.
 
Kisa msafara wa Raisi kikwete Kupigwa mawe kinanikumbusha kisa kimoja kwenye Biblia amabapo wapagani kama mimi waliokuwa wakimpeleka Yesu kusulubiwa walimvalisha vazi la kifalme na kumwambia yeye ni mfalme wa wayahudi halafu wakaanza kumtemea mate na kumpiga vibao na mijeledi barabara mfululizo non stop.

Na Raisi Kikwete naye alipofika Mbeya wapagani wanyakyusa wa Mbeya wakamvalisha vazi la Kichifu na kumtangaza rasmi kuwa yeye ni Chifu Mwangupili halafu wapagani wanyakyusa hao hao wakamtandika Chifu huyo na mawe barabara mfululizo nonstop na msafara wake na kumfanya kuwa chifu wa kwanza wa kinyakyusa msafara wake kupigwa mawe na waliomvisha vazi la kichifu.

Hii lazima iwekwe kwenye rekodi kuwa kuna Chifu wa Kinyakyusa alishawahi kushambuliwa kwa mawe kwenye maktaba za wanyakyusa.

wapagani hawatabiriki.Siku ingine watu wakitaka kumvisha vazi la kichifu akumbuke yaliyopata Yesu akatae.


waliyompiga mawe siyo wanyakyusa.Wanyakyusa kwao ni Rungwe na Kyela. Sehemu nyingine ni wahamiaji tu. Chunya kuna makabila mengine.
 
Tujisenti,

..ukweli uko palepale kwamba amepigwa mawe.

..haijapata kutokea ktk historia ya Tanzania.
 
mag3,

..ungekuwa specific na timeline tungeweza kujua wahusika wa suala hili.
..i didnt know kwamba Cigwiyemwisi Malecela alitamka kwamba serikali haina mpango wa kuwalipa!!
..the impression i had ni kwamba probably serikali had some pressing needs, wakaamua kutumia fedha hizo, wakiamini kwamba baadaye watakuja kuwalipa wastaafu wa EAC.
..nashukuru kwa kutupa habari hii. imenifungua macho.

JokaKuu,

Mimi hili swali nalielewa vizuri sana kwa sababu nimekula miaka (lol). Kuna wakati hata wafadhili walikuwa tayari kuisaidia serikali kwa kuikopesha fedha iwalipe hao wastaafu kupunguza fedheha mradi tu serikali ieleze ilitumiaje hizo fedha. Kwa kuwa fedha zenyewe zilitumika kiajabu ajabu na katika mazingira yasiyoeleweka, serikali ilishindwa kufanya hivyo na hapo kuonyesha wazi kuwa fedha zilihujumiwa. Katika kujaribu kujikosha kuna wakati serikali ilitoa malipo ya kati Tshs. 100.00 hadi 500,000.00 kwa kandika hundi katika kile kilichoonekana kama matusi kwa wastaafu.

Serikali siyo tu imewaibia wananchi wake bali imekaidi hata amri ya mahakama kwa kutotekeleza makubaliano yaliyofikiwa. Madai ya wastaafu yamewatajirisha wezi serikalini na kinachonisikitisha ni ukimya wa bunge letu kwenye jambo hili. Kwamba wabunge wanapigana vikumbo na hao wazee huko wizarani wakifuatilia posho zao bila chembe ya huruma kwao ni dalili ya uozo ndani ya nchi na ishara ya kupotea kwa maadili. Inasikitisha.
 
Tujisenti,

..ukweli uko palepale kwamba amepigwa mawe.

..haijapata kutokea ktk historia ya Tanzania.

Historia lazima kitokee kitu kipya kama hicho.Hata hivyo kupigwa mawe si ishara ya kwamba hakubaliki maana ktk uchaguzi hakupata kuungwa 100%

Na hata ikumbukwe hakuna ktk historia yetu hakuna Rais ktk kampeni aliyevamiwa na jamaa wenye vibuyu pale jukwaani .

Kupigwa mawe ni kawaida tu yeye si amezaliwa kama wewe kwani tofauti yake na wewe ni nini sana sana tofauti iliypo ni hiyo watu kuweka kura kwa pen kwa kutick.

No more special
 
Mag3,
Ahsante kwa ufafanuzi wako wa kina kuhusu suala hili. Sina sababu ya kutotaka kulielewa hili kwa kuwa wanaohangaika ni ndugu zetu, Watanzania wenzetu. Wengi wa Wazee wetu hawa waliendelelea na AJIRA zao kwenye mashirika mapya ya UMMA yaliyoanzishwa kuchukua nafasi ya haya ya EAC iliyovunjwa na wanasiasa wetu. Kwa nini madeni na mafao yao haya hayakurithiwa na mashirika haya mapya?
 
Back
Top Bottom