Ulaya na China hawataweza kuwa super power kwasababu moja tu hawapendi na hawajui kupigana. Nchi za ulaya zimepiga kampeni ya kumpindua Ghadafi na wenyewe walikuwa mstari wa mbele lakini sasa umekuja wakati wa kupigana na mabomu wanataka kumwachia Mmarekani mwenyewe!. Obama hakutaka hata kuingia kwenye vita lakini alikuwa ana unga mkono Ghadafi kuondoka. China wenyewe hawapendi fujo wanataka vitu viende kama vilivyo hata kama ni Kiongozi anaua watu wake China haiwezi kupinga. Hawa wote China na nchi za ulaya wana vifaa vya kijeshi lakini tatizo sio vifaa kama hutaweza kupigana hasa pale unapofikiri ni lazima!. Marekani wasemeni tu lakini kama wanaamini kitu wanaweka maisha yao na si kuongea siasa nenda rudi. Ulaya iko dhaifu sana na miaka ijayo hata Africa inaweza kuichukua Ulaya ukizingatia idadi kubwa ya watu wanaoishi huko ni wazee. Marekani inatawala kijeshi Japan, Korea ya Kusini, Iraq, Israel, Saudi Arabia, Afighan, Pakistan, Bahrain, Egypt na German.Mimi navyoona Marekani nguvu zinaongezeka na hazipungui kama watu wanavyofikiria. Obama anasikilizwa Japan sasa wakati wa tetemeko kuliko waziri mkuu wa Japan na anaaminika south Korea kuliko kiongozi wao.