Angeiua NCHI usingeikuta wala usingekuwepo. Nchi inauwawa sasa. Aliacha mashirika ya UMMA zaidi ya 400 mikononi mwa wazawa. Karibu yote hayapo. AJIRA ni tatizo sasa. Aliacha migodi yote ikiwa bikira kabisa. Sasa tunaachiwa mashimo. Hakuna tunachoambulia. Aliacha TANZANIA ni moja. Sasa ZAnzibar ni NCHI na mipaka yake. Hakuacha tajiri mzawa. SAsa wapo. Bila kujali utajiri wanaupataje. Aliacha watu wanasoma bila mikopo na shule za umma zikiwa na hadhi ya aina yake. Sasa watoto wetu wakifaulu kwenda shule za UMMA wanalia.Na kuna wanaomchukia kwa kuiua nchi, kutesa watu na kushindwa kabisa kuongoza, duhh, tazama wakati wake, sisi tulikuwa wapi na wenzetu wa Kenya walikuwa wapi?
NYERERE 1985......VYAMA VINGI 1992....!Kwangu mimi kosa moja kubwa la Nyerere ni katika transition ya kutoka chama kimoja hadi vingi. There and only then, a level bar would have been set. i.e. CCM should have been dissolved. Kila chama kingeanza na moja, kuanzia wanachama hadi vitega uchumi vya chama. Aliruhusu au kukubali la vyama vingi na papo hapo akajing'atua!
Nyambala,
You want me to answer your question? Nipe muda. Unamkumbuka Yesu? Hata wale mitume wake waliokuwa naye muda wote hawakumwelewa wakati wote.
Faizafoxy kwa kifupi kama utakuwa unaandika pepa yoyote halafu inahitaji citation na wewe ukaweka wikipedia kama reference yako, trust me hiyo pepa haitapita iwe ni kwa ajili ya kuhitimu mafunzo ya certificate, Stashahada au Shahada, na kama itapita basi ujue huyo Mwalimu wako atakuwa mvivu wa kusoma.
Faiza,Kwani ilukuwepo? labda wewe ndio ulikuwa hupo. Kulikuwa kuna nchi hapa au uozo tu. Unanchekesha.
Hayo mashirika ya umma yalikuwa yanasaidia nini? aliacha majina ya mashirika, yote yalikuwa hohehahe.
Wewe ndio mwenye utando, unaambiwa wakati wa nyerere watu tulikuwa hohehahe, wewe haikuingii akilini, labda tu ulikuwa hauko kama hayo huyajuwi.
"...Rashid! You are responsible to see that they go home..."
***
Na ndio maana alifanya kazi na Mwalimu hadi mwisho. Mtu pekee kuwa hivo kwa miaka yote ya utawala wa Mwalimu tangu uhuru. Aliachiwa Nchi na Mwalimu na baadaye akamrudishia. Jaribuni sasa muone.As usual, Rashid the henchman was the one to do the dirty work.....!!!
Sawa, hivyo unakubali kwamba Nyerere alikandamiza uwingi wa kisiasa lakini hoja yako ni kwamba hakuwa peke yake. Sitakai.kwa kutumia mkono wako wa kulia, hesabu ni nchi ngapi Africa zilikua na vyama vingi, kabla ya 1990.
Mobutu hadi anaondolewa madarakani kulikuwa vyama vya siasa zaidi ya 100 pale Zaire. Wengine wote uloowataja isipokuwa Banda (Rais wa Maisha) na Obote ( Uganda ilikuwa na vyama vingi) walikuwa wanajeshi. Unathubutu kumweka Mwalimu kundi hilo kweli? Uko mbali mno na ukweli na uhalisia wa mambo ya nchi hii. Uko huru sana kwa maoni yako haya.Sawa, hivyo unakubali kwamba Nyerere alikandamiza uwingi wa kisiasa lakini hoja yako ni kwamba hakuwa peke yake. Sitakai.
Kwa hiyo alikuwa na kina Bokassa, Banda, Obote, Babangida, Compaore, Samuel Doe, Mobute, n.k, n.k
Nakubali.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ailure-some-say-yes-he-did-4.html#post2113282...
...Angewezaje wakati yeye alipokuw madarakani miaka 27 alishindwa? Alivifuta vyama vingi!
...
...
...Julius Kambarage Nyerere was the president of theUnited Republic of Tanzania between April 1964 andOctober 1985, when he retired out of his own free will butcontinued to influence the Tanzania political scene untilhis death on October 14th 1999 in a London hospital ofleukaemia. He was the architect of an exemplary mode ofuniting two sovereign states in Africa (Kesller, 2006) inwhich, despite the existence of all the ingredients...
Faiza,
Nilimaliza kidato cha sita enzi hizo za Mwalimu, ajira ilikuwa inanisubiri. Haikuwa ya kutafuta. Watanzania sote kwa ujumla wetu tulikuwa hohehahe. Sasa hivi wapo wanaokula na kusaza na wengine wanatutapikia miguuni kabisa. Kuna WATANZANIA sasa hata mlo mmoja kwa siku ni shughuli pevu. Haujui hata mashirika ya UMMA yalisaidia nini? Unakifahamu kitega uchumi chochote cha Mwalimu au mwanaye hapa nchini?
Akitowe wapi and he failed economically? unauliza jibu?
Sasa hebu isomeni hiyo sppech aliobandika mkjj halafu m-judge wenyewe, alikuwa anamawazo finyu kweli kweli, wakati watu wanapigania kipato kikubwa yeye anapigania kipato kidogo. So pessimist.
Wapo wengine wanadiriki kusema kuwa Mwalim Nyerere ndie aliye ruhusu vyama vingi, wakati yeye na serikali yake ya TANU wakishirikiana na Afro Shirazi Party ndio walivipiga marufuku vyama vingi. Kupenda kweli maradhi.
Mwenye majibu mazuri kwa swali lako ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Tume iliyokuwa chini ya Jaji Francis Nyalali.Nani aliruhusu vyama vingi wakati 80 percent ya Watanzania walivikataa walitaka kuendelea na chama kimoja? Kama demokrasia ni mawazo ya watu wengi kukubaliwa kwanini mawazo ya wengi hayakukubaliwa huoni kuwa kwa kukubali vyama vingi tumejikuta kwenye matatizo la heri tungebakia kwenye chama kimoja kama majority ya wananchi walivyotaka? Kwanini tuliingia kwenye vyama vingi wakati sauti ya wengi ilikuwa ni chama kimoja?
Mwenye majibu mazuri kwa swali lako ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Tume iliyokuwa chini ya Jaji Francis Nyalali.
__________
Nakumbuka uchaguzi wa kwanza baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi wa mwaka 1995. Mkapa alishinda kwa kupata asilimia 61.82