Mkuu
FJM,
Tumekuwa tukiamini kwamba mawaziri wengi wamekuwa wakiwekwa kwenye wizara ambazo hawana utaalam nazo na ndio maana kumekuwa na madudu mengi. Case ya Mh. Nundu, inaweza kutumika kama proof ya kwamba tatizo sio utaalaam wa mawaziri, bali ni mfumo mzima.
Nikisema mfumo, ninaongelea Kanuni za Utumishi; Taratibu za Mawasiliano na Uwajibikaji, nani anawajibika kwa nani, na ana report kwa nani? Je, kuna mianya ya kum-by pass Waziri na hivyo Katibu Mkuu au Naibu Waziri kuwa na direct access na Ikulu au PMO? Then, kuna namna ambavyo hawa watendaji wanapoteuliwa, je, wanapatikana kwa kutumia vigezo gani? Kuna mahusiano gani yaliyopo kati ya mteuaji na mteuliwa?
Juzi kwenye case ya Prof. Mahalu, Mkapa ametamka kwamba kuna maagizo alimpa Prof. Mahalu kwa mdomo [Mahalu alikuwa Balozi, kiutaratibu anatakiwa ku-report kwa Katibu Mkuu au Waziri wa Foreign Affairs, and in special circumstances, anaweza ku-report moja kwa moja Ikulu, lakini info hiyo inatakiwa pia iende kwa Katibu Mkuu/Waziri wa Foreign Affairs].
Tumefika mahali marafiki wanapeana teuzi na kutokana na misingi hiyo hata utendaji kazi unakuwa ni wa kienyeji enyeji na ndio maana Mkapa anasema alitoa maelekezo kwa mdomo wakiwa wawili tu, Mkapa na Mahalu! Waziri husika akisikia huo upuuzi unategemea atakuwa na imani na huyo balozi? Kuna mangapi ambayo yanaenda behind his/her back? Je, hao watu watashirikiana ipasavyo kufanya kazi? Chochote kile atakacholetewa Waziri atakiangalia kwa angles zote kwamba usije ukawa ni mtego, kama amezowea kwenda Ikulu direct, kwanini leo anapitishia hapa? The whole system is broken kwa sababu ya uswahiba na "u-mwenzetu". So, some of wateuliwa are considered as insiders while others are outsiders!
Kuna haja ya kurekebisha mfumo wa uteuzi, Kanuni za Utumishi kwa Wateule, Reporting System na madudu yote, baada ya hapo tutaweza kumlaumu mhusika moja kwa moja.