This is Rostam I know... The Story Behind the Man

This is Rostam I know... The Story Behind the Man

Rostam ndio baba wa kina JK na wengineo wote ndani ya ccm. Hakuna hata mmoja mwnye nguvu ya kumtosa
 
Huyu alinunua kiwanda cha ngozi kule Morogoro halafu alikuwa na kampuni ya African Trade pale PUGU Road ambayo kasheshe wewe'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
 
Mwanasheria wa serikali , fredrick werema amesema dowans ilisajiliwa costa rica na rostam alipewa nguvu ya kisheria kumiliki.
Sasa kwa nini watu wanataka serikali imutaje mumiliki wakati werema amemtaja?
 
Ni kwa nini serikali/prosecutors wanapata kigugumizi kuwafikisha mamiliki wa Dowans mahakamani kwa Fraudulent Misrepresantion ya KAMPUNI YAO Kwamba kampuni yao Richmond/Dowans ina uwezo wa kufua umeme wakati uwezo huo haikuwa nao?
 
Wana Jf na watz wote kila siku tunaona kuongezeka kwa mateso na adha toka mtu huyu mmoja. Ana mkono wake kila ilipo shida ya mtanzania. Kwanza yeye hajulikani alikotokea na kuanza kuikamua nchi hii si Richmond, si Kagoda si usimamiaji wa siasa mbovu za kizandiki zilizojaa uonevu si utoroshaji wa mali za nchi. hivi kweli nchi yenye watu milion zaidi ya 40 hakuna lolote tunaloweza kufanya tuendelee kutekwa na ufisadi wa mtu 1? Wake up Tanzanians sisi si dhaifu kiasi hicho bwana....
 
ukitaka kujua rostam ana uzito wa tani ngapi, angalia rafiki zake
 
Analingana na mawe ya Piramidi za Misri, kwani alikuja hata tanzania kimiugiza, akwa wakala wa ngozi Iran na sasa ni wakala wa Uranium Iran na mbunge Mkuu wa mafisadi Tanzania akifuatiwa bigwa wa Mikataba Mibovu Tanzania Mkono mzee wa Musoma
 
Mkuu wewe kwani siyo mtanzania? hivi hujui kuwa Rostam Aziz ndiye rais wa nji hii?Nafikiri nimekujibu.
 
RA ni king maker, ndiye aliyemuweka muzeiye pale magogoni, ndiye aliytoa Msekwa kwenye uspika na kuimuinua SS na kumpatia usipika, ndiye aliyemtosa SS kurejea kwenye uspika baada ya kumfanya mbaya El. Ndiye aliyemshawishi Mama Makinda kumchallenge bosi wake. Ndiye mmiliki wa vodacom, kampuni ya simu za mkononi yenye mtandao mkubwa kuliko humu nchini. Ndiye mmiliki wa Caspian Construction, kampuni host ya Richmond na Dowans.
Ndiye mbunge ambaye katika bunge lililopita, hakuuliza swali lolote, hakuchangia hoja yoyote bungeni, na ni miongoni mwa wabunge wawili wenye kumiliki ndege zao ndogo zikiwapeleka pale bungeni Dodoma na kuwasuburi kuwahi kwenye madili yao.

Pia ndiye mmiliki wa magazeti ya Rai Dimba na Mtanzania na major share holder wa Chanel Ten na Magic Fm kupitia partner wake Tanil Somaiya wa deal ya rada na gulf stream
 
rostam, mkwere na lowasa ni wa3 ndani ya moja kama ilivyo utatu mtakatifu wa mungu baba,mwana na roho mtakatifu.
 
Ndugu muuliza swali, napenda kukujuza kuwa:

Rostam Aziz ni muhimili wa nne wa nchi yetu.

Kama ulikuwa hujui, napenda kukufahamisha kuwa, Tanzania, baada ya mihimili mitatu uijuwayo, ina mhimili ujulikanao kwa wenye werevu, na huu ndio nnao kufahamisha leo!

Muhimili wa nne wa nchi yetu, kwa kifupi tunauita SYSTEM! Sasa kama unataka kujuwa zaidi kuhusu system, tutakueleza.

System ina idara nyingi na nyeti na si lazima uzijuwe au zijulikane na kila mtu, na kadri zinavyokuwa hazijulikani na wengi ndio zinaweza zikafanya kazi zake vizuri na kwa uafanisi wa kiwango cha juu.

Baadhi ya watu uwajuao ambao wapo kwenye system na kila mmoja ana majukumu yake na ana shughuli zake na ana report kwa ajuavyo yeye mwenyewe ni:

Mbowe
Slaa
Kabwe
Lipumba
Mrema
Marando
Rostam
Rashid H.
Rashid I.
Zakaria
Dewji
Patel

Nadhani hao wanakutosha kwa leo. Na hizo kampuni unazozikia zipo kwa maslahi ya Taifa. Amini usiamini.

Kama una swali la ziada, uliza tu!
 
Tani 7,948.
Je kuna crane ya kumnyanyua? Madesigner hawajafanikiwa kuitengeneza.
 
hahahaha MR Rostam Aziz....me ni Anti CCM Lakini huyu mbwenga kwa kweli hata mimi nina gadhabu naye sana tuu!...hapa nipo ninamfanyia mahesabu ...kama nyie wote hamuwezi nitamuingilia mwenyewe kama Osama Bin Laden....
 
Wana Jf na watz wote kila siku tunaona kuongezeka kwa mateso na adha toka mtu huyu mmoja. Ana mkono wake kila ilipo shida ya mtanzania. Kwanza yeye hajulikani alikotokea na kuanza kuikamua nchi hii si Richmond, si Kagoda si usimamiaji wa siasa mbovu za kizandiki zilizojaa uonevu si utoroshaji wa mali za nchi. hivi kweli nchi yenye watu milion zaidi ya 40 hakuna lolote tunaloweza kufanya tuendelee kutekwa na ufisadi wa mtu 1? Wake up Tanzanians sisi si dhaifu kiasi hicho bwana....


Unamwulizia Rostam yupi? Je ni huyu aliyemwajiri Kikwete?
Kama unamwulizia huyo please shut up your mouth? Vinginevyo unaweza kusabisha JK akafukuzwa job.
 
hahahaha MR Rostam Aziz....me ni Anti CCM Lakini huyu mbwenga kwa kweli hata mimi nina gadhabu naye sana tuu!...hapa nipo ninamfanyia mahesabu ...kama nyie wote hamuwezi nitamuingilia mwenyewe kama Osama Bin Laden....

Rostam na wanasiasa wanaomsupport yeye wanajua kuwa WaTZ hawana ujasiri wa kufanya chochote hata kama wangenyimwa chakula na kulazwa nje. Angalia mambo wanayofanya wanasiasa na mahakama zetu ndio utajua kuwa wanasiasa wanawafikiriaje waTZ. Hukumu ya kuendesha kizembe kwa yule mheshimiwa sana ni laki saba... gari yenyewe ilikuwa haina insurance - technically, familia ya wale marehemu wangeweza kum-sue mbunge wetu na wakashinda kupata fidia kubwa tu. Just imagine, kama hao waliouwawa kwenye hiyo ajali wangelikuwa dada zako ungefanyaje? Angekuwa mlalahoi anaendesha hilo gari hukumu yake ingekuwa kifungo cha miaka mingi. Kule Vunjo mwenyekiti wa kijiji na brother wake wanachomewa nyumba moto serikali haisemi hata neno moja kwa sababu waliochomewa nyumba sio mtu wa CCM. Wananchi badala ya kupiga kelele wanaamua kuchanga wao wenyewe kuwajengea nyumba. Kova anawanyima watu kuandamana kwa amani lakini waTZ wanakaa kimya. Mambo kama haya yako mengi. WaTZ wanajulikana kama watu ambao wanaongea sana lakini hawafanyi chochote. Wanasiasa wanajua kuwa scandal yeyote wakiikalia kimya kwa muda mfupi waTZ watasahau na wao wataendelea kupeta. It's a joke. WaTZ tunajiridhisha kuwa ni muhimu kuishi kwenye so-called "nchi ya amani" na wanasiasa wanajua huo umbumbumbu wetu kwa hiyo wanaendelea kutuumiza with impunity. At some point, one of us is going to have to make a sacrifice and do something that will make a statement lakini mpaka muda huo utakapofika waTZ tuendelee kuumia tu.
 
Richmond/Dowans; Matokeo Ya Unyonge Wa Mtanzania

28 December 2010

Mwishoni mwa mwaka jana, gazeti moja nchini liliandika habari zenye kichwa, “Giza Nene” kuhusu sakata la kampuni moja “bandia” ya Amerika ya kufua umeme wa dharura nchini
Tanzania. Wote tunaijua kampuni hii. Na mmojawapo wa wakurugenzi wake, Naeem Mohammed, sasa kafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusema uwongo na ufisadi!

Wengi wetu bado tumo katika “giza nene” la sakata la Richmond kwa kutoelewa tunazungumzia kampuni zipi! Sijui ni makosa ya vyombo vya habari. Tusomapo au tusikilizapo habari kuhusu sakata hili, yaonekana kuwa kuna kampuni sita zinazotajwa tajwa (mbali na kampuni mbili za Dowans (Afrika Kusini na Tanzania):

Richmond Development Co. (RDC); Richmond Development Corporation (RDEVCO);

Richmond Development, LLC.; LLC.; Richmond Tanzania Limited; na Richmond Development (Tanzania), Ltd.

Kwahiyo, kabla ya kuelewa “giza nene” lililotangazwa na gazeti hilo, ingekuwa vizuri tusaidiane kuliondoa. Tubakie na kampuni mbili za awali. Nionavyo, kuna kampuni mbili tu.
Moja, ni kampuni tanzu ya utata ya Richmond Development Company of Houston (RDEVCO) iliyojidai kusajiliwa huko Houston, Texas, na kampuni-toto ya Richmond Development
Company Tanzania, Ltd. iliyosajiliwa nchini Tanzania, pia kwa utata. Wakati mwingine yaandikwa kama Richmond Development Company (Tanzania), Ltd. Hii ina maana kuwa ni
“extension” ya kampuni tanzu ya huko Houston!

