Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 64
Mimi nashusha mavitus tu. Hayo ya chuki na ukabila unayaleta wewe na nitawaachia wasomaji wengine wenye fikira nzuri wa-tu-judge. Wakishasoma na ku-comment then nitajibu hoja including za bibie Asha. Naipost tena hoja yangu kwa manufaa ya wasomaji.
Asha Abdala said:Mimi napingana na hilo wazo la kumpendekeza Dr. Slaa kuwa mgombea uraisi. Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya wapinzani kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;
Contradiction!
Huwezi kubadili mfumo mzima wa utawala kama hutabadili institution ya urais ambayo inateua mawaziri, wakurugenzi, mabalozi, wakuu wa wilaya nk. Hivyo wapinzani lazima walenge pia kumwondoa Kikwete 2010 na CCM.
Yes We Can. Kenya just did by being the majority in the parliament. Zimbabwe is on her way of doing the same. Uraisi is not the only way to democracy. Wapinzani have to be smart on how to achieve their objectives. They should stop inhibiting themselves by overspending on unachievable projects.
Asha Abdala said:
- Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia bungeni, mahakamani na kwa wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.
Tofauti ya kuwa na mtu mmoja mzuri inaonekana bayana ukimlinganisha Nyerere na Kikwete. Rais ana mamlaka makubwa ya utuezi na utendaji. Ukiwa na Rais msanii kama Kikwete utakuwa na Mawaziri kama Chenge, Mramba, Lowassa na wenzake lakini ukichagua Rais bora utapata safu nzuri ya uongozi
1. Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
2. miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
3. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.
Kama huna taarifa, Kenya na Zimbwabwe wapinzani walishinda vyote pamoja - bunge na uraisi. Tafuta mfano mwingine.
Asha Abdala said:3.Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Uchaguzi wa hivi karibuni Kiteto inatoa picha ya ugumu uliopo.
Unajichanganya!
Kama unasema wapinzani hawatashinda urais 2010 kwa kuwa wameshindwa Ubunge Kiteto kwanini unawashauri tena kwamba ni vyema wakagombea Ubunge? Kwanini ushiwashauri wajenge mazingira ya kushinda vyote ama kutoshiriki uchaguzi kabisa? Au unataka kuhamamisha attention yao kwa Kikwete?
Mgawanyo wa upinzani umeouna wapi wakati sasa wana ushirikiano na wamekuwa wakisimamisha mgombea mmoja katika hizi chaguzi za hivi karibuni? Kipimo chako cha mgawanyiko huo ni kipi wakati wapinzani wanashirikaina katika mambo mbalimbali?
Asha
Asha Abdala said:4.Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.
5.Uongozi mbovu ndani ya vyama vya upinzani nao ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.
Acha generalization wewe?
Uongozi mbovu upi? Wa Katibu Mkuu Dr Slaa wa CHADEMA au Mwenyekiti Lipumba wa CUF?. Wasomi na wafanyabiashara hawaachi kujiunga na upinzani kwa kuwa kuna uongozi mbovu bali ni hofu tu ya kulinda maslahi yao. Mbona Msomi Prof Baregu amejiunga CHADEMA? Au mfanyabiashara Ndesamburo mbona anafanya vizuri tu katika siasa za upinzani.
Ushabiki wa kimajimbo gani huo ulioko kwenye vyama?
Mi naona wewe kazi yako ni kupandikiza hofu tu kwa wananchi ili waogope kujiunga na upinzani.
Asha Abdala said:6.Nyerere alisema upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM, na mimi nakubaliana naye kabisaa hata baada ya kufariki. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.
Dr Slaa alitoka CCM; kama assumpition yako juu ya kauli ya Nyerere ni sahihi kwanini bado unampinga Dr Slaa kuwa hafai? Mbona wanaCCM wanahamia tu? umewaona wakina Pesha, Balozi Ngaiza etc
Karibu kila mtu aliyeenda JKT miaka ya 90s na kurudi nyuma, ilibidi awe CCM au TANU by default.
Elewa kuwa sipingi Dr. Slaa au mwingineo yeyote kugombea uraisi, ninachosema ni kuwa ni vema kwa yule mwenye nafasi ya kushinda ubunge agombee ubunge maana kushinda uraisi probabilities zake ni ndogo. Wapo wengi ambao hawana uwezekano wa kushinda ubunge lakini wana-qualify kugombea uraisi, na hao ndio ningependekeza wapewe hiyo nafasi lakini resources nyingi zipelekwe kwa wagombea ubunge.
6. Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Na hii ndio sababu kubwa ya kupinga kumuingiza Dr. Slaa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi. Uwezekano wa yeye kushinda ubunge ni mkubwa kuliko uraisi na isingekuwa vema akakosekana kwenye ulingo wa kisiasa kwa miaka 5, kama ilivyokuwa kwa Mrema, na kushindwa kufanya yale tuliyoona anaweza kuyafanya akiwa bungeni. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.
