- Mkuu ukisoma tena post yangu, utaona haina uhusiano wowote na ya kwako, hebu soma vizuri post yangu hapo juu.
William.
Naomba kuuliza BAK, Je, hivyo vitisho ilivyotolewa na hao wastaafu wa CCM ni vya kuganga njaa au? Spati picha katika ulimwengu wa kidemokrasia watu kusimama na kutoa hoja zisizo na makanyagio.
Hata mimi sielewi ndugu yangu, inasikitisha kwa kweli halafu Kikwete mwenyewe pamoja na vitisho hivi yeye kakaa kimya kabisa kama kawaida yake!!!!
Bubu Ataka Kusema;
Huyu ni mmoja wa kambi ya "Ni Mwenzetu huyu" hivyo kazi yake hapa ni kutaka kuonyesha kinachoandikwa na yeyote yule ambacho yeye hakiafiki kina kasoro.
Tunajua fika kutokana na dalili za wazi kabisa kwamba upinzani hauna dalili ya kuchukua Urais 2010, lakini pamoja na hayo haina haja ya kumpa tena Kikwete. Katiba ya CCM inaruhusu wagombea wengine wanaotaka kufanya hivyo kuchukua form, sasa hivi vitisho dhidi yao vya nini tena? Na lini katiba ya CCM ilibadilishswa na kuruhusu vitisho kwa wale ambao wanataka kumpinga Rais!? Haya mambo ya unafiki ndiyo yanaifikisha nchi yetu pabaya. Rais kama kuna mazuri aliyoyafanya yawekwe hadharani, lakini hakuna hivyo Watanzania tunastahili kabisa kupata Rais mpya ambaye ataweka maslahi ya nchi mbele kwa manufaa ya Watanzania.
Nami sikusema kwamba ina uhusiano hebu isome tena, bali nimeongezea sababu za wao kutoa vitisho badala ya kuishia pale ambapo wewe ulitaka waishie.
Ndugu WJM, nini msimamo wako katika hili suala la hao wastaafu wa CCM kumpigia debe JMK? May be itatusaidia na kumsaidia BAK pia katika kufanya tafakuri?
- Wastaafu wanne wa CCM, wanawezaje kuwaamulia wananchi Millioni 40, nani awe rais wao? I mean kama kweli wanaweza basi hili taifa tuna tatizo kubwa sana, otherwise ninaamini kwamba kila mwamnanchi wa Tanzania ana haki ya kusema maoni yake kuhusu nani awe next rais,
- Na ni haki ya kila mwananchi kupingana na mwingine kwa hoja, lakini tunahitaji kuepuka kejeli na matusi kwa sababu zinaishia kuigawa jamii na kuharibu mshikamano wetu wa taifa, binafsi sijaamua nani anafaa kuwa next rais, au kutoka chama gani.
William.
1.
- Usiogope kivuli chako mkuu, maana hizi name calling ni dalili za uoga na kukosa hoja, mimi ni mwananchi wa Tanzania kama wewe na mwenye haki kama zako za kuwa na mawazo huru na kuyasema bila kuogopa, hayo ya mwenzetu ni yako, naomba usinitishe au kuniogopesha kutoa maoni yangu mkuu, wewe toa yako na mimi niweke yangu, tulisaidie taifa tusibaguane kwa sababu tu ya nyimbo tofauti.
2.
- Haya ni mawazo yako, na pia wananchi wengine wanatakiwa kuwa na mawazo tofauti au sawa na yako, ndio demokrasia at work.
William.
Hakuna tusi wala kejeli hilo la huyu ni Mwenzetu ni neno lenye umaarufu mkubwa ndani ya CCM na si kejeli wala tusi.
Njaa zao zitawaua, yani wako radhi kuuza hutu na haki zao kisa kuseek audience na favors kutoka kwa JMK.
Kazi kweli kweli!
- Ahsante mkuu, lakini sijawahi kusema mimi ni mwachama wa chama gani, na sijui wewe ni mwanachama wa chama gani, na sidhani kama ni muhimu sana, au? Lakini nimekuelewa.
William.
Wa Tz tumezoea kuwa na Rais kwa vipindi viwili sasa kelele za nini kuhusu Mh. Kikwete?? Kuna nini hasa kinachofanya watu waanze kampeni sasa??
- Wakuu ufike wakati tujadili alternative, otherwise politically tunakuwa tunakubali kwamba ni CCM, au hakuna,
- Tutoe mapendekezo ya kuelekeza wananchi kwenye mabadiliko, na pia tuseme mchango wetu utakua ni nini hasa katika njia hiyo ya kuwabadilisha mawazo wananchi wapiga kura, au tujiunge na vyama vya siasa now.
Respect.
FMES!
Ndg WJC, unajua kuna kitu kinaitwa'presumption' kutokana na uhusiano na ubini wako na matendo yako yanamfanya kila mtu afikie hitimisho hilo. Hii presumption ni 'rebuttable' na wakuikanusha na kuonyesha sivyo ndivyo ni wewe pekee uliyebeba hiyo dhamana ya kukanusha hiyo 'presumption'