The internet is undefeated: A painful lesson

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,232
113,610
I hope this was a teachable moment.

From it, they will grow through what they went through and do better going forward.

They say if you know better, you do better.

So I’m crossing my fingers that they will publicly acknowledge the error of their ways and promise us to do better and use some common sense in the future. Common sense goes a long way.

And honesty is always the best policy. Just tell people the truth. You don’t have to tell every single solitary detail. Just the basics would suffice.

Ilisikitisha kuona serikali ikishindana na tetesi za mtandaoni ambazo hatimaye zimekuja kudhihirika zilikuwa za kweli.

Watu wa Mtandaoni ambao kimsingi ndo waliokuwa wanatupatia taarifa za hali ya marehemu Rais Magufuli [hata kama kila detail haikuwa sahihi], wamejiongezea heshima ya kuaminika na watu ilhali serikali ikipoteza uaminifu.

Serikali ijayo ya Mama Samia [and I’m rooting for her badly] ina kazi kubwa ya kuirejesha imani hiyo iliyoshuka.

Hivi kwa mfano miezi michache tokea sasa zikitokea tetesi zingine kuhusu jambo nyeti nchini halafu kambi ya akina Kigogo na wenzake wakinzane na upande wa serikali katika kilichotokea au kinachoendelea, unadhani ni nani wananchi wataomwona ndo anasema ukweli?

Serikali ya Tanzania inabidi ibadilike iendane na zama hizi za kidijitali. Haiwezekani tena kuficha ficha mambo halafu mambo hayo yasijipenyeze kwenye umma. Yatapenya tu.

Njia za watu kuwasiliana zipo nyingi mno na ni rahisi sana.

Ni vyema kama kuna jambo linaendelea na ambalo lina maslahi kitaifa, serikali ikawa ndo ya kwanza kulitolea neno jambo hilo ili kuepusha sintofahamu zisizo na ulazima.

Hakukuwa na ugumu wowote ule kwa serikali kusema kuwa Rais Magufuli ni mgonjwa, yuko wapi, na maendeleo ya hali yake ikoje.

Hayo yangefanyika awali na mapema, basi hata waziri mkuu Majaliwa asingekuwa contradicted na Mama Samia siku chache zilizopita.

Badala yake tumeona watu wakinyanyaswa kisa tu wanahabarishana kuhusu kilichomsibu Rais wao, ambaye, mind you, alipata 84% za kura kwenye uchaguzi uliopita!

Waachane na hayo mambo ya kipuuzi yanayozidi kuwapunguzia heshima.

Time to put some respect on the information superhighway’s name.

It is undefeated for a reason.
 
Serikali lazima ijifunze kutoa habari mapema na bila chenga zozote.

Sera ya Ukweli na uwazi za Marehemu Mkapa ziliishia wapi?

Wanaotoa habari za siri wanatoka humo humo serikalini, na wengine ni wale waliokula kiapo cha kutunza siri vifuani.

Bora kutoa habari rasmi, uaminike kuliko kuficha ficha halafu uumbuliwe.
 
Serikali lazima ijifunze kutoa habari mapema na bila chenga zozote.
Sera ya Ukweli na uwazi za Marehemu Mkapa ziliishia wapi?
Wanaotoa habara za siri wanatoka humo humo serikalini.
Bora kutoa habari rasmi , uaminike kuliko kuficha ficha halafu uumbuliwe
Tulijenga mfumo mbovu sn wa kumuogopa mtu badala ya kusimama na nchi yetu
 
Wajifunze kuwa smart, taratibu za kikatiba zisiyumbishwe na maneno ya watu mtandaoni , walichokuwa wanaficha kuhusu Hali ya Afya ya Raisi ni nini sasa, hata kilichomuua raisi nafkri ni Ile Nia ya kuwaoutclass wanaompinga kwamba Aumwe kimya kimya apone kimya kimya atokee kukanusha tetesi hvyo watu wamshangilie , na imegharimu uhai wa Raisi, so sad Kwa kweli.

Mtu kaumw , kazidiwa pandisha ndege peleka hospital za kibabe duniani huko akafe mikononi mwa madaktari bingwa au apone. Kujifungia fungia ndani hamna kitu aisee kisa unaogopa watakucheka sababu ya misimamo yako aaaah
 
Serikali lazima ijifunze kutoa habari mapema na bila chenga zozote.
Sera ya Ukweli na uwazi za Marehemu Mkapa ziliishia wapi?
Oh yeah! Leakers wamo humo humo serikalini.

Hizi ni zama tofauti sana.

Kuficha ficha mambo ambayo yanajumuisha watu wengi ni vigumu sana.

Taarifa zitapenya tu.

Si ajabu ukakuta waliokuwa wanavujisha hizo taarifa ni hao walinzi wa rais.
 
Aisee...!

Nyie watu wa Lumumba mu wagumu sana kujifunza na kujua kuwa ujinga haulipi badala yake ni tego na chanzo cha mauti yenu tu...

Haya endeleeni hivyo hivyo, tutakuwa tunawazika mmoja baada ya mwingine ili mkajifunze kuwa wakweli huko ahera...
Tatizo wanapuuza ukweli kuwa tayari wamekufa watu wengi sana Dodoma, tena wa Ikulu, kwa sababu ya kushabikia ujinga wa kutomwambia mkuu kweli!
 
Ndugu huyu mtu hakufa jana wala juzi...

Huyu mtu hakufia kwenye kituo cha afya cha Mzena...

Huyu mtu kama tetesi zilivyokuwa zina trend kuwa aliugua wiki kadhaa huko nyuma, akapelekwa Nairobi Kenya usiku kwa usiku na baadaye India, ndivyo ilivyokuwa na huu ndiyo UKWELI unaofichwa...

Huyu mtu kafa siku nyingi zilizopita. Laiti wangekuwa na uwezo wa kukaa na maiti miaka mitano, wangekaa nayo hawa...

Lakini hili ni gumu, haliwezekani. Tulisema, MFICHA MARADHI, MAUTI HUMUUMBUA. Ndivyo ambavyo imekuwa...

Hili ni tatizo kubwa na haieleweki lengo la kuficha wananchi taarifa hizi inakuwa ni nini tu...
 
Kwa mantiki hiyohiyo, wajifunze kuwa kutunga sheria za kuminya uhuru wa habari na kuwekeana sheria za maudhui ni jambo futile. Jambo ambalo wakilikazania wataishia kujenga uhasama na kupotezeana wakati na mali.

Tuwe na Glasnost yetu, hatukutakiwa kufanya makosa ya wenzetu, tulitakiwa tu kusoma historia ya USSR lakini naona si wanafunzi wazuri.
 
Kinachoisumbua Tanganyika Mr Nyani Ngabu ni u communist uchwara . Tunaiga vya kina North Korea . Ni aibu hawa hawa waliokuwa wanatuambia Rais yuko salama anachapa kazi. Eti ndiyo wanaoenda kutuongoza ?!. Shame
Halafu walikuwa wanadai eti wameongea naye?

Hivi alikuwa kwenye hali ya kuweza kuongea na watu kweli au walikuwa wanatudanganya tu?
 
Nchi iliyodai imeishinda Korona, na sasa Korona inaenda kuua Safu yote ya uongozi wa juu wa nchi , naskia viongozi wa juu ambao hawaonekani onekani wapo Hoi vitandani .... Ifikie hatua waache ushamba , Taifa linakuwa kituko na mithali Kwa walimwengu
 
mzee wa spana
Leo nimepumzika nyumbani najisikia amani sijawahi kuipata kwa muda sana
Kayafa kafa!Shangazi mimi nina furaha ya ajabu,kwa mara ya kwanza leo nimejikuta napiga Komoni baada ya Bia,Konyagi na K-vant kushindwa kufua dafu!Kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yangu furahaa imeninyima usingizi,leo usiku kucha sijaweza kulala.Nilikuwa macho kodo!
 
Back
Top Bottom