The Lioni Tamer

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,303
1,559
jamaa mmoja alikuwa anataka kuwa Lion Tamer (mchezo fulani wa kucheza na simba kwenye maonyeso)
rafiki yake akamuuliza,
basi ilikuwa hivi
rafiki: je simba akiangusha ile stuli ndefu wanayopanda utafanyaje?
jamaa: si nitadandia kamba
rafiki: na kamba ikikatika
jamaa: nitamchapa na mjeledi
rafiki: na aking'ata huo mjeledi
jamaa: nitampiga na ile fimbo ndefu
rafiki: na akiing'ata hiyo fimbo ndefu
jamaa: nitachukua ile bastola na kumpga risasi
rafiki: na kama risasi ikimkosa
jamaa: nitachukua mavi na kumpiga nayo usoni
rafiki: na kama kutakuwa hakuna hayo mavi je?
jamaa: sasa kama simba ameangusha stuli, kamba ikakatika, akang'ata mjeledi, akang'ata fimbo, na risasi imemkosa
we unafikiri kutakosekana mavi kwenye suruali yangu kweli!
 
Hahaha! kweli hapo mavi lazima yawepo na ni silaha tosha kwakuwa Simba atashanagaa harufu na kumpa jamaa nafasi ya kukimbia.
 
Aaaaaaaaaaaahhhahahahahahahahahahahhahaha
aaaaaaaaaahahahahahahahahah
mbavu na masihara ..................................
 
Umenikumbusha yule mwanariadha aliyepewa siri ya kushinda mashindano ya marathonina mwalimu wake;
aliambiwa kuwa risasi ya kuanza mashindano itakaposikika ajaribu ku-imagine kama anakimbizwa na simba.
Basi risasi iliposikika, jamaa akaanza kujinyea...
 
ha ha ha, teh hii kali
 
teh teh...
 
nyinyi bana.........wacha tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom