The readings I read...vitabu nilivyosoma mwaka 2021

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070
Mwaka 2021, ambao tunaelekea kuimba ule wimbo maarufu wa “Auld Lang Syne, ambao umetumia maneno ya Kiingereza cha Kiskochi, ukimaanisha ‘For The Sake of Old Days,’ ikiwa ni ishara ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mwingine (au kusheherekea kukamilisha/kumaliza jambo), nimefanikiwa kufanya mwendelezo wa vitabu kadhaa ambavyo sikuvimaliza mwaka wa jana, nikajitahidi kusoma vitabu vingine vipya na majarida ya kimataifa hususan kuhusu masuala ya uchaguzi, demokrasia katika muktadha tofauti tofauti na pia kurejea kusoma baadhi ya vitabu ambavyo nimewahi kuvisoma huko nyuma.

Jambo la muhimu na kujivunia zaidi ni kufanikiwa kupata walau muda ‘kiduchu’ wa kuendelea kufanyia kazi, kuandika kitabu changu pia, kazi niliyoianza likizo ya mwisho wa mwaka 2019, ambacho nimekipatia jina la “Die or Survive, Make or Break, Crash or Win; A Year That Was. Kusema kweli, kila muda unavyopita, tangu nilivyoanza kufikiria na kisha kukata shauri kuandika hiki kitabu, mambo yanayotokea katika maisha ya kila siku, kijamii, kikazi na kitaaluma, yamekuwa yakisadifu sana jina la kitabu hiki, ambalo kwa uhakika lilitokana na ushawishi wa mwanazuoni nguli, Noam Chomsky, kwenye kitabu chake “Hegemony or Survival; America’s Quest for Global Dominance”.

Idadi ya ‘readings’ ambazo nimefanikiwa kuzisoma kwa mwaka huu, ni matokeo ya msukumo wa masuala kadhaa, iwapo naweza kuyataja machache kwa haraka kwa minajili ya kutochosha au kuchusha mada. Kuna masuala ya mapito/mapitio mbalimbali ya maisha ya kila siku; kuna uzoefu wa masuala anuai kikazi/kitaaluma, kuna mambo ya kisiasa, kuna maamuzi madogo na muhimu (wengine huita maamuzi makubwa) katika kuamua mstakabala wa mambo mengi ya wakati ujao baada ya kujifunza jana na leo.

Kuna ‘readings’ nimesoma (iwe ni mpya, kufanya mwendelezo au kurejea) kwa sababu ya msukumo au ushawishi fulani wa kutaka kuelewa zaidi muktadha wa mambo yanayotuzunguka au kutukabili (kisiasa, kiuchumi na kijamii), kuongeza mwanga wa ufahamu, kubadili mtazamo wa namna ya kuyaona mambo, kuongeza maarifa na taarifa, bila kusahau kutanua wigo wa fikra ili kuvielewa vitu ‘katikati ya mistari’ au kumuona shetani ambaye hufichwa kwenye maneno yasiyosemwa moja kwa moja. Halikadhalika kuongeza ujuzi na utaalam. Bila kusahau ‘soul searching’, ile hali ya kujitafuta wewe, wa leo, kesho, keshokutwa, mtondo na mtondogoo kwa kutumia 5W&H.

Jambo muhimu hapa ni kwamba, kujitahidi kuwa na MALENGO katika kusoma. Si kusoma tu kufunua karatasi ili kumaliza aya, kurasa au sura za vitabu au machapisho.

Katikati ya mikikimikiki ya mwaka jana, nilikuwa nasoma vitabu kadhaa, kikiwemo kitabu cha Rais Mstaafu wa Marekani, Billy Clinton, kinaitwa, My Life, nikitaka kuelewa mambo makubwa matatu, dhahama za maamuzi kadhaa yaliyofeli katika utawala wake, hususan huko Somalia, dhahama ya skandali yake na mdada mrembo, Monica Lewinsky, lakini kubwa zaidi ni response ya Hillary Clinton katikati ya wakati mgumu, wa majaribu makubwa, kama ule na namna alivyoandika kitabu kuhusu maisha yake kwa ujumla. Nimefanikiwa kukimaliza mwaka huu.

Vitabu vingine nilivyokuwa naendelea navyo tangu mwaka wa jana ni; Where Power Lies: Prime Ministers V the Media (Lance Price), Political Communication in Britain: the Leader Debates, the Campaign and the Media in the 2010 General Elections (Dominic Wring, Roger Mortimore & Simon Atkinson).

Biblia Takatifu na Seize The Day (Dietrich Bonhoeffer), vitabu hivi viwili ni chakula cha kila siku. Biblia ni kitabu cha majira yote na nyakati zote.

Mnamo Aprili mwaka huu, kutokana na masuala kadhaa yaliyokuwa yakiendelea, nilipata hamu kubwa ya kurejea tena kuwasoma mojawapo ya wanazuoni nguli, Profesa Issa Shivji (Let the People Speak; Tanzania Down the Road to Neo-Liberalism) na Profesa Ali Mazrui (The African Condition: A Political Diagnosis – The Reith Lectures 1979). Nilikuwa najaribu kuweka muktadha au kujenga taswira ya “The Tanzanian Condition: A Political Diagnosis.” Kwamba iwapo ungelikuwa daktari wa binadamu na ukaletewa Tanzania kwenye kitanda chako cha kupima na kutibu, ungebaini nini na ungechukua hatua gani? Kwa masikitiko, pamoja na jitihada kubwa, sijafanikiwa kukipata tena kitabu cha Prof. Shivji hadi muda huu. Bila shaka nitakamilisha jambo hili mwaka ujao mapema.

Vitabu vingine nilivyorejea ni pamoja na The Young Guns – A New Generation of Conservative Leaders (Paul Ryan, Eric Cantor & Kevin McCarthy), Che Guevara; The Revolutionary Life: Revised and Updated (Jon Lee Anderson), The State of Africa: A History of the Continent Since Independence (Martin Meredith), Animal Farm (George Orwell), My Hope for Tomorrow (Ruby Dhal), Nyuma ya Pazia (Dkt. Wilbroad Slaa).

Pamoja na changamoto kadhaa, nikafanikiwa kuanza na kumaliza kusoma ‘readings’ mpya: Ujamaa ni Imani: Azimio la Arusha, The Story of the American Coup in Guatemala (Stephen Schlesinger; Stephen Kaizer), Social Market Economy’ as Europe’s Social Model? (Christian Joerges & Florian Rodl), Men Are From Mars, Women Are From Venus (John Gray), Life of Muhammad (Hadrat Mirza Bashiruddin Mahmud Ahmad), Encyclopedia of Espionage, Intelligence and Security Vol III (Lee Lerner and Brenda Lerner), The Real Politics of the Horn of Africa: Money, War and Business of Power (Alex De Waal), African Heroes (Jim Haskins), Miseducation of the Negros (Carter Godwin), How to https://jamii.app/JFUserGuide Woman’s Brain Out (Thorn Daddy);

Hujuma na Kivuli (Elvis Musiba), Fixing Failed States: A Framework for Rebuilding A Fractured World (Ashrat Ghani, Clare Lockhart) na Africa’s International Relations: The Diplomacy of Dependency and Change (Ali Mazrui), pia Journal of Democracy; April 2021, Vol. 32, Issue 2 na October 2021, Vol 32, Issue 4, Reflections on the 2000 US Presidential Election, The Rally – Intensive Campaign: A Distinct Form of Electioneering in Sub-Saharan Africa and Beyond (Dan Paget) na MWONGOZO wa Chama wa Mwaka 1981.

Jumla ya readings kwa mwaka 2021 ni 29, zikihusisha vitabu na majarida.

Malengo ya mwaka ujao ni pamoja na; kuboresha zaidi utamaduni wa kusoma vitabu, hasa katika kupata muda na kufanya ‘contextualization au localization’, pia kuboresha kawaida ya kusoma/kujisomea mapema alfajiri, magazeti na makala za uchambuzi wa masuala ya kitaifa na kimataifa (zenye sifa za kuwa makala za uchambuzi).

Kuongeza kasi ya kusoma, kujifunza na kuielewa Biblia Takatifu kila siku na kuona namna ya kuweza kusoma Quran, kuongeza idadi ya vitabu na majarida ya uchambuzi wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, kitaifa na kimataifa, kurejesha kasi ya kusoma kazi za watunzi wa vitabu vya riwaya wa hapa nyumbani. Kizazi cha akina Kezilahabi, Mtobwa, Kabwe Makenika/Jitu Kumbuka, Musiba hadi kizazi hiki cha akina Fadhy Mtanga, Hussein Tuwa na wengine.

