Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 87,219
- 150,525
Tuna tatizo la zaidi ya lugha, kwa sababu wengi kati ya hao wasomi hata Kiswahili hawawezi kujieleza kwa ufasaha. Mpaka viongozi wetu.
Ukienda kwenye Kiingereza ndiyo janga la taifa. Na kama ni mtu ambaye maisha yako hayahusiani na matumizi ya Kiingereza, labda hili linaweza kuwa si muhimu, lakini kama umesoma angalau kwenye shule za sekondari basi ni muhimu.
Nakumbuka tulivyokuwa sekondari Tambaza tulikuwa tunazungumza Kiingereza hata nje ya darasa kwa nia ya kujifunza, wengine waliona ubishoo. Leo nimekuja kugundua kwamba ule utashi wa kusoma vitabu vya Kiingereza na kuzungumza lugha hiyo umenisaidia sana katika kazi zangu za kimataifa.
Leo hii Mtanzania akiandika Kiingereza cha "The Economist", "The New York Times" au "The Wall Street Journal" (publications I subscribe to) anaonekana anaandika lugha ya ajabu.