7. Upinzani wapunguze hili la ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye ubunge. Kwa mfano CHADEMA walitumia zaidi ya TShs 220millioni (30% ya pesa waliyokuwa nayo) kwenye kukodisha helicopter tu. Lakini jumla ya pesa yote walizowapa wagombea wa ubunge wao ilikuwa ni TShs. 59 millioni tu (8% tu). Kama wangewekeza zaidi kwenye wabunge labda watu kama Bob Makani wangekuwa wabunge hivi sasa.
[/list]Changamoto langu kwa vyama vya upinzani ni kuungana na kuwekeza zaidi kwenye ubunge maana kwa hali ilivyo hivi sasa, hakuna atakayemng'oa CCM in 2010.
We kweli kubwa jinga!
1. Kwani hiyo helikopta ilikuwa inafanya kampeni Kenya? Si ilikuwa inapita maeneo ya wagombea ubunge na udiwani ikiwa imembeba mgombea Urais na Mgombea ubunge wa eneo husika kupiga kampeni? Sasa maanake ni kwamba hizo milioni 200 za helikopta zimetumika pia na wagombea ubunge kwa kuwa walipanda helikopta kwenda kwa wapiga kura wao. Zitto na Mnyika si waliwahi kusema kuwa walitumia helikopta ilipokwenda kwenye majimbo yao?
2. Hebu tumia akili, hizo milioni 59 walizopewa wagombea ubunge ni zile walizopewa fedha taslimu. Hizo milioni 500 zingine hazikutumiwa na mgombea urais binafsi. Utaona humu kulikuwa na fedha za mafunzo ya wagombea ubunge, kutengeneza vifaa vya kampeni na kufanya kampeni za vyombo vya habari nk. Vyote hivi vingine vilikuwa vinatumiwa na wagombea ubunge wenyewe moja kwa moja na vingine vililenga kujenga taswira ya CHADEMA. Na ukijenga taswira ya CHADEMA unawasaidia pia wagombea ubunge katika maeneo yao.
Sasa nieleze, kati ya hizo milioni 700 CHADEMA ilizotumia kwenye kampeni zake, ni zipi ambazo Freeman Mbowe kama mgombea urais alitumia mwenyewe; ni zipi hazikutumika katika majimbo. Kwani mgombea urais alifanya kampeni zake katika sayari ya Mars? Kazi yake si ilikuwa kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea wake? Hebu acha kuwakatisha tamaa watanzania kuunga mkono upinzani.
Ni kweli ni muhimu kuweka mkazo kwenye ubunge, lakini si kwa unavyoonyesha wewe. Wewe hukosoi kwa kujenga, unabwabwaja kwa lengo la kuchafua.
Au ndio maana ya kubwa jinga? Hivi kwani nini umechagua jina hilo?
Asha
Labda and wish so. Lakini tunajua Kenya raisi bado ni Kibaki. Lakini mafanikio ya Odinga na wenzake ni kuwa hivi sasa hawana uraisi lakini bado wataongoza mijadala yote bungeni no matter what? This is what should be upinzanis target.
...... Kenya walilitambua hili na sasa wamefanikiwa kushinda.
Mimi hawa watu wanaosema eti wapinzani bado hawawezi kushikilia uraisi wananiudhi sana. Kama uraisi wenyewe unashikiliwa na watu kama Mwinyi, Mkapa, na Kikwete,...how worse can it get?
KJ said:Karibu kila mtu aliyeenda JKT miaka ya 90s na kurudi nyuma, ilibidi awe CCM au TANU by default.
Elewa kuwa sipingi Dr. Slaa au mwingineo yeyote kugombea uraisi, ninachosema ni kuwa ni vema kwa yule mwenye nafasi ya kushinda ubunge agombee ubunge maana kushinda uraisi probabilities zake ni ndogo. Wapo wengi ambao hawana uwezekano wa kushinda ubunge lakini wana-qualify kugombea uraisi, na hao ndio ningependekeza wapewe hiyo nafasi lakini resources nyingi zipelekwe kwa wagombea ubunge.
Unapendekeza mambo mengi sana mkuu, wakati at the same time ukisema kuwa wengine hawafai kugombea uraisi, au kuwa ni ndoto kwa wapinzani kushinda uraisi! unajichanganya sana, hebu soma ulichoandika kwa sauti ili uone vile unavyoweka commedy hapa ukumbini.
Mwafrika wa Kike,
Isome tena article yangu yooooteeee bila ushabiki na hapo ndio utakapoelewa vema ninachoongelea. Asha angalau anakubaliana na mimi kuwa pesa nyingi itumike kwenye ubunge na sio kurusha watu na helicopter. Shida yake ni moja tu kuwa, article yangu pia inaipiga vijembe CHADEMA, na kusahau kuwa ukilea mtoto lazima umchape na kumfokea.
Dr. Slaa ni vema akabaki kwenye ubunge ambapo ana uhakika wa kupata, kuliko kuingia kwenye uraisi na kutumia over 60% ya mtaji halafu unapata kura 10%. Huu unaitwa ukichaa au u-bishoo. Ugombea uraisi apewe mtu asiye na jimbo analoweza kushinda. Wengine wote wakazanie ubunge au hata udiwani.
Bado hujatoa sababu za kwanini Dr Slaa asigombee uraisi na kwa nini wapinzani wawaachie ccm kwenye uraisi.