Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Najiuliza hivi historia ya Tanzania itaandika nini kuhusu mchango wa Kingunge katika Taifa letu ukiondoa jina hilo la "Kingunge" ambalo limebakia kuwa alama ya mtu ambaye ni kigogo na kiongozi mkubwa? Ni nini hasa mchango wa Kingunge katika siasa, uchumi, na maisha ya Tanzania? Ni kitu gani tunaweza kusema kuwa kisingefanyika kama Kingunge asingekuwepo? Je historia itaandika nini juu ya Kingunge au atabakia na alama ya nyota tu katika footnote ya historia?