The Legacy of Kingunge Ngombare Mwiru

Ule ugonjwa wa kupukutika meno yote mdomoni unautwaje? Nasikia ati huyu babu hahitaji tena mswaki, ya kwake huwa anayasafisha "in vitro" (wameniambia madaktari kuwa hii inamaanisha "nje ya mwili") kwenye beseni lenye JIK. Ingawa nakusudia sentensi iliyotangulia iwe utani, ung'ang'anizi wa babu Kingunge kwenye siasa za bongo ni mfano mbaya sana na ni jambo la kukemewa kabisa, hasa ushirika wake na mafisadi siku hizi.
 
kila jambo linamipaka si kwa vile ni kiongozi lazima wasifu binafsi wake wa ndani na nje ujadiliwe unakua unaelekea ktk umbeya.

Na mtu ukitaka kujadili wasifu binafsi wa mtu kwa swali hilohilo unalotaka kumuuliza anza kujiuliza kwanza wewe mwenyewe swali hilo hilo na ukipata jibu lake kutoka kwako mwenyewe ndipo nenda hatua nyingine zaidi kuhoji ndg yako.


mkuu hii ni mada nzuri sana kama ukiiangalia kwa undani! Tulia ajadiliwe inawezekana amefanya mambo makubwa ndo maana ni mshauri wa rais au unakitu unaficha hapa jamani tuwajadili wotetumeanza na yeye then ufuate kina malechele na wengine ili kabla hajafa ajue watanzania watamuongeleaje akindoka, hii pia itasaidia walioko madarakani waanze kutengeneza cv zao mapema! Hapa tutajadili tutatengeneza wasifu wake ajue nini kitaongelewa! Nakushukuru sana mleta mada
 
natamani kujua elimu yake kabla hatujamhukumu. ana upeo mdogo sana huyu mzee.. he is senile
 
Kiongozi anayeshikilia nafasi ya juu kabisa kwa unafiki tangu enzi ya mwalimu; hakuna msimamo wowote anayaliowahi kuisimamia. Yeye kwenye kila jambo anaangalia upepo unakoendelea na yeye huko ndiko aendako.

Nathani japo kwa Jijini Dar "Kinje" atakuwa na legacy yake kuliko huyu mzee. Kwani legacy lazima iwe positive..!!!
Duuh,
 
Najiuliza hivi historia ya Tanzania itaandika nini kuhusu mchango wa Kingunge katika Taifa letu ukiondoa jina hilo la "Kingunge" ambalo limebakia kuwa alama ya mtu ambaye ni kigogo na kiongozi mkubwa? Ni nini hasa mchango wa Kingunge katika siasa, uchumi, na maisha ya Tanzania? Ni kitu gani tunaweza kusema kuwa kisingefanyika kama Kingunge asingekuwepo? Je historia itaandika nini juu ya Kingunge au atabakia na alama ya nyota tu katika footnote ya historia?
kwa kushirikiana naye unaweza kuandika kitabu ,au tumuombe ghasanny atuandikie historia ya mzee kingunge
 
Back
Top Bottom