The girl from Oslo. Series kali ya kijasusi na kigaidi

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Kama wewe ni Mpenzi wa Series za Kijasusi na Kigaidi, utakubaliana na mimi kwamba Series ya The Girl From Oslo ni moja ya Series kali sana. Inagusa nyanja ya Kijasusi, kiintelijensia na Kigaidi.

Storyline
Wakati wakiwa Vacation katika jangwa la Sinai lililopo kwenye Mpaka wa nchi ya Misri na Israel, Msichana kwa jina la PIA na Wenzake 2 wote raia wa Israel walitekwa na magaidi wa ISLAMIC STATE OF IRAQ AND SYRIA (ISIS). Kundi hili la ISIS linajulikana kwa kuwa na misimamo mikali ya dini ya Kiislamu huku likiwa na historia ya ukatili wa kuwachinja mateka mbele ya kamera.

Matakwa ya Magaidi
Baada ya kufanikiwa kuwateka raia hao wa Israel, Kundi la ISIS linaweka madai yake kwa mara ya kwanza. Wanataka kuachiwa kwa wapiganaji wake 12 walioko kwenye Magereza za Norway na Israel kabla hawajawachinja raia hao waliotekwa na kundi hilo.

MWISHO

Jamani naomba kwa mwenye link ambayo itaniwezesha kupakua Epsode zote 10 za Series hii basi aweke hapa ili kila mwenye uhitaji aweze kuipata. Shukrani sana.
 
Back
Top Bottom