Nimepanga kuanza na readings zifuatazo kadri itakavyowezekana; Bi. Ubwa (Zuhura Yunus, Venus Nyota), Tawasif ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tawasifu ya ‘Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu’, My Life My Purpose cha Hayati Benjamin Mkapa.

Makene, Tumaini
 


 
Die or Survive, Make or Break, Crash or Win

Linaonekana ni jina zuri.

Nikirejea kwenye vitabu ulivyo some naomba pdf ya fixing failed states na pdf ya Hujuma na Kivuli
 
Die or Survive, Make or Break, Crash or Win...
Naweza kujaribu kukutumia PDF ya Fixing Failed States. Hiyo ninayo. Ni kati ya vitabu vilivyonilazimisha kusoma soft copies. Sipendelei sana na kimsingi zinanipatia ugumu kiasi fulani.

Napenda hard copies sana. Nikishindwa hapa muda huu naweza kukutumia mapema asubuhi. Unipatie njia ya kukutumia sasa.

Hujuma na Kivuli nina hard copies. Sijui nakusaidiaje!
 
Die or Survive, Make or Break, Crash or Win

Linaonekana ni jina zuri.

Nikirejea kwenye vitabu ulivyo some naomba pdf ya fixing failed states na pdf ya Hujuma na Kivuli

Asante kwa compliment kuhusu jina la kitabu ninachoandika;

Die or Survive, Make or Break, Crash or Win: The Year That Was
 
Makene Hongera Sana. Wewe ni Moja ya vijana wenye upeo mkubwa na uwezo wa kupambana mambo. Toka ukiwa Chuo Kikuu (UDSM) Shule ya Uandishi na Mawasiliano nimekuwa mmoja ya wanaokuelewa. Kila la heri katika Uandishi wa kitabu.
 
na MWONGOZO wa Chama wa Mwaka 1981.

Jumla ya readings kwa mwaka 2021 ni 29, zikihusisha vitabu na majarida.

Makene, Tumaini
Mkuu Tumaini Makene , kwanza hongera sana kusoma vitabu hivyo na karibu tena jukwaani maana uliadumika.

Kwa sababu wewe ni mtu mkubwa kule ulikokuwa na humu ni alwatan na mtu maarufu, unapobadili makazi, unatujulisha rasmi na sio tusikie kwa kusikia sikia, jee ni kweli umehama mtaa ule na sasa umehamia mtaani kwetu?.

Tunaisubiri kwa hamu "Die or Survive, Make or Break, Crash or Win; A Year That Was"
Sisi wengine ni ma kiritiki kwa lengo la kuboresha. The Title is too long. Kwanza ondoa "a year that was", twende na "Die or Survive, Crash or Win"

My take ni hicho kitabu ni kizuri na kitauza sana kwasababu usiange amua ulicho amua, kule unge die but now you survive, kule hata ungepanda vipi, mwisho wa siku unge crash tuu, ila huku sasa uta win!. Kitafute kitabu kiitwacho "The Winning Coalitions" ukicheza na timu za washindi una wini.
Ukilipitia bandiko langu hili
Sasa utakubaliana na mimi I was right.
Welcome to home sweet home.
P
 
Mkuu Tumaini Makene , kwanza hongera sana kusoma vitabu hivyo na karibu tena jukwaani maana uliadumika.

Kwa sababu wewe ni mtu mkubwa kule ulikokuwa na humu ni alwatan na mtu maarufu, unapobadili makazi, unatujulisha rasmi na sio tusikie kwa kusikia sikia, jee ni kweli umehama mtaa ule na sasa umehamia mtaani kwetu?...
Bwana Pascal ni kama umesoma mawazo yangu. Naunga mkono hakuna sababu ua Long title. Die or survive Inatosha na inavutia sana.
 
Sidhani kama wamemfukuza bali ni yeye mwenyewe amefungua macho na kuona ukweli wa alipo na anakwenda wapi, akafanya uamuzi sahihi.
p
Asante Pascal. Naomba uje utuletee uchambuzi nini hatma ya Chadema endapo Mbowe ataishia jela.

Maana kiukweli tumeona Chadema haina direction bila uwepo wa Mbowe.
 
Kuna kitabu namalizia kuandika kinahusu jinsi biashara ya kununua Wanasiasa wa upinzani ilivyofanyika awamu iliopita. Polical prostitution in Tanzania jina la kitabu

Hongera sana. Kila la heri. Nitajialika kuwa mmojawapo wa wahariri ! Sijui nitasaidia kitu hapo with experiences from the field
 
Back
Top Bottom