The World is a flat plane and not a globe

Sasa wakuu nyie mmesoma hizo nadharia, full of conspirancy bila kufanya uchunguzi wenu binafsi😃😃.Kina Armstrong wameenda nje ya dunia wameipiga picha, sattelite zinaenda juu zinapiga picha kitu kinatoka cha duara, nyie mnataka kutufundisha nini sasa?😃😃😃.

Watu wa meditation wamegonga meditation zao wanaona ni ya mfano wa mviringo pia, kina Gallilei Gallileo mpaka wakahukumiwa kifo kwa sababu ya kusema ukweli ngoma ni ya mfano wa duara! Sasa wafiche tukijua kuwa iko kama meza watapoteza nini?
 
Siyo inaonekana? Wote wanaona tufe. Wote wanazunguka tufe, sivyo?
Kama Dunia ni bapa, unaizunguka namna gani?
Vipi unaona umbo lake jinsi unavyopita juu yake, kuona mapya kila ukiendelea pale yaliyoonekana kama chini ya upeo (horizon)?
Hasa vipi unasurvive ukirushwa juu vile kama hakuna tufe ambalo mashine yako inapaswa kuzunguka, kwa kuzingatia nguvu ya graviti kulingana na kiasi cha mafuta unachobeba??
Samahani, sijakuelewa vizuri ukimaanishacho. Nitapenda unieleweshe maana ya maswali yako kutoka katika comment yangu.
 
Nikisikia wanachosema wale waliozunguka Dunia angani au pia kwa ndege: Ndio!
Nikisikia wanachosema hao waliopo juu pale sasa hivi: Ndio!
Nikiangalia picha za kamera za ISS (na satelaiti nyingine): zinalingana!
Nikichungulia habari zote ninazujua kuhusu jambo hili na kutumia akili ya wastani: Ndio.
Tuanzie mwisho huku pale unapotumia akili yako ya wastani... maana kusikia na kuangalia sio jambo gumu sana na bado mengi tutasikia na kuyaona.

Mkuu kwa akili hizo za wastani, unaliona jua linatembea au limesimama?
Kwa akili hizo hizo za wastani, unayaona mazingira katika utambarare au uduara?
Kwa akili hizo za wastani unazani palikua na ulazima gani kufundishwa umbo la dunia na hasa katika dhana moja ya uviringo peke yake?
Kwa akili hizo za wastani dunia ikiwa tambarare unadhani kipi kinachowezekana sasa kisingewezekana kutokana na shape hiyo?
Kwa akili hizo za wastani juu ya dunia ni wapi?
 
Asante mkuu ,watu wamekuwa watumwa,mimi nilisoma science mpaka chuo ila namshukuru Mungu ufahamu wangu ulipenda sana kuhoji because am SKEPTICAL ikanifungua mengi sana sasa hivi sina hata wasiwasi kama nilivyokuwa kwenye ulimwengu wa dunia inayozunguka jua zaidi ya speed ya mwanga.kumbe ni michezo ya nasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu na mimi naomba kitabu
 
Asante mkuu ,watu wamekuwa watumwa,mimi nilisoma science mpaka chuo ila namshukuru Mungu ufahamu wangu ulipenda sana kuhoji because am SKEPTICAL ikanifungua mengi sana sasa hivi sina hata wasiwasi kama nilivyokuwa kwenye ulimwengu wa dunia inayozunguka jua zaidi ya speed ya mwanga.kumbe ni michezo ya nasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ulisoma political science


Ulisoma wapi dunia inazunguka jua zaidi ya speed ya mwanga kama sio uonho huo.

Unaijua speed ya mwanga wewe ?
 
Mkuu neil armstrong moja hajawahai kwenda mwezini,pili sattelite ni uzushi wanatumia underground communication cables na long tower cameras pamoja na drones,mkuu dunia sio mpira nasiokuwa ni mzaha am serious jiulize why wanasayansi wanatumia straightgeometry na sio sphericalgeometry jiulize kwanini ukitumia p9 camera unaona meli iliyo umbali mrefu sana hata zaidi ya mile 70 kukiwa na low humidity hakuna curve mkuu sema nikupe lengo lao kwanini wamedanganya mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga wewe spherical geometry inatumika kwenye geodetic studies. Plane table assumption inafanya kazi over short distances.
 
Satellite ni uongo nikuulize nasa imeanza 1958 satellite je?ukijibu ntakuambia kitu kuwa zipo ila una ushahidi wowote?zaidi sarakasi za NASA za kupotosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
We mshamba NASA imeanzishwa kipindi ambapo warusi washaenda kwenye space zaidi ya mada tatu, washarusha sputnik
We unadhani satellite zinarushwa Na NASA tu?

Currently Kuna satellite za China, India, wafaransa, ESA ( ZA ULAYA ) ,RUSSIA hadi za waarabu

Wote hawa wamekaa wakakubaliana wakudanganye wewe mjinga mmoja uliye Tanzania?
 
Jamani masomo ya urubani ni free kabisa online ingia kasome ila ujue siri moja sio kuwa na malengo ya kua kuwa rubani

Hivi unajua ndege inaruka umbali mrefu sana pasipo kupaa kwa kujikunja kufuata the way dunia ilivyo but huwa inaenda straight tu?

Kama kuna satellite kwanini kuna mkonge duniani kote?
kwanini mmarekani mwenye teknolojia kubwa aliweza kupigwa na kushindw akujiokoa huko mapangoni kwa watu wa iran kisa tu hawawezi wasiliana na ndugu zao? na kumbuka wanasatellite yao binafsi?

Kwanini uwekewe mnara kwa babu yako kule upate shida ya network wakati ingeachiwa moja kwa moja kutoka juu ingefika kwa urahisi?

kwanini ndege zinawekewa rada chini duniani na hazitumii sattelite?

Siwaaaminishi muamini dunia flat ila nataka tujiulize na kujifunza kwanini baba anasema anahela laki mbili ndani lakini amekopa buku ya nauli

Hujui satellite signals zinazingua kwenye maeneo yenye obstacles kama ukiwa pangoni, kwenye forests pia geometry ya satellite mahala ulipo Na wakati husika inachangia sana kupata signal nzuri mbaya.
 
Mnaouliza Sunrise na Sunset ni kuwa Sun linatembea from East to West (Points hizi mlizokaa na kuamua ziwe hivyo).

Hivyo Jua Uanza safari kutoka Mashariki na Kufika Magharibi, Kisha jua la Magharibi huanza safari na Kufika Mashariki.

Mwezi ni mfano wa Rubber Bracelet (Culture/Bangili za Mpira) ambazo wakati wakiza utoa uan'gavu na wakati wa mwanga hufifia.

Upepo ni hutokea from Outer Space (Ulimwengu) na sisi hupata hisia.

Mvua hutokana na evaporation inayoathiliwa na maji na joto. Mfano; Uwapo jikoni umefunika Pressure Cooker, Rice Cooker au Sufuria pressure ya chini usugua juu na kuleta mvuke ambao urudi chini.

Je Iweje nchi za kaskazini na kusini (Hio Uliyopangwa) hupata Snow, Winter, Fog etc?. Ni Uwepo wa nchi hizo katika kingo za dunia ambayo ni made of Ice.

Uwepo wa vumbi ni kutokana na ardhi ya juu ya dunia kutifuliwa au kusongwa na upepo.

Round/Spherical Earthers mbona mnashindwa kutoa ithibati ya ramani zenu?! Ramani ya Spherical na Round Earthers inaonyesha Middle East ni Northern Central ya Dunia na uwepo wa Strait of Hormuz, Persian Gulf na Gulf of Oman, huku mkiskia United States Navy Ships zinaenda katika location hiyo kwa 7 Days from Florida Keys (Tampa au Miami Base).

Ukaribu wa SA (Afrika Kusini) na UK (Uingereza) ni prove dunia siyo Kiazi, Kichwa, Mviringo, Tufe, Chungwa wala Yai!

Ukaribu wa Oceania na Chile, Peru na Argentina huku ukubwa wa so called Pacific Ocean unazidi kujipinga.

Oke! Nile inatwa maji kutoka Lake Victoria (South) na Kupeleka Mediterranean Sea (North)

The World is Flat pure Flat Bense!
Mkuu unaonekana hauna uelewa Na somo LA map projections.

Ramani zote ( plane) unazoziona ni projected maps from spherical/ellipsoidal earth call it what what you like

Na projections zipo za aina nyingi.

Moja ya sifa ya projections ni kuleta distortions so kuna baadhi ya projections zina leta false representation ya uhalisia ( ground truth).

Mfano kuna nchi utaziona kubwa kwenye ramani lakini ni ndogo in reality.

Ndiomana different projections zinatumika kutengeneza ramani for different purposes.
 
Dunia ni duara na hilo halina ubishi, anayepinga ni mjinga tu. Toka na meli pale Cape Town uelekee mashariki mwisho wa safari yako utajikuta umerudi pale pale.

Huu ubishi wa kijinga wenzenu waliufanya millennium kadhaa nyuma. Sayansi inathibitishwa kwa sayansi.

Mnakuwa kama mtu moja anaye idanganya dunia kwamba nchi yake haina Corona huku hadi wateule wake wanakufa kwa huo ugonjwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom