Mh OR Nundu, pole saaana kwa yaliyokusibu. Kwa mtizamo wangu ni kuwa, kwa serikali iliyopo sasa hivi, ni afadhali ukakataa uteuzi wowote ili kuepuka matokeo kama haya. Kikwete anataka watu ambao ni maswahiba wake au maswahiba wa mwanaye wenye uwezo wa kufanya ufisadi na kuficha vizuri ufisadi wao. Kama ikitokea ukafanya ufisadi na ukajulikana kupitia Kamati ya Bunge, au kupitia Mkaguzi wa Mahesabu ya Fedha, Kikwete atakugeuka na kukubebesha lawama zote.
Kikwete ukifanya naye kazi utachafuka na kuharibu jina lako. Ni raisi wa ajabu sana dunia haijapata kuona. Kama wa-Tz wangekuwa na nusu ya roho ya ki-Arab Kikwete asingeweza hata kumaliza mwaa mmoja pale Ikulu yetu. Lakini bado yupo pale kwa sababu sisi wananchi tupo kama tulivyo, wapole kama kondoo.
Tatizo jingine ni aina ya wasaidizi unaojikuta kufanya nao kazi. Wizara yako ina watu ambao ni hatari sana kwa taifa hili. Mfano Omary Chambo - huyu mtu hana hata 0.0% ya uzalendo moyoni mwake, na mtu anayemhifadhi pale ni huyo Kikwete kwasababu zilizopo na zinahifadhiwa. Mtu mwingine aliyekuzunguka ndiyo huyo jamaa mwenye maneno meeengi, fisadi asiye na haya Mh Mfutakamba. Jamani hata anayewateua sijuwi huwa anawatowa wapi na anatumia vigezo gani kuwapata watu wa jinsi hii!!! Mtu mwingine ni huyo mutu yenye maneno miingi Saad Fungafunga... orodha ni ndefu ya viongozi wabaya wakiongoza Wizara nyeti na mhimili wa uchumi wa taifa.
Pole sana, mimi nakuomba utumikie taifa lako kupitia Bunge la JMT. Kule serikalini hakuna kitu huko ni wizi tu..