The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

kinachowakost man city ni sajili mbovo, Huwezi kutoka kwenye KDB, Bernando, Mahrez, Gundogan halafu ukaishia kwa Anderson, forden, Doku, semenyo Dah inasikitisha sana
 
Mtaenddelea kuponea tundu la sindano mpaka lini?

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Mtu amecheza anavyoweza yeye, ndio jinsi alivyopanga karata zake, namna ya kushida. Wewe unasema ameponea kwenye tundu la sindano, je amepata point zake alizofuata? Na nini kilikuwa kinatakiwa kwani?
Ndio stail yake ya kucheza ... Eti wewe unaumia..... Achana na City mkuu huiwezi
 
kinachowakost man city ni sajili mbovo, Huwezi kutoka kwenye KDB, Bernando, Mahrez, Gundogan halafu ukaishia kwa Anderson, forden, Doku, semenyo Dah inasikitisha sana
Wachambuzi wa Bongo bana dah.....

Mzee umeanza kuchambua matokeo kabla mpira haujachezwa. Jana unasema Anderson, Semenyo na wengine ni sajili mbovu, wakati Man City leo ndiyo wanaanza ligi. Hata hawajapewa muda wa kuonyesha uwezo wao. Uchambuzi wa mpira sio kutaja majina ya KDB, Bernardo, Mahrez na Gündogan halafu moja kwa moja ukahukumu vizazi vipya. Subiri wacheze kwanza ndio tupime usajili.
 
GOAL! Guehi gets his head on the ball and puts it into the net! Man City 1-1 Bournemouth

hao jamaa wengi wao hawajaja leo, anguko la City limeanza misimu miatatu iliopita, na sababu kuu ni replacement za wachezaji waliopo mwanzo zinashindwa kuwa na standard kama za watangulizi wao.
 
hao jamaa wengi wao hawajaja leo, anguko la City limeanza misimu miatatu iliopita, na sababu kuu ni replacement za wachezaji waliopo mwanzo zinashindwa kuwa na standard kama za watangulizi wao.
Hapo ndipo sikubaliani na wewe. Ukisema anguko la City lilianza misimu mitatu iliyopita,
2022/23
City ilishinda UEFA Champions League kwa mara ya kwanza, Premier League na FA Cup — TREBLE.

2023/24.
City ilishinda Premier League kwa mara ya 4 mfululizo na points 91. Gündogan na Mahrez walikuwa tayari wameondoka, lakini City bado wakachukua title.

David Silva alipoondoka tuliambiwa pia City itashuka kwa sababu hakuna atakayefikia standard yake. Lakini De Bruyne akaendelea kuwa engine ya creativity ya City. Na De Bruyne hakuhitaji kuwa David Silva mwingine ili City iendelee kushinda.

Vivyo hivyo Fernandinho alipoondoka, Rodri ndiye aliyekuja kuchukua nafasi yake. Lakini Rodri hakuhitaji kuwa Fernandinho mwingine, alikuja na style yake mwenyewe, akawa mmoja wa viungo bora duniani na akashinda Ballon d’Or. Na Rodri ndiye aliyefunga goli la ushindi kwenye Champions League final ya 2023, akasaidia City kukamilisha Treble.
 
DOGO acha mihemko, Rodri alikuja kama upgrade ya Fernandinho na sio replacement. Wakati Silva KDB tayari alikuwa kwenye Top of his game.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…