Kampuni iliyosajiliwa huko Houston, Amerika, ilijulikana kwanza kama Richmond Development Corporation (RDC). Lakini sasa yajulikana kama Richmond Development Company of Houston (RDEVCO). Kampuni hii iliundwa na mmoja wa familia ya Gire ya huko Houston, Mohamed S. Gire. Hao akina Gire ni Wahindi wa kutokea Tanzania!

Akina Gire hao Bwana Mohamed S. Gire (Alim Gire) wana kampuni ya ki-familia yenye kuchapisha na kurudufu “nyaraka” ijulikanayo kwa jina la Richmond Printing Company.

Bwana Mohamed S. Gire (Alim Gire) ni Chief Executive Officer). Wengine ni ndugu zake:

Samad Gire (Vice President, Business Development), Javeed Gire (Manager), Zahoor Gire (Vice President Finance), na Imad Gire (Vice President Operations). Dada zao wawili
wanaishi nchini Uingereza, ambako baba yao alikwenda kuishi, kama mfanyabiashara.

Anwani:

Richmond Printing L.L.C. ni 5825 Schumacher Lane, Houston, Texas 77057.

Kampuni zote mbili, Richmond Printing Company na Richmond Development Company of Houston (RDEVCO), zinatumia fax moja: (713) 952-0932-5825. Hii ina maana kuwa kampuni hizi mbili zinatumia, pengine, jengo moja.

Tovuti ya mwanzo ya Richmond Development Corporation ilionyesha historia ya habari za Gire kuhama Chicago kwenda Houston kuanzisha kampuni ya kurudufu nyaraka (“copying
centre”) iitwayo, Richmond Printing Company, mwaka 1985. Pia kulikuwa na habari nyingi za michango ya Bwana Mohamed S. Gire ya takrima na kutunisha mfuko wa kampeni za Democratic Party (“political campaigns contributions”) kwa House of Representatives.

Inaonekana kuwa Richmond Development Corporation (RDC) ilibadili jina na kuitwa Richmond Development Company (RDEVCO). Lakini sasa vyombo vya habari vinaitaja kama
Richmond Development, LLC. Na mara nyingine inatajwa tu kama LLC.

Je, Richmond Development Corporation (RDC) au Richmond Development Company (RDEVCO au LLC ilijuaje kuwepo kwa makaribisho ya zabuni za kufua umeme wa dharura na hali wako huko Texas, Amerika? Nafikiri kuwa huyo Mohamed Gire wa Marekani alipata kujua uhondo wa tenda hiyo kutokana na “dugu” yake Naeem Gire wa Dar es Salaam!

Alichofanya Mohamed Gire ni kuunda kampuni uchwara ya Richmond Development Corporation (RDC) na kumkaribisha mtu mwingine aliyebobea katika utalaamu wa ki-biashara, Dr. Mohammed S. Huque, (mwana-uchumi m- Pakistani/m-Amerika), ambaye ni Mkurugenzi-Mwenza wakiwakilishwa na REX ATTORNEYS hapo Dar ambaye mmoja partners wao ni Balozi Mwanaidi Maajar Sinare.

Na kuna habari za kuaminika kuwa hao akina Gire (Mohamed na Neem) na huyo Dr. Huque walikuwamo katika tenda nyingine yenye utata ya kujenga bomba la kusafirisha mafuta
kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Na hata tovuti yao iliwahi kuandika kuwa kati ya miradi iliyotekelzwa ni ujengaji wa bomba la mafuta katika mojawapo ya nchi zinazoeendelea.
Na kuna habari kwamba huyo Naeem wa Dar es Salaam, alikuwa pia na u-wakala wa kuuza majumba ya serikali! Ndio kusema kuwa yupo karibu karibu na baadhi ya “vigogo” na “wakubwa” wa serikali na chama chao tawala, CCM.

Kufuatana na mantiki hii, huyo Naeem Gire wa Dar es Salaam ndiye aliwaatarifu hao ndugu zake wa Houston, Texas, kuweko kwa tenda ya kufua umeme wa dharura, kutokana na ukame uliokithiri ufauji wa umeme kwa kutegemea maji ya mabwawa yetu.

Baada ya Richmond Development Company (RDC) kupewa hiyo tenda, huyo Naeem Gire wa Dar es Salaam alisajili upesi upesi kampuni nyingine ya Richmond Tanzania Limited
au Richmond Development (Tanzania), Ltd. kwa ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (Brela), “…Julai 13, 2006 ikiwa ni mwezi zaidi ya mmoja baada ya
mkataba huo kusainiwa, ikiwa na wanahisa wawili ambao ni LLC na Naeem Gire.”

Cha kutatanisha ni kuwa Kampuni hii ya Richmond Development Company inabadilikabadilika. Kama nilivyotaja hapo awali imebadilika na kupewa jina la Na sasa jina linalotumika ni la Richmond Development Company, LLC. Na hapo juu bwana Naeem Gire anakiri kuwa jina la kampuni ni “…LLC…”, kama alinukuliwa vizuri!

Ukweli ni kwamba Richmond Development Company au Richmond Development Company of Houston (RDEVCO) au LLC haina na wala haitengenezi hizo mashini za kufua umeme (turbines)! Ni kampuni ya u-wakala tut u chini ya Mohamed A. Gire (m-biashara Mhindi m-Tanzania/m-Amerika na Dr. Mohammed S. Huque, (mwana-uchumi m-Pakistani.m-Amerika).

LLC si jina la kampuni; ni kifupi cha maneno ya Kiingereza, “limited liability company”, sawa na neno tulilozea la “limited”, au kwa kifupi, “Ltd”! Kwahiyo, badala ya kuandika Richmond Development Corporation, Ltd. huandikwa Richmond Development Corporation (LLC)!

Usajili wa kampuni ya LLC. au Ltd. ni uchu wa u-nyang’au Yutaka kunyonya kwa kujikinga ki-sheria endapo itafikishwa mahakamani kudaiwa! Au isihitajike ki-sheria kuwataja wenye
hisa wake! Kama wenye hisa hizo ni “wakubwa na vigogo” wa Tanzania, twafa!

Katika hali ya utata, Richmond Development Company of Houston (RDEVCO), au kwa kifupi, RDEVCO, ilijitoa katika tenda hiyo ki-siri siri na kuirithisha kampuni ya Dowans.

Tulielezwa kuwa kampuni hii ya Dowans ni ya mojwapo ya nchi za ki-Arabu huko Mashariki ya Kati! Lakini sasa yajulikana kuwa Dowans Holdings SA ni ya huko Afrika Kusini! Baadaye, kama walivyofanya kuhusu Richmond Development Company Tanzania, Ltd. waliunda kampuni nyingine ya Dowans Tanzania, Ltd. Pengine, ni janja tu ya “danganya toto”; ni wale wale!
Richmond Development Corporation (RDEVCO) = Dowans Holdings SA; na Richmond Tanzania, Ltd. = Dowans Tanzania, Ltd.
Sakata hilo limesababishwa na unyonge wa m-Tanzania katika kufua nguvu za umeme/nishati, kwa upande mmoja, na uchu wa u-nyang’au wa walalaheri, kwa upande mwingine,
wanaokula njama na ma-wakalakuichoma na kuiangamiza nchi yetu kwa maslahi yao na watoto wao!

Kuna mengine yaliyofichwa na Tume ya Bunge, chini ya m-Bunge Harrison Mwakyembe (CCM-Kyela Magharibi). Na cha kushangaza ni kwamba TAKUKURU haikuona cha ufisadi katika sakata hili!

Awali kwenye tovuti yao “Richmond” waliandika kuwa miradi yao ni pamoja na kujenga bomba lenye urefu mkubwa la kusafirisha mafuta katika nchi moja inayoendelea. Nafikiri
hili bomba ni ule mradi waliokuwa wameukania wa kujenga bomba la mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Lakini sasa maelezo hayo yamefutwa na badala yake wanajidai, In 2006, we completed the Ubungo Emergency Supply Power Plant Project in Dar es Salaam, Tanzania. We provided
full project development and engineering, procurement and commissioning (EPC) for the first 25MW, and all preparatory work for the second phase, of a 100MW ISO gas-based
generation plant.”

(Tafsiri yangu: Mwaka 2006 tulitekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa Dharura wa Ubungo, Dar es Salaam, Tanzania. Tulikidhi yote ya mradi huo ikiwa ni pamoja na uhandisi, kununua
na kuweka mashini za kufua umeme wa 25MW, na matayarisho ya awamu ya pili ya mitambo ya gesi yenye uwezo wa kufua umeme wa 100MW ISO.)

Katika ripoti ya Mwakyembe au ya TAKUKURU, hatukusikia mchakato wa Ofisi ya u-Balozi wa Tanzania nchini Amerika! Maafisa wa juu u-Balozi wetu huo waliandikwa wakisifiwa kutokana na utekelezaji wa sera mpya ya ki-balozi (“new economic diplomacy”) iliyokitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa zamni, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, wakati wa Awamu ya Tatu.

Balozi na Msaidizi Mkuu wake walijua (na wanajua wazi) matayarisho ya Mohamed A. Gire katika kufanikisha mkataba huo wenye utata. Bwana Mohamed A. Gire aliwakaribisha ma-
Balozi wetu hao kumtembelea na kuzuru Houston, Texas! Si ajabu, pengine, aliwalipia nauli na mahali pa kulala hapo Houston!

Wa-Tanzania wa huko Houston wengi walifikiria kuwa Balozi na Msaidizi Mkuu wake walikwenda huko kuwatembelea wao! Soma taarifa ya habari zilizopokelewa na kuandikwa na ripota wa Guardian (ippmediaonline ya 2003-08-19 10:21:22). Sijui chanzo cha habari hii; pengine, kilikuwa ni sehemu ya Idara ya Habari na Utangazaji ya Ofisi ya Ubalozi wa Amerika nchini Tanzania, u-Balozi wee nchini Amerika au kutoka huko Houston, Texas.

Zaidi, habari zilizoandikwa na mojawapo la magazeti ya nyumbani, THISDAY, ziliwahi kueleza kwa undani na kuyataja majina ya walioshiriki katika tenda ya ufisadi wa Richmond
wenye mtaji wa shilingi karibu milioni 173-!

Sakata la ufisadi wa Richmond, lilitangulia ujio wa Rais Bush wa Amerika, likiongezea kutonesha kidonda cha wa-Tanzania waliposikia kuwa kampuni ya Richmond Development
Company (LLC) ikitamka kuwa iliingia mkataba na serikali ya Tanzania wenye thamani ya dola za ki-Amerika milioni 83. Lakini serikali ilitamka kuwa kondrati hiyo ilikuwa na thamani ya shilingi bilioni 172.9/-.

Richmond Development Company (LLC), ilikataa kata ikisema kuwa haijapokea na kwamba hakuna hata mfanyakazi wake hata mmoja amewahi kulipwa “ki-jisenti” kimoja kutoka serikali ya Tanzania au afisa wake (“a single penny from, or paid a penny to, the government of Tanzania or any of its officials.”)

Wa-Tanzania walibaki wakijiuliza maswali mawili muhimu:
Moja, je, “sirikali” imekuwa ikimlipa nani kiasi cha dola za ki-Amerika 140,000 elfu, kila siku!

Mbili, kwa nini Richmond Development Company (LLC) haikusitisha mkataba endapo ilikuwa haijapokea malipo yeyote kutokana na kukamilisha kazi iliyopewa? Kwani kwenye tovuti
yake, Richmond Development Company (LLC) inautangazia ulimwengu, kama nilivyonukuu kwa Kiingereza hapo juu, kazi iliyotakiwa kufanywa na kumalizika.

Huyo ndugu ya Mohamed A. Gire aliyeko Dar es Salaam (Naeem Mohamed) anajua zaidi makubaliano hayo ya ki-biashara! Na pai anawajua wenye hisa katika kampuni zote mbili.

Ni lazima mahakama ikaze nati kwake!

Huenda, huyo Gire wa Dar es Salaam anao “insiders” wake katika Tanesco au/na Serikali!

Huenda, huyo Naeem Gire wa Dar es Salaam yu karibu karibu na “vigogo” na “wakubwa” fulani wa serikali ya Tanzania na chama chao tawala ambao ni walikuwa ni wana-hisa katika
Richmond Tanzania Ltd. au wenye hisa katika Dowans Tanzania Ltd!

Hao “vigogo” na “wakubwa” ndio waliomkaribisha Naeem Gire kuvua tenda! Labda, katika uchu wa u-nyang’au, waliunda kampuni ya siri siri, bila kuwataja rasmi wenye hisa katika
kampuni hiyo ya Richmond Development Corporation (Tanzania), Ltd. Na hapo baadaye kwa siri kubwa wakaunda kampuni ya maficho (“offshore”) ya “ki-fisadi” na kuisajiri huko
Mauritius ili wasilipe kodi kwa Tanzania au Afrika Kusini – kampuni ta Dowans!

Kuna wana-habari wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiandika juu ya ufisadi na maingiliano ya siasa na biashara. Kuna misamiati mipya inayosimulia mwingiliano
huo, “ubiasharishaji wa dola na usiasishaji wa biashara”.
Mwandishi Padre Karugendo wa RaiaMwema aliwahi kuandika akionya, “Michakato hii miwili, yaani ubiasharishaji wa dola na usiasishaji wa biashara inaendelea hapa Tanzania hivi sasa chini ya utawala wa CCM. Ni mfumo ambao umeshika kasi kiasi cha kutisha…”

Zaidi, Padre Karugendo, akiandika juu ya nia nzuri ya “(u)binafsishwaji wa mashirika ya umma”, Padri Karugendo alijutia sera hizo: “…wananchi hawakuelezwa bei za kuyauza
mashirika hayo ambazo hazikufanana na bei za soko zililikuwapo wakati huo. Bei zilikuwa chini kwa kiwango kikubwa mno.”

Makala hiyo ya Padre Karugendo iliendelea kuelezea kile kinachowashangaza wengi.

Aliandika:
“Baadhi ya kampuni zilizobinafsishwa zilinunuliwa na mawaziri na watumishi wa Serikali wa ngazi za juu kupitia makampuni yao au yale waliyokuwa wana hisa ndani yake. Maana yake ni kwamba bei zilipindwa ili kuwapendelea.

Zoezi hili liliwasaidia viongozi wa Serikali kupata mitaji. Watu hawa walikuwa na nyumba zao, na wengi wao wakawa wamesipangisha na kukaa katika nyumba za Serikali. Ukarabati
uliofanyika kwenye nyumba hizi unaonyesha kwamba zinatumiwa kama dhamana ya mikopo, maana ziko katika maeneo yenye thamani ya juu.”

Je, pengine hiyo ndio sababu ya baadhi ya ma-Waziri na hata Rais wa Awamu ya Pili na ya Tatu kujiingiza katika mambo ya biashara! Kulikuwepo na mtindo wakati wa Awamu ya Tatu
ya Rais Benjamin Mkapa kwa baadhi ya “vigogo” na “wakubwa” wa chama tawala na serikali yao kukamata vya umma shauri ya uchu wa u-nyang’au wao, ili usemi “Chukua Chako Mapema”, utimie hivi, mithili ya unabii!

Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Ernest Nyanda (marehemu) wa Awamu ya Kwanza, Pili na Tatu alisemekana aliunda kampuni yake ya Victoria Marine Passenger Transport Services
Ltd. na kukopa pesa za EPA kununua meli ya “mv Zahara”, ambayo utata wake, sijui, umeishia wapi!

Waziri Nizar Kamaragi naye kaunda kampuni ya “ukuli” (Tanzania International Container Terminal Services (TICTS), hapo bandarini, ambayo inazidi kuleta utata wa ki-upendeleo.

Naye aliyekuwa “amiri jeshi mkuu” wa wizara zote, Rais Benjamin Mkapa, mkewe pamoja na Waziri Yona walinunua kampuni ya umma kwa bei ya “karanga”! Ofisi ya kampuni yao
ilikuwa hapo Ikulu. Si ajabu hiyo ofisi ilikuwa ndiyo “maktaba binafsi yake” iliyoungua kwa pasi wakati “amiri jeshi mkuu” akiwa safarini huko Masasi nje kabisa na hapo Ikulu!

Hivi hawa viongozi wa serikali wanapata wapi muda wa kuhudumia hizo kampuni zao
binafsi na hali wakiwa bado wafanyakazi wa serikali! Pengine, ndio maana hawana muda wa kutosha wa u-nahodha wa “mitumbwi, meli na ndege zetu”. Sio viongozi wa serikali tu
kuna, pia, viongozi wa chama tawala ambao ni ma-Waziri na wafanyabiashara binafsi!

Je, wanatumia wakati wa umma kujinufaisha? Je, wanalipwa mshahara kwa kufanya kazi za umma na huku wanatumia muda huo huo kushughulikia maslahi yao binafsi? Wakati wa
Azimio la Arusha majambo haya hayakuwezekana!

Ilituweze kuondoka na “ubiasharishaji wa dola na usiasichaji wa biashara”, ambako kunaangusha taifa letu, mwandishi mwingine wa Raiamwema Ayubu Rioba aliwahi kushauri:

“Tunahitaji fikra mbadala kutuwezesha kupunguza vifo vingi visivyo vya lazima katika nchi yetu; vifo vya kifikra (vinavyodhihirisha ujuha wetu katika mikataba mibovu,
wizi wa BoT, Richmond, mtambo wa kuonea ndege, ndege ya rais, n.k.) na vile vya kimwili kama tunavyoendelea kuvishuhudia kwa majonzi kila kukicha.”

Kusema kweli waliotia saini mkataba huo ni kampuni ya Richmond Development Corporation (LLC) na Tanesco! Katika mikataba mingi kati ya Tanzania na wawekezaji wa nje kuna
kifungu cha PSA (Production Sharing Agreement): Mfano, mwekezaji kubaliwa A anaweza kushirikiana na mwekezaji mwingine mpya chaguliwa B katika mkataba uliosainiwa na
mwekezaji A, endapo ataiarifu na kupata idhini ya serikali ya Tanzania.

Ukiangalia makampuni yaliyokwishajiingiza katika mikataba mingi ya awali baina ya Tanzania na wawekezaji wa nchi za nje, utagundua msululu wa makapuni mapya ya PSA, kwa mfano, mikataba ya migodi ya madini na gesi. Ndio maana ingawa Rais Jakaya Kikwete aliamuru mikataba mingine mipya isisainiwe hadi hapo Tume ya Jaji Bomani itakapopitia na kutoa riporti yake kwa serikali. Bado tunayangoja hayo ya Utekelezaji wa Ripoti ya Jaji Bomani! Lkini kila mara mikataba ya PSA mipya inafunguliwa na kutiwa saini.

Ukiachilia mbali hayo ya Tume ya Jaji Bomani, si siri kwamba makampuni ya madini ya dhahabu na gesi yamekuwa yakiongeza wawekezaji wapya, kupitia PSA, na serikali ya Tanzania kuridhia makubaliano hayo bila kizuizi chochote.

Napenda sana PSA imulikwe wazi. Makampuni ya migodi ya dhahabu, almasi, nickel na uranium, na visima vya gesi na mafuta huingiza wawekezaji wapya kupitia PSA hususan
pale ambapo serikali yetu huwapa hao wawekezaji kumiliki maliasili yetu kwa 100%!

Inakuwa ni mali yao; na wanayo haki ya kuigawa mali hiyo kwa wale wawapendao. Kwani kila mara huwa ni wageni tu wanaoruhusiwa kutumia kipengere cha PSA! Pengine, wazawa
nao huwa ni sehemu ya siri siri! Je, hii ni janja ya “vigogo” na “wakubwa” wa serikali na chama chao tawala kuweza kupata lolote kutokana na uhondo huo?

Nashauri kuwepo na u-wazi wa kuhusu si makampuni mapya yaliyojiingiza kupitia PSA bali pia uwazi wa kuhusu wazawa wapi walio na hisa katika makampuni hayo. Kwa nini nashauri
hivyo? Mambo matatu ya wazi yanayozalisha “vi-ji-senti”.
Moja, ni utata wa kampuni ya Richmond Development Corporation (LLC), ambayo mambo yaliyojitokeza yalifunua shinikizo la “vigogo” na “wakubwa” wa serikali kukiuka ushauri wa wataalmu wa Shirika la Tanesco! Sio ajabu, “vigogo” na “wakubwa” wa serikali na chama chao tawala wana hisa katika Kampuni ya Richmond Development (Tanzania) Ltd!

