This is too much, Morogoro to Mwanza 17 hours

tatizo la ajali sio mwendo kasi peke yake gari nyingi ni mbovu kuanzia matairi hadi engine, pia kuna malori yamebadirishwa kuwa mabsi kiukweli safari ya mwanza dar inakera
 
Tusiwe wepesi kulaumu bila kufanya utafiti japo kidogo, Ukisoma taarifa za vyanzo vya ajali kwa hapa tanzania asilimia zaidi ya 70 ni human errors ( mwendo kasi, uzembe wa kutozingatia sheria, ulevi na mengineyo) kwa mliosafiri karibuni mtakuwa mashahidi siku hizi hakuna tena zile ligi za kijinga Barabarani, wahenga walisema KAWIA UFIKE, Naunga mkono hatua yoyote itakayopunguza hata ajali moja tu kwa mwaka
 
Niliwahi kuendesha mwanza-Dar nimejaza kinamama full kujjamba njia nzima. Hawana msaada zaidi ya kulia njaa
 
Bola uchelewe kufika ajali zimepungua sana
Ajali zimepungua kutangazwa kwenye media

Ukiingia kwenye magroup ya wahusika hali si shwari karibia kila siku kuna ajali

Mabasi yanafanya juu chini kulinda brand
Polisi nao wamechoka kuweka mambo hadharani.
 
Me nadhani Kuna umuhimu wa kupitia sharia zetu.. wangeruhusu basi zitembee usiku kucha unatoka zako ubungo saa 1 usiku unaingiaa mwanza asubuhi tu.
Hii sheria ipite hata kesho kabisa
 
UMEPIGA NYUNDO KWENYE MSUMARI
 
Hata iwe km 10 kwa saa ni sawa tu ili mradi tufike salama atakayetaka kuwahi aanze safari mapema au apande ndege, tumepoteza ndugu zetu wengi mno watu wamepata vilema vya maisha jamani, kuna vitu vingi vinasababisha ajali laki spiidi kubwa inachangia sana ajali kuliko kitu kingine kile, mfn kama umewahi kuendesha baiskeli , pikipiki au gari ukaanguka unaweza kupata jibu hapa, ni wapi unapata ajali mbaya ukiwa na mwendo wa taratibu au spiidi ya juu. Lakini watu wanaoshabikia spiidi na kulaumu serikali kwa hili nadhani hayajawakuta ndo maana wanaona ni makosa kuweka speed limit.
 
Nauli ya Pangaboi ni madafu 230000 tu Dar to Mwanza. Muda saa 1:45 tu unaingia home. Mateso ya nini kama vyuma havijakaza? Wakati unarudi wahi tiketi mapema achana na mgongo wa chura mwendo wa kobe.
 
Dodoma to Dar? 10 Hrs! Nimekumbuka miaka ya nyuma wakati miundombinu ikisemwa kuwa haikuwa na ubora na pia ilikuwa finyu lakini tulikuwa tunatumia masaa 5! Hivi tunaenda au tunarudi?
Tunaenda coz sheria zinafuatwa. Kama hutaki panda ndege
 

Kwani ulisikia huko Marekani hakuna safari za gari za masaa 17?
 
Binadamu hatuna jema. Kiukweli polisi nawasifu kwa kusimamia sheria. Ajali zimepungua sana. Na ni kwa sababu ya kudhibiti madereva watukutu. Kila mara abiria walikuwa wanapukutika tunaambiwa in mapenzi ya Mungu.

Polisi nawasifu sana. Muendelee kukaza. Kuhusu kuchelewa barabarani basi muwe mnaanza safari mapema. Hata Kama in masaa 20 it is worth it! Plan ahead always.

Sheria zikisimamiwa vizuri in faida kwa wananchi na serikali pia.
 
Barabara zetu ni za kimasikini. Tungekuwa matajiri tusingeweka matuta tungeweka vivuko vya raia.

Matajiri hawana highway ya kupishana. Wana barabara mbili au zaidi za kuelekea upande mmoja na hakuna magari yanayokutana kama yanauelekeo tofauti.
 
Barabara zetu ni za kimasikini. Tungekuwa matajiri tusingeweka matuta tungeweka vivuko vya raia.

Matajiri hawana highway ya kupishana. Wana barabara mbili au zaidi za kuelekea upande mmoja na hakuna magari yanayokutana kama yanauelekeo tofauti.
ETI !!!!!!! TRUNK ROADS ZETU ZOTE NCHINI ZINAKIDHI VIWANGO VYA KIMATAIFA!!! ACHENI SIASA FANYENI UTAFITI HALAFU MUANDIKE
 
Na kwa viwango hivyo hivyo ndio maana mwendo ni 80 kwa 50
Hebu soma vizuri nilichoandika hapo nyuma sababu kuu ya sheria hiyo na vile vile niliwaomba mfanye utafiti ili tujue hasa tatizo nini? na vile vile ninaweka utafiti wa wataalam kuhusu ajali hizo. Hivi bado hujapata picha???? Soma tafakari halafu tujadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…