Watu Kazini...
Katika huu uzi, kuna matundiko mawili yanayoandaa usuli kwa tundiko hili.
Tundiko la kwanza - Hili lina mawaidha ya kutosha juu ya jinsi gani 'Kusafiri Kiwakati' si kama watu wanavyoona katika filamu...
Kwamba, tayari watu tunaishi katika ulimwengu ulio ni namna 'alimwengu sambamba' nyingi isivyo idadi. Hili linadadavuliwa na Bashar katika video ya kwanza.
Video ya pili inataja kilicho ni wazi, sisi wote ni 'Wasafiri Kiwakati'... Labda watu wanakwenda mbali isivyolazima wanapokuwa wakidadisi ukweli wa jambo hili... Nimepata kudokeza hili katika
tundiko hili.
Video ya tatu ina nasibu kuelewa 'vizio vya habari'; namna gani 'milele' inakutana na 'sasa'... Japo haya yanawasilishwa kwa mujibu wa mapelekeo ya fikizia ya leo na tafiti, mule katika video kuna 'madini' kuhusiana na 'umodelishi wa Kihisabati' na 'Tafsiri' vinavyoonekana kana hivi ama vile katika ulimwengu wa sayansi yenye kufungama na maumbo.
Video ya nne, ni ya
muhimu sana.... Hii inawaanda watu wote wanaotaka kuelewa kusafiri kiwakati kunaweza 'kuendeshwa vipi' -- inapokuja kwa nasibu za akili ama hata mitambo. Cha muhimu kuchukua katika video ile ni kuwa dhana ya '
ulimwengu unaomwekua' ni halisi... Nimezungumza hili katika
tundiko hili. Kumwekua huku ndiko kunakowezesha maingilliano na 'kinishati-habari' kuwa ni jambo linalowezekana...
Tundiko la Pili - Hili lina mawaidha juu ya 'Ngamuzi ya Kikwantumu' na namna gani hii pekee ndicho kitu kinachoweza kutumika 'kimtambo' kuratibu uwezo wa kuhama kutoka nukta moja hadi ingine, wakati mmoja hata mwingine -- kusafiri katika 'unafasishi' ni 'kusafiri kiwakati'... Ulimwengu wote ni namna ya 'Kinishati-habari'... Kila nukta ya 'umahala' ama 'tukio' lina 'saini' yake ya kipekee; ukiweza kubaini saini ya mahala ama tukio kwa 'mkaribiano' wa 'uhalisia' ama simetria, unaweza 'kurukia' pahala bila 'kusogea' -- kwa kutumia mtambo, ngamuzi ya kikwantumu na alogarithimu sahihi... Lakini 'akili' zetu tayari ni 'namna ya ngamuzi za kikwantumu'... Na basi, msije kushangaa, ngamuzi za kikwantumu ni nusu-mtambo, nusu-akili... Ni 'kinu' cha kuweza hata kuendesha mfumo wa maisha wa watu kwa kutumia Akili Bandia; Ni chombo hatari kwa mtu/watu wasiojua kikitumia kwa busara, hatari hata mara nyingi kuliko 'bomu la nyuklia' kwa mtu ama jamii ya 'washamba'...
Pia katika tundiko hili, kwa mara ya kwanza uliletwa ushahidi wa mtu na taasisi ya kushughulika na utafiti, kuvinjari katika hali ya hisia zisizo na mahala pamoja na kupata habari kwa fahamu zote tano na zaidi -- kokote mbali, nje ya wakati, kwenda nyuma, kwenda mbele ya wakati na zaidi. Yaani, unaweza kutazama mtu aliyeishi nyuma ya wakati na 'kusoma mazingira yake', 'hisia zake na hata mawazo yake'... Vivyo hivyo unaweza kufanya kwa mtu aliyepo sasa na hata mbele ya wakati... Mzee
Courtney Brown, Ph.D., Mswahili mwenzetu, anatumia mbinu na itifaki za kisayansi katika jambo tunaloweza kuliita 'Ukiona Mbali wa Kisayansi'; yeye analiita hili 'Scientific Remote Viewing' katika lugha ya Kiingereza. Huku ni namna ya kukusanya 'data' na 'kuchanganua' hizo ili kuunda 'habari' na mielekeo ya tafsiri kwa kilichoshuhudiwa na 'Kiona/Viona Mbali' wanaofuatisha itifaki rasmi na zenye kukubalika katika ujuzi na ufundi wa namna hii--wakifanya kazi katika hali ya upofu wa somo.
Katika tundiko hilo la pili, kuna video ya Mzee Courtney Brown akielezea ufundi wa SRV / OMkiS katika kubaini Habari za Kina za Jambo lililotia shauku kujua kuhusu Sayari ya Miiri; na yeye kama taasisi ya
Farsight Institute na washirika waliendesha zoezi la 'Kubaini Ukweli' kuhusiana na kitu kilichoonekana kama mlima wenye bomba lenye kupuliza maji nje... Na ilikuja kubainika eneo hilo kuna 'Kambi' na ina wanadamu wakishughulika... Ndiyo, tena binadamu kutoka duniani hapa... Picha hii ilidakwa na satilaiti, na ilipata kuwa katika
tovuti hii.
Sasa, kwa kuwa watu wengi wamevutiwa na mambo ya "kusafiri Kiwakati' kupitia filamu na Tamthilia; wengi labda wanakosa kudadisi--hao wanazitengeneza hizo filamu wanatoa wapi mawazo na ubunifu wao?
Farsight Insitute, katika mradi wao mpya wanafunua asili hasa ya kazi za Mtayarishaji George Lucas --- Mbunifu wa Visa na Simulizi za 'Vita vya Kimanyota'... Nilipata kuzungumza kuhusu hii filamu humu JF katika
tundiko hili...
George Lucas, Maisha haya na mengine... Chimbuko la Visa na alikopata kuishi nje ya sayari yetu...
Tazama treila...