Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
Niliachwa ghafla bila kuambiwa sababu ya kuachwa. Nilijitahidi ku let go...... ilinisumbua kwa muda mrefu sana ingawa sikuendelea kubembeleza. Akili yangu iligoma kukubaliana na hali halisi kwa kutoelezwa what went wrong.... hadi mahusiano yakavunjwa
.....hapo juu mwanajamiiOne ametoa mfano, "nimepata mwingine zaidi yako!"....
Je? Wewe binafsi ungeweza kubali SABABU kama hiyo? Utajikubalisha 'you are 2nd best...'au hujakidhi viwango na vigezo baada ya miezi, miaka kadhaa pamoja?
...hiyo ndiyo "the power of letting go!...." Ile hali ya kwa upole na unyenyekevu unakubaliana na mwenza wako MUACHANE kwa kheri, bila shari wala shaka yoyote, kwani kwa hali hiyo pekee ndipo nae (bila hasira, jazba wala matusi) atakwambia 'sehemu' ya sababu au sababu 'zote' kwanini ameamua kusitisha mahusiano.
...ulipitia hatua hizo?