The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

Salute
Mnamo mwaka wa 4BC jijini Galilaya katika kitongoji kiitwacho Nazareth kulikuwa na familia ya Bw. Joseph na mkewe Maria; walipata mtoto wa kiume wakamwita Jina Yeheshua au Yesu.

Ilikua ni moja ya kaya ya kimaskini, Bw. Joseph alikua anajishughulisha na shughuli za uchakataji wa mbao yaani useremala pia mkewe Bi. Maria alikuwa anajihusisha na shughuli ndogo ndogo za mikono. Yesu alifundishwa kusoma na kuandika tu maana wazazi wake hawakuweza kumudu gharama za kumpeleka shule zaidi, lakini alisoma pia masomo ya dini kwa walimu wa kiebrania waitwao “Rabi”. Kijana huyu alikuwa akisaidiana na baba yake kufanya shughuli za uchakataji mbao.

Alipotimiza miaka 30 kijana huyu ndio nyota yake ya mafanikio ilipoanza kung’aa, alianza kazi zake za kufundisha watu kama “Rabi” mambo mbalimbali yahusiyo falsafa ya maisha. Alifundisha kwa muda wa miaka mitatu tu, so alipokua na miaka 33 alifariki dunia kwa kuwambwa msalabani na dola ya Rumi iliyokua inatawala nchi nyingi kipindi hicho.

Kosa lake lilikua ni uhaini kwa kujiita mfalme wakati nchi hiyo ilikuwa ina mtawala ambaye ni Herode na Gavana Pilato wakiwa chini ya mtawala Kaisari Tiberius, pia kuweka maandamano yasiyo na kibali.

Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe. Japo kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hapo zamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini kijana mdogo sana ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watuwote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.

Kaacha miongozo ambayo ilikuja kutengeneza taasisi kubwa yenye nguvu na washirika wengi ambayo ni Catholics. Inaonyesha watu wengi mashuhuri duniani wamepita kwenye taasisi hii au ni wafuasi wa mafundisho ya huyu kijana mdogo. Yeye ndiyo binaadamu zaidi maarufu ulimwenguni. Kaacha historia ambayo haiwezi vunjwa maisha yote maana jina lake limeshindwa kufutika. Hebu fikiria kama alifanya mambo yake kwa muda wa miaka 33 tu ila umaarufu wake unazidi kukua na wafuasi wanazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Wakuu mimi kiukweli namuonea sana wivu huyu kijana, haiwezekani kwa muda wa miaka 20+ niliyoishi hapa duniani sijawahi kufanyiwa Happy birthday, sidhani kama kuna mtu mwingine tofauti na mama anayekumbuka siku yangu ya kuzaliwa. Lakini kijana mdogo aliyekufa miaka mingi sana iliyopita karibia dunia nzima wanajua siku ya kuzaliwa kwake na hua wanasherhekea nyumbani huwa wanapika wali kabisa na kuchinja yule mbuzi mnene tuliemchunga muda mrefu halafu mimi first born kwenye kumbukumbu yangu ya kuzaliwa sijawahi pewa hata andazi.

Kinachoniumiza zaidi najua siku nikifa tu watu watanisahau mara tu baada ya kutandua msiba wangu, sitakumbukwa na yoyote kama yesu tunavyomkumbuka labda nyie wa huku JF mtanikumbuka kwa posts zangu.

Kiukweli mimi sikubali, kwanini Yesu atushinde watu wote wakati alikuwa binadamu sawa kama sisi? Tunakosea wapi? Kweli tumeshindwa kuvunja rekodi zake nasi basi tukumbukwe hata kwa muda wa miaka 10? Lakini je, huyu kijana mdogo alifanyaje hadi akaweza kufanya mambo makubwa yote haya ndani ya muda mdogo?

Maneno yote huko juu ni kuonyesha jinsi huyu kijana alivyoweza fanaya mambo mengi ndani ya muda mchache lakini kubwa la msingi ni kujua je aliwezaje? Alitumia nini?

Yesu aliwezaje?

