Mkuu kumbuka hata hawa Jamaa wa flat Earth hawataki kutoa ushirikiano wa kutosha ktk maswali wanayo ulizwa! Mfano Swali limeulizwa kuhusu picha ya hizo dome3 za vioo zinazo ifunika Dunia.Aliye piga picha ya hizo Dome zote 3 aliwezaje,iwapo roket inashindwa kupenya na kutoka nje ya dome ya kwanza tu?! Hata katika vitabu vya Dini hiyo habari ya Dome ya kioo kuifunika Dunia haija andikwa! Tungesema wanao pinga flat Earth iliyo funikwa na dome za kioo wanapingana na Mungu! Sasa Jamaa huyo mwingine utetezi wake ni kutuwekea Vijumba na Majengo yenye Dome kwa juu!
Mkuu nimekusoma, nadhani hizo domes ni imaginary kutokana na ancient beloefs kwa sababu elimu ya globe earth imekuja hivi majuzi tu. Kwa sasa nafuatilia expeditions mbalimbali huko Antarctica, inaonyesha kuna jambo limefichwa kabisa.
Mpaka sasa nimeweza kuzikubali facts kadhaa mfano:
1. Hakuna carveture ya dunia kwa kutumia vitu hakisia zaidi ya kwamba ipo kimahesabu (theory) tu
2. Hoja ya meli kutokeza ni perception tu
3. Hakuna mwanadamu ama chombo kilichovuka parking orbit mpaka sasa (maneno ya mwanasayansi wa NASA akiwa ISS)
4. Kwa kuzingatia hilo ina maana safari ya mwezini ni hoax
5. Dunia ina centre ambayo ndio NORTH POLE ndio maana sumaku zote zinaelekea huko.
6. Kila nikitazama mwenendo wa jua nashawishika kuwa haliwezi kuwa na ukubwa unaosemwa wala huo umbali wa km milioni 150
7. Mwezi unaweza usiwe mchanga kwa sababu kuna kioindi unafifia na tunaweza kuona upande wa pili kupitia huo huo mwezi
8. Kwa nini ndege hazirekebishi uelekeo kufuata umbo la dunia?
9. Nakubaliana na hoja kuwa picha zote za dunia ni CGI
10. Kama umbali uliochimbwa kwenda chini ni 12.3 km pekee, tunajuaje yaliyopo huko?
11. Kwamba dunia inazunguka haiingii akilini hata kidogo, yako mengi yanayokataa logic hii.
12. Kwa nini land navigation (Topographical maps) haizingatii umbo la dunia?
13. Kwa nini meli zinatumia flat earth model?
14. Gravitatinal force ni halisi?
Etc, etc. Nahitaji mwanasayansi wa globe earth anisaidie kwenye hayo ili nisipotee.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk