The return of Sabata: Zitto is back, with a vengeance!!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,668
Reaction score
14,683
Kwa wale wenzangu na mimi, wa siku nyingi kidogo, mtaikumbuka filamu hii ya The Return of Sabata.
Sabata alionewa sana mtaani kwake na akaingia mitini, lakini aliporudi mtaani pakawa hapakaliki!

Nimeifananisha filamu hii na matukio ya hivi karibuni yaliyoibuliwa, tena kwa umahiri mkubwa na mh. Zitto Kabwe, Mbunge machachari wa kutoka Kigoma Jimbo la Kaskazini.
Zitto, mwanasiasa mchumi, vile vile ni Mwenyekiti wa PAC- Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma(Public Accounts Comittee).

Kama kawaida yake, Zitto si mtu wa kukurupuka, ni kama vile mchezaji mahiri wa mchezo wa chess.

Katika sakata zote alizoibua hivi karibuni, nyavu zake zinaelekea kukamata samaki wa kutosha, tena ma big fish wa pande zote za kisiasa na kiutendaji serikalini.

Sakata la kushindwa kukagua mahesabu ya vyama limekuwa kirungu kizito kwa vyama vyote, lakini kwa CCM na CHADEMA limewaumbua zaidi.
Makelele ya watu wa uenezi toka vyama vyote yamekuwa ya kujitetea zaidi kuliko kuonyesha usafi wao.

Hili la pili ndio kali zaidi, ufisadi wa kutorosha fedha na kuziweka nje ya nchi.
Na hili linaelekea kukamata hata tuliokuwa tunawaona kama malaika wa kisiasa.

Kwa wananchi walio wengi wanaona Zitto anafanya kazi nzuri, anaanika unafiki wa wanasiasa ambao ni mahiri kuongea majukwaani lakini vitendo vyao havifanani na wanayohubiri.
Na wanao umbuka ni wanasiasa wa pande zote vile vile na watendaji serikalini.

JK anamaliza muda wake hivi karibuni, ni vyema wananchi tukaona anavyomaliza katika masuala haya.
 
I wanna see how will this soap opera finally end?Either way i am not that fond of two-faced politicians.
 
This is why i always stand firm into my belief towards the Arusha declaration and CCM policies, sihitaji kuwa shabiki wa mtu au bendera fuata upepo, nasimama mwenyewe katika misingi ya taifa letu iliyojengwa kwa siasa safi za CCM, mwalimu wangu mmoja alishawahi kuniambia, wakati unataka kuchagua sensei mzuri, fanya uchunguzi wa haraka kwa background ya sensei wako kabla ya kujiunga na dojo yake,fahamu kwanza misingi yake, tabia yake kwa jamii, na mafunzo yake yakoje, msemo huu unasaidia kuwa makini na watu na kuwachunguza kwanza na kujitahidi kuwafahamu kabla ya kujiunga nao, si ajabu tena watu kuanza kuhama chama baada ya kusikia madudu ya viongozi wao, itakua aibu na utaonekana mtu ambaye huna msimamo, kama wewe ni kuhama hama tu na watu, si kila anayesema ANAMAANISHA, demokrasia ya kweli inaanza kwa kujitambua na kujenga misingi yako mwenyewe kabla ya kutafuta wale unaowaona mnaendana kimtazamo, na kabla ya kujiunga nao, chukua muda wa kuwafahamu kwanza, bila haya tunaweza kuwapa nchi majambazi tukabaki tunalia..
 
Zitto kazaliwa kiongozi ukipambana nae jiandae kupasuka msamba.
 
Nakubsliana mkuu.
Na ndio maana naona katika safu ya wspinzani, at least Zitto ana msimamo umaotokana na principles..
Ila awe careful maana sasa atapata maadui toka sehemu zote na si mafisadi waliomo serikalini tu.
Hatujasahau ya Wangwe
 
Ndio ume andika nini?mimi nimefikiria umekuja na maji ya hao wausika unakuja na porojo hapa JF
 
Jambo la ajabu kidogo ni kuwa Zitto kama Naibu katibu mkuu wa Chadema anatenda atendayo kwa kufuata Ideology ya chama chake sasa inakuwaje washabiki wa CCM wanamfagilia kama mtu wao? Ukiona mke anamsifia na kumtaja sana mume wa nyumba ya pili ujue kuna neno hapo
 
mtu akifanya kazi nzuri lazima apewe heshima yake, lkn muulize silaa na zito huwa wanakutania wapi km si kupishana kwenye kordo tuuuuuu??
 
Mimi najua hili la kumweka Mbowe kwenye picha lina maana pana sana .Mimi sina haraka ya kusema lolote .Nampongeza sana Zitto kwa kazi yake lakini nadhani kazi inataka kuharibiwa kwa kumchanganya Mbowe ili wezi wapate justification ya wizi .Chadema is clean and again they will this batttle like many .
 
mtu akifanya kazi nzuri lazima apewe heshima yake, lkn muulize silaa na zito huwa wanakutania wapi km si kupishana kwenye kordo tuuuuuu??

Hayo ni maneno yenu nyie na Zitto alishakanusha kwa kinywa chake kuwa utendaji wao ni wa pamoja. Hamuachi umbea? Huko kwenu hawapo wachapa kazi?
 
Jambo la ajabu kidogo ni kuwa Zitto kama Naibu katibu mkuu wa Chadema anatenda atendayo kwa kufuata Ideology ya chama chake sasa inakuwaje washabiki wa CCM wanamfagilia kama mtu wao? Ukiona mke anamsifia na kumtaja sana mume wa nyumba ya pili ujue kuna neno hapo

Inawezekana jirani anamhujumu jirani yake. Hii inashangaza kidogo. Mashabiki wengi wa Zitto wanatoka chama tawala. Mmh!
 
Jambo la ajabu kidogo ni kuwa Zitto kama Naibu katibu mkuu wa Chadema anatenda atendayo kwa kufuata Ideology ya chama chake sasa inakuwaje washabiki wa CCM wanamfagilia kama mtu wao? Ukiona mke anamsifia na kumtaja sana mume wa nyumba ya pili ujue kuna neno hapo
Zitto hakuonyesha unafiki wa siasa.
Amelima pande zote zinazohusika na ufisadi, au ulitaka amsifie Mbowe na kumpongeza kujenga nyumba Dubai?
Hili bandiko lako linakuumbua kuwa umnafiki, sasa kama mnaulea ufisadi mnakimbilia kuchukua nchi ili mjilimbikizie mali?
 
Hayo ni maneno yenu nyie na Zitto alishakanusha kwa kinywa chake kuwa utendaji wao ni wa pamoja. Hamuachi umbea? Huko kwenu hawapo wachapa kazi?

Nyie ndo mnajichanganya hata msijue upinzani ni nini!
Kwa hiyo hebu tupe mwongozo , akiiba Slaa na Mbowe si wizi, wizi ni pale anapoiba Rostam na Ngeleja tu!?
 
Zitto hakuonyesha unafiki wa siasa.
Amelima pande zote zinazohusika na ufisadi, au ulitaka amsifie Mbowe na kumpongeza kujenga nyumba Dubai?
Hili bandiko lako linakuumbua kuwa umnafiki, sasa kama mnaulea ufisadi mnakimbilia kuchukua nchi ili mjilimbikizie mali?
Sikiliza,mie sijasema kuhusu nyumba Dubai. Nimezungumzia mtiririko wa muda mrefu humu jukwaani kuonekana kama Zitto yeye sio kiongozi wa Chadema bali anawakilisha kundi lingine na washabiki wake wanapatikana CCM na wao ni kama kiongozi wao kunani? Mwenye akili lazima apate mashaka.
 
This is why i always stand firm into my belief towards the Arusha declaration and CCM policies, sihitaji kuwa shabiki wa mtu au bendera fuata upepo, nasimama mwenyewe katika misingi ya taifa letu iliyojengwa kwa siasa safi za CCM, mwalimu wangu mmoja alishawahi kuniambia, wakati unataka kuchagua sensei mzuri, fanya uchunguzi wa haraka kwa background ya sensei wako kabla ya kujiunga na dojo yake,fahamu kwanza misingi yake, tabia yake kwa jamii, na mafunzo yake yakoje, msemo huu unasaidia kuwa makini na watu na kuwachunguza kwanza na kujitahidi kuwafahamu kabla ya kujiunga nao, si ajabu tena watu kuanza kuhama chama baada ya kusikia madudu ya viongozi wao, itakua aibu na utaonekana mtu ambaye huna msimamo, kama wewe ni kuhama hama tu na watu, si kila anayesema ANAMAANISHA, demokrasia ya kweli inaanza kwa kujitambua na kujenga misingi yako mwenyewe kabla ya kutafuta wale unaowaona mnaendana kimtazamo, na kabla ya kujiunga nao, chukua muda wa kuwafahamu kwanza, bila haya tunaweza kuwapa nchi majambazi tukabaki tunalia..
Huu ndo unafiki sasa...currently mbona unakumbatia majambazi na chama ambacho hata criticism tu hakivumillii.Huna msimamo mkuu..despite the fact that unataka watu wakuamini hivyo.The Arusha Declaration is dead in the water!....and you know it...lakini bado eti unalisimamia(chini ya mwamvuli wa ccm)...Kama unaamini juu ya misingi ya Azimio la Arusha na bado ni kada wa ccm...ww ni mnafiki.
 
This is why i always stand firm into my belief towards the Arusha declaration and CCM policies, sihitaji kuwa shabiki wa mtu au bendera fuata upepo, nasimama mwenyewe katika misingi ya taifa letu iliyojengwa kwa siasa safi za CCM, mwalimu wangu mmoja alishawahi kuniambia, wakati unataka kuchagua sensei mzuri, fanya uchunguzi wa haraka kwa background ya sensei wako kabla ya kujiunga na dojo yake,fahamu kwanza misingi yake, tabia yake kwa jamii, na mafunzo yake yakoje, msemo huu unasaidia kuwa makini na watu na kuwachunguza kwanza na kujitahidi kuwafahamu kabla ya kujiunga nao, si ajabu tena watu kuanza kuhama chama baada ya kusikia madudu ya viongozi wao, itakua aibu na utaonekana mtu ambaye huna msimamo, kama wewe ni kuhama hama tu na watu, si kila anayesema ANAMAANISHA, demokrasia ya kweli inaanza kwa kujitambua na kujenga misingi yako mwenyewe kabla ya kutafuta wale unaowaona mnaendana kimtazamo, na kabla ya kujiunga nao, chukua muda wa kuwafahamu kwanza, bila haya tunaweza kuwapa nchi majambazi tukabaki tunalia..
Hicho ndicho kilichonihamisha CCM! Wamaiasi misingi ya Azimio la Arusha na kukumbatia rushwa, wizi wa mali ya uma, ufisadi, kutorosha na kumilikisha rasilimali za wazawa kwa wageni, kukosa usawa, kuendesha nchi bila kuzingatia miiko ya uongozi, na kubadilika kuwa chama cha wafanya biashara na mabepari huku kikiwa mikononi mwa mafisadi! Vipaumbele vyake vilihama kutoka kupambana na maadui watatu yaani umasikini, ujinga na maradhi na sasa wanatuletea sera walizokopo na kupesti kutoka nje kama Big result now! Hakuna ubunifu tena. Tofauti na wewe hata baada ya kuona kuwa wamevunja misingi ya Azimio, bado umo humo. Mgonjwa huyu hana dalili za kupona!
 
Jambo la ajabu kidogo ni kuwa Zitto kama Naibu katibu mkuu wa Chadema anatenda atendayo kwa kufuata Ideology ya chama chake sasa inakuwaje washabiki wa CCM wanamfagilia kama mtu wao? Ukiona mke anamsifia na kumtaja sana mume wa nyumba ya pili ujue kuna neno hapo

Watu wa CCM wakimsifia mpinzani ujue kafanya jambo lenye maslahi kwao.. Zitto amekuwa mtatanishi sana Chadema ikiwa chafu yeye anakuwaje msafi..
 
Hicho ndicho kilichonihamisha CCM! Wamaiasi misingi ya Azimio la Arusha na kukumbatia rushwa, wizi wa mali ya uma, ufisadi, kutorosha na kumilikisha rasilimali za wazawa kwa wageni, kukosa usawa, kuendesha nchi bila kuzingatia miiko ya uongozi, na kubadilika kuwa chama cha wafanya biashara na mabepari huku kikiwa mikononi mwa mafisadi! Vipaumbele vyake vilihama kutoka kupambana na maadui watatu yaani umasikini, ujinga na maradhi na sasa wanatuletea sera walizokopo na kupesti kutoka nje kama Big result now! Hakuna ubunifu tena. Tofauti na wewe hata baada ya kuona kuwa wamevunja misingi ya Azimio, bado umo humo. Mgonjwa huyu hana dalili za kupona!

Ulikoenda sasa umeipata nafuu au ni chengachenga kama kawaida?
 
Watu wa CCM wakimsifia mpinzani ujue kafanya jambo lenye maslahi kwao.. Zitto amekuwa mtatanishi sana Chadema ikiwa chafu yeye anakuwaje msafi..

Chadema ikijichafua yeye anasimama na utaifa wake. Hakuna lengine ila zitto anapendwa na watanzania wa ccm na cdm na hata vyama vyengine kwakuongoza maslahi ya taifa mbele na sio mwenye kuendesha siasa za kichamachama.
 
Back
Top Bottom