Na sasa kampuni hii inawalinda kwa kutolopoa ni akina nani wana hisa katika kampuni hii licha ya Naeem Gire!

Mbili, Mheshimiwa m-Bunge “kijana” Zitto Kabwe (CHADEMA Kigoma Rural) alikuja na tuhuma dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi kukimbia huko London hima na kusaini mkataba eti akiwa hotelini na kampuni ya migodi ya dhahabu ya Barrick huko Buzwagi! Pengine, Mheshimiwa Waziri wa Umeme na Nishati Nizar Karamagi alitia saini yake kuridhia tu mkataaba wa awali wa Barrick kwa kupitia mapatano ya PSA!

Tatu, aliyekuwa Waziri wa Umeme na Nishati Bwana Nizar Karamagi, huyo huyo, ana pia kampuni yake ya “ukuli” hapo Bandarini. Sijui naye aliiunda lini? Pengine, alijua kuwepo
kwa PSA. Hivyo, kaiunda kampuni hiyo, ambayo hatuwajui wenye hisa, na hapo baadaye Rais Benjamin Mkapa kuiongezea muda wa kumiliki “ukuli” hapo bandarini kutoka miaka 15 hadi 25 bila kibali rasmi!

Tunaambiwa kuwa Tanzania iliingia mkataba na kampuni moja ya Houston, Texas, Amerika, ya Richmond Development Corporation, LLC. yenye kuzalisha au kufua umeme wa dharura
kutokana na ukame uliosababisha mabwawa yetu ya maji kutosetri kuzalisha umeme.

Wamiliki wa Richmond Development Corporation, LLC. Ndio walikuwa na 100% za hisa za kampuni hii. Lakini cha kushangaza ni kwamba “wamiliki’ fulani walipoona uhondo upo katika mkataba huo, waliunda kampuni yao ya Kampuni ya Richmond Tanzania LTD na kuisajili “mwezi zaidi
ya mmoja baada ya mkataba huo kusainiwa. Wana hisa wa kampuni hii ni LLC na Naeem Gire, kulingana na habari rasmi tupatazo, kama ifuatavyo: “(k)atika mchanganuo wa hisa,
Gire ana miliki 250,000 na LLC 750,000 huku ikianza na mtaji wa Sh1,260,000,000 (1.2 bilioni).”

Je, si huyu huyu “mfanyabiashara” aliyeshindwa kabisa kuweza kupata mapesa ya kusafirishia mitumba yake hadi hapo serikali yetu ilipoingilia kupia Tanzanian Rural Development Bank (TRDB) – ambayo kwa bahati mbaya ofisi yake ya Barabara ya Lumumba iliungua moto!

Halafu kukaja ya Waziri “Vi-ji-senti”! Kauli ya Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge (aliyejiuzulu) kuita dola za ki-Amerika milioni moja (pengine, hongo) anazotuhumiwa
kuzificha Ulaya, kuwa ni “vi-ji-senti” ilitingisha muktadha wa lugha toka “semantics, pragmatics (logic)”, “linguistics” hadi “semiotics”! Waziri Chenge alieleweka! Waziri wetu
huyu alipaka matope hali halisi ya walalahoi wa Tanzania! “Kiongozi” huyu alijikweza!

Kiongozi huyu alikiuka kiapo chake!

Miktadha ya “diminutive or miniature” (kupunguza hadhi na thamani) katika lugha za Kisukuma, Kiswahili na Kiingereza si tofauti. Hivyo, ki-lugha Bwana Chenge alitupiga
chenga za kuibia! Kimanufaa, kwetu komputa ya laptop ni komputa tu kama ile ya zamani iliyokitumia “punch card! Kimanufaa, kwetu kiselula ni simu tu sawa na zamani
ya kuzungusha kwa mkono! Kimanufaa, kwetu sisi “vi-ji-senti” vipatavyo milioni moja (kwa dola za ki-Amerika) ni dola za ki-Amerika milioni moja hata kama Bwana Chenge ataziita “vi-ji-senti”!

Zaidi, Bwana Chenge mwanasheria wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam (Tanzania) na Harvard (Amerika). Kwa kawaida, wana-sheria huwa makini sana katika matumizi na maana
ya maneno! Bwana Chenge hakuiita hizo pesa zilizotajwa, “vi-senti”; aliziita, “vi-ji-senti”!

Na katufundisha kuwa kama hizo pesa ni “vi-ji-senti”, basi Bwana Chenge anazo nyingi zaidi alizoficha kushinda hizo! Kuna uwezekano Bwana Chenge anawajua “wenzake” walio na
nyingi kuliko hizo alizo nazo katika benki ya nchi za nje!
Bwana Chenge ni m-Bunge wa Bariadi Masharik; ni m-Sukuma aliyejitetea, hapo baadaye, kwamba Kiswahili kinampiga chenga. Wengi hatukukubali kuwa Kiswahili kinampiga chenga,
Chenge! Kuzunguka pote Tanzania kando ya Ziwa Victoria wazawa wanaelewa sana maana ya “vi-ji-senti”! Na wa-Tanzania wanajua matumizi ya Kiswahili ya vianzo vya “ki/vi”! Na
wanaelewa sana wakati ambapo “ki” inapofuatiwa na “ji” kuwa “kiji…” au “viji…” katika muktadha wa kupunguza hadhi na thamani ya kizungumzwacho!

“Simply put”, uchu wa u-nyang’au wa baadhi ya walalaheri wa kufuatilia na kuchuma “vi-ji-senti” unaangamiza taifa letu, kama Johnson Mbwambo anavyowahi kuandika katika toleo la
Raiamwema kuhusu “Ya Don Corleone, Yakuza na Mafisadi Wetu!”
Je, TAKUKURU ilifanya kazi yake, kitaalamu? Haikufanikisha ushirikiano na Kamati Teule ya Bunge.

Je, yote yale Kamati Teule ya Bunge iliyoyagundua yalianikwa nje? Hapana!

Kwa nini Tanesco imegeuka kinyonga? Tanesco ilikataa kununua mitumba ya Dowans;

Tanesco ikakubali na kukiuka msimamo wa Bodi yake; na sasa Tanesco imekataa tena!

Je, Tanesco sasa inasema, “Potelea mbali hata kama nchi inazama gizani?” Je, Bodi ya Tanesco nayo ilifanya uamuzi mzuri wa kutaka kutuma tena wataalamu wa Tanesco waende huko Houston, Texas, kuzatiti bei hasa ya mitambo (turbines) hiyo ya kufua umeme? Ni kupoteza mapesa ya umma; Ofisi yetu ya u-Balozi, Washington, DC, inaweza kufanyakazi hiyo (kulingana na sera ya diplomasia ya uchumi).

Brela iliamua kuifuta “Richmond” ifikapo Septemba 15, 2008 kutokana na ufisadi na utata uliozalisha sakata la “Richmond”! Lakini kufuatia kushindwa kufua umeme wa dharura, leo hii bado tunaikumbatia “Richmond” kwa jina la “Dowans”! Malumbano yamejitokeza ya kukidhi mahitaji ya umeme kwa kununua mitumba ya mashini za “Richmond/Dowans”!
Wenye kutaka mitumba hiyo inunuliwe, wamezua mantiki ya kuunda na kutekeleza sera za umeme na nishati hadi 2014! Tunaihurumia “Dowans” na huruma hizo zimevalishwa
nondo ya uzalendo, kwa upande wa Tanesco, Kamati ya Bunge uya Ununuzi – Mashirika ya Umma).

Waziri wa Madini na Nishati, na akili zake, kaamuru hiyo mitumba inunuliwe! Hata kwa Ikulu kidiriki kutamka eti Tanesco ni kampuni kamili yenye kufanya itakalo ni kukiuka uwajibikaji – uongozi unaokwenda kombo!

Kwa nini tusifikirie mbinu nyinginezo: nuklia (uranium tunayo kwa wingi..kwa nini wawekezaji wachimbe na kuuza nje kwa manufaa yao)! Jua tunalo, tena la masaa 12!

Upepo tunao tena wa nguvu milimani, mabondeni na tambarare! Gesi tunayo tena inachotwa pengine kuuzwa nchi za nje! Maji-mvuke moto moto tunayo! Na vyanzo vinginevyo vya umeme na nishati tunavyo.

Kwa nini tunang’ang’ania mitambo mitumba, tena ya ghali, ya “Dowans” – kampuni ambayo haistahili kuwepo na Ambato imetushitaki huko Paris? Hivi tuliambiwa na Muumba kuwa
chanzo cha umeme na nishati ni mabwawa yetu tu? Mbona hatujajifunza lolote (kama tunafundishika?) kuwa tunaathiriwa na ukame kila mwaka?

Lini tutaamka! Ama tuliishaga-kula “vi-ji-senti” vingi vya wawekezaji ambavyo vinatufunga nongwa na mitambo ya kufua umeme kwa mabawa ya maji? Si ni afadhali tufuge samaki
kwa wingi katika mabwa hayo au tuyatumie katika umwagiliaji mashamba?

Nihitimishe na BAPism:

Uchu wa u-nyang’au unaangamiza mataifa!
Uchu wa u-nyang’au unaangamiza mfumo wa uchumi wa u-bepari wa Nchi za Magharibi!
Uchu wa u-nyang’au unaangamiza nchi ya Tanzania kwa kutaka kuchuma ‘vi-ji-senti’!
Uchu wa u-nyang’au hujikinga ki-sheria kwa kuvaa nondo ya “limited liability Company” (LLC) au, kama tulivyozoea kuita, “limited” (Ltd), endapo kampuni itafikishwa mahakamani kwa ufisadi.

Uchu wa u-nyang’au (kupitia baadhi ya “vigogo” na “wakubwa” na ma-wakala uchwara) hunyonya jasho la wananchi masikini wanaosamehewa madeni na nchi tajiri!
 
Mwulize EL,Jk,kwani wanajua kilo yamtu iko fasi anaikalaga jovile mtu ya ngufu inakalaga kwa bunge.
 
Back
Top Bottom