Ukichunguza utajua kabisa huyu mtu alikuwa ana vitu anafanya ili kutimiza mipango yake hiyo yenye matokeo makubwa. Yesu alitumia vitu vitatu ili kufanya yote hayo. Kwanza kabisa alikua anajtambua (nilishaliongelea hili), pili alikuwa anafahamu kusudi lake (nitaliongelea hili panapo majaliwa) tatu alijali muda kuliko kitu chochote. Yes! Hapa ndiyo kwenye kiini cha mada yetu; Time Management. Jinsi nidhamu nzuri ya matumizi ya muda inaweza kukuletea mafanikio makubwa.

Japo Yesu hakuwa na elimu kubwa lakini alijitambua na alitambua kusudi lake mapema mno ndiyo maana alitumia muda wake vizuri sana akaweza kufanya mambo mengi makubwa. Alithamini muda wake alifanya kazi yake kwa nidhamu ya hali ya juu muda ukiwa ndio silaha yake kuu.

Kuna mtu aliwahi muuliza The Godfather Mwl. Julius Nyerere kwamba anawezaje kufanya mambo mengi kama vile kuhudhuria vikao, kuwa na familia yake, kuandika vitabu na makala kwenye magazeti, kuongoza nchi, kufanya ziara n.k kwa wakati mmoja? Nyerere alisema yeye anaheshimu muda. Muda wa kula anakula tu, muda wa kikako anakua kikaoni, kutembea anatembea tu, muda wa kulala analala tu n.k n.k

Najua humu wengi wetu hili ni ngumu sana. Unakuta mtu yupo anatembea kwenda mahali fulani lakini muda huohuo anasimama kuchat, muda wa kulala yeye anasoma kitabu, muda wa kusoma yeye anakula, muda wa kula ndiyo kwanza anaanza kuongea na simu, muda wa kazi yeye anaingia JF, muda wa kutafuta watoto yeye anapiga stori na mwenzi wake.

In short, muda hatuuthamini hasa huku kwetu Afrika, ndiyo maana Wachina wanatuendesha sana na tunaona kuwa wanatunyayasa huko makazini maana wao wamekulia kwenye malezi ya kufanya kitu kutokana na muda unaruhusu kufanya nini, sasa ile silka yao wakiileta huku twaona hawa watu wapo kama mashetani.

Kijana amka jali muda wako ulionao. Kwani nyie wenzangu hamumuonei wivu huyo jamaa huko juu aliyefanya mambo mengi ndani ya muda mfupi? Moja kati ya utajiri mkubwa binaadamu alionao ni muda.

Kama umefanikiwa kuwa na leo basi wewe ni tajiri mkubwa, leo hii ndio muda wako amka ukafanye yale unayotamani kufanya. Usisubiri kesho, kesho haipo siku zote ipo leo tu! Achana na kupoteza muda wako kwa kwenda location kupiga picha za kupost Facebook upate like 300, unadhani siku ukifa kuna mtu atakukumbuka kwa kuacha picha zenye like nyingi na quality nzuri huko FB? Sahau hili.

Yesu alijitambua mapema ndiyo maana aliweza fanya mambo makubwa, jitambue kijana mwenzangu hautakumbukwa kwa kuweza kutaja kikosi kizima kinachocheza ligi daraja la tatu huko Italy au England. Tumia muda wako huu ulionao leo kwa kufanya mambo yatakayoacha alama isiyofutika hapa duniani.

Huyo ndio Yesu the Greatest man, hakuna mtu mwingine kama yeye, hakuna atakayeweza kuvunja rekodi zake alizoacha sana tunaweza fuata matendo yake ili kufanya mambo makubwa kwenye maisha ila kumpita tuache legacy kubwa kuliko yeye haitawezekana kamwe.

Tujali muda jamani, ipo siku tutajutia huu muda tuanaopoteza kufuatilia mwanamke mmoja miezi sita halafu kila siku unatumia zaidi ya masaa 4 kuwasiliana nae wakati muda huo ungefanya mambo mengi ya msingi ndani ya miezi hiyo 6 yakamfanya huyo mwanamke akajileta mwenyewe.

Utajiri wetu mkubwa sisi watoto wa maskini ambao tunaweza kuutumia kupunguza kiwango cha umaskini kwenye familia zetu kama Yesu alivyofanya kwenye familia yetu ni MUDA. Jali muda utakutunza uzeeni.

JE WEWE BINAFSI NI NANI UNAONA NI GREATEST MAN ALIYEFANYA VITU VIKUBWA AMBAE TWAWEZA KUJIFUNZA KUPITIA YEYE?
Ahsanteni.
Like & Share

Da’Vinci
El maestro.
Umepoteza muda mwingi kuandika fact ya kutisha huku ukificha mambo muhimu kwenye mada yako, Yesu alikufa na siku ya Tatu alifuduka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiamini yanayosemwa huku unaweza kukuta huyo ni zito kabwe
Mleta mada unasema umri wako ni miaka 20 kama ni kweli basi Mungu atakuwa amekujalia kipawa fulani. Ninachojua vijana wengi wa umri Kama wako wamejikita kwenye mambo ya kipuuzi tu . Mambo yasiyowasadia hata kidogo. Wengi wao wako kwenye vibanda wakibenti mechi za ligi za Ulaya.

Wengi wao hawana uwezo wa kusoma hata makala fupi yenye aya 10 kumi tu.

Wengi wao wake kwa waume wanashinda wakitazama thamthlia za Korea na India bila hata kuelewa maudhui ya senema hizo.

Katika umri huu mdogo ulio nao nani kakufundisha maarifa haya yote?

Nani kakupa hii hekima?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudia kusoma,rudia tena,
Uongo mtupu ulioandika Maria na Joseph hawakuwa Kaya maskini.

Wote walikuwa ukoo wa kifalme .Ukoo wa Mfalme Daudi..Kasome mathayo sura ya kwanza.Koo za kifalme hazijawahi kuwa Kaya maskini miaka hiyo Hadi Leo hii

Maselemala Sio watu maskini.Nenda keko dar es salaam kaangalie maselemala waliopo pale Wana magari ya mamilioni nyumba za uhakika na huuza funiture zao Hadi nje ya nchi.Aliyekuambia selemala ni mtu maskini Ni Nani?

Hata Yesu alizaliwa kwenye Holi la ng"ombe Sio sababu familia ya Joseph walikuwa Kaya maskini Bali sababu nyumba ya wageni ilikuwa imejaa.Pesa za kulipia walikuwa nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukute huyo ni msabato mkuu. Hata kuelewa
Yesu hajawahi kuwamaskini Kama mnavyomchora kwenye picha akitembea pekupeku Akiwa Hana viatu .Yesu hajawahi tembea bila viatu alikuwa na viatu Tena vya kufunga na kamba.

Alipoenda kwa yohana mbatizaji alikuwa kavaa viatu vya uhakika kiasi kuwa yohana mbatizaji akasema sistahili haya kulegeza gidamu za viatu vyake

Yesu alikuwa na mhasibu wake wa pesa zake binafsi Yuda Iskariote.Na alikuwa akiiba Lakini Yesu hakushtuka alivyokuwa nazo nyingi

Utamwitaje kuwa alikuwa maskini Wakati alikuwa Hadi na mhasibu wapagani nyie? Mimi Ni mfuasi wa Yesu tajiri Hilo pepo lenu mnaloita Yesu maskini bakini nalo wenyewe.

Yesu hakuwahi kuwa maskini na hakuzaliwa familia maskini .Hilo pepo Yesu maskini mnaloabudu nyie bakini nalo wenyewe
 
Yesu alkuwa anapata kipato kupitia miradi ipi hadi awe na muhasibu wake?
 
Yesu alkuwa anapata kipato kupitia miradi ipi hadi awe na muhasibu wake?
Alikuwa selemala maarufu na aliachisha watu wenye kazi zao Mathayo alikuwa ofisa forodha mkubwa wa TRA Kama tuliyonsyo Leo,,Luka alikuwa Daktari,Petro alikuwa mvuvi maarufu nk

Alipowaambia waache kazi zap wamfuate walimhoji sisi tumeacha vyote tukakufuata tutalipwa Nini? Yesu Tajiri Bwana wangu ninayemfuata Akawambia nitawalipa Mara Mia kuliko mlichokuwa mnalipwa hapa Duniani hapa hapa mlipo na Baadaye Uzima wa milele

Wakasema sawa na Hakuna aliyeacha kazi kwa Yesu Ina maana walichokitaka walilipwa bila ubabaishaji.

Ndio maana Yesu aliweka mhasibu Yuda Iskariote Afanye kazi hizo za kushughulikiwa mapato na matumizi Yake ya pesa zake binafsi ikiwemo kulipa mishahara ya mitume

Kazi ya uselemala ilikuwa inalipa hasaaaa na aliirthi kwa baba Yake mlezi tajiri Yusufu
 
Aisee

So stupid ani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu ni Mungu na Mungu hawezi kuwa maskini

Utajiri wa familia yake Ni kuwa Siku ya kuzaliwa hoteli ilikuwa imejaa pesa walikuwa nayo hivyo hawakuwa maskini.Maskini gani Ana pesa ya kulipia hoteli?

Familia yake ilikuwa na hadhi ya Hali ya just ndio maana hata zawadi mamajusi walizopeleka walipeleka dhahabu .

Herode alipotaka kumuua Yesu familia yake waliondoka kwenda nje ya nchi misri.Walikuwa watu wa kimataifa wenye uwezo mkubwa Pesa ilikuwepo ya kuishi nje ya nchi kwa kipindi kirefu .Wangekuwa maskini uwezo wa kwenda nje ya nchi na gharama za kuishi huko wasingeweza
Leta ushahidi Kama yesu ni mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta ushahidi Kama yesu ni mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Haikuhusu wimbo wa Taifa unaimba Mungu ibariki Afrika anayeabudu chura Kama Mungu akiimba Mungu ibariki Afrika anaamaanisha Mungu wake chura na anaimba kwa hamasa,mwingine akiimba Mungu ibariki Afrika anaabudu babu yake marehemu anaimba kwa hamasa akimaanisha babu yake Anayeamini Ni Mungu Abariki Afrika,Mwingine anaabudu nyoka chatu Kama Mungu akiuimba wimbo wa Taifa anaamaanisha Mungu wake chatu Abariki Afrika,mwingine anaabudu Allah akiimba Mungu Ibariki Afrika anaamaanisha Mungu Chatu na hatakiwi kuthibitisha kuwa huyo mungu ni Mungu kweli

Swali dogo wewe huwa unaimba wimbo wa Taifa au hajawahi imba? Popote toka uzaliwe?

Vipi wimbo wa Taifa ulishawahi imba popote
 
Alikuwa selemala maarufu na aliachisha watu wenye kazi zao Mathayo alikuwa ofisa forodha mkubwa wa TRA Kama tuliyonsyo Leo,,Luka alikuwa Daktari,Petro alikuwa mvuvi maarufu nk

Alipowaambia waache kazi zap wamfuate walimhoji sisi tumeacha vyote tukakufuata tutalipwa Nini? Yesu Tajiri Bwana wangu ninayemfuata Akawambia nitawalipa Mara Mia kuliko mlichokuwa mnalipwa hapa Duniani hapa hapa mlipo na Baadaye Uzima wa milele

Wakasema sawa na Hakuna aliyeacha kazi kwa Yesu Ina maana walichokitaka walilipwa bila ubabaishaji.

Ndio maana Yesu aliweka mhasibu Yuda Iskariote Afanye kazi hizo za kushughulikiwa mapato na matumizi Yake ya pesa zake binafsi ikiwemo kulipa mishahara ya mitume

Kazi ya uselemala ilikuwa inalipa hasaaaa na aliirthi kwa baba Yake mlezi tajiri Yusufu
Wewe ni mgonjwa mkuu jikague
 
Tusaidie kurani inasema vitabu vilivyotelemshwa Kuna torati,zaburi ,injili na kurani.

Kurani tunaiona.Hivyo vitabu Vingine viko wapi? Waislamu tuonyesheni
Mkuu torati ilikuwa kipindi Cha Nabii mussa na Zaburi ilikuwa kipindi Cha Nabii Daud, Sasa Kama unataka kuviona hivyo vitabu Rudi nyuma kipindi Cha Nabii mussa na Nabii Daud utaviona mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da'Vinci,
Mkuu samahani naomba ufafanuzi kidogo juu ya elimu ya dini nasikia yesu mama ake bikra maria na huyu mama akuwahu guswa na mwanaume yoyote!sasa hapa inaonekana maria mumewe ni joseph na mtoto wao ni yesu ilikuakuaje hapa kwa hawa wanandoa .samahani mie sio mwandishi mzuri utanirekebisha
Mkuu umenifikirisha hapo, "Maria alikuwa bikra lakini ana mume "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom