Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,077
Kama inavyofahamika, karibia makundi yote ya kigaidi Duniani huanzishwa na husaidiwa na Iran.
Siku chache zilizopita, kundi la kigaidi la Houthi, ambalo hufanya maangamizi zaidi huko Yemen, na ambalo hivi karibuni limewahi kurusha makombora kwenda Israel, lilieleza kuwa litaanza kuteka meli zote zenye bendera ya Israel na zile zinazomilikiwa na mataifa yanayoiunga mkono Israel.
Kundi hili Houthi limeiteka meli ya Galaxy Leader iliyokuwa safarini toka Uturuki kuelekea India. Haikuwa na muisrael hata mmoja, wala haimilikiwi na Israel, bali kuna muisrael mmoja tu mwenye hisa kwenye kampuni inayomiliki meli hiyo.
Meli ilikuwa na watu 22 ambao wanatoka mataifa ya Ukraine, Mexico, Philippines na Bulgaria. Magaidi wanasema watawashikilia mateka kwa kadiri ya miongozo ya dini ya kiislam!!
Israel imesema kuwa utekaji huo uliofanywa na kundi la Houthi, umeratibiwa na Iran, na kuongeza kuwa hali hii itaathiri biashara nzima ya usafiri wa meli.
Iran imesema kuwa kutokana na yanayoendelea Gaza, hakuna uwezekano wa kuzuia kusambaa kwa vita.
Marekani imesema inawasiliana na mataifa mengine kupitia UN ili kuamua hatua za kuchukua, lakini imelitaka kundi hilo la kigaidi kuiachia meli hiyo na mateka wote, mara moja.
Watanzania tujiandae kwa janga jingine tena la kupanda bei bidhaa. Haya magaidi yatafanya upatikanaji wa bidhaa uanze kuwa wa shida maana makampuni mengi ya meli yatasitisha shughuli za usafirishaji au kulazimika kupita mbali kabisa kukwepa bahari inayokaribia maeneo ya mashariki ya kati ambako magaidi haya yameweka mizizi yao.
Lakini haya magaidi hayana simile, yanaweza kuteka hata vyombo vingine vya usafiri, hata usafiri wa abiria kama ndege.
Hapo mashariki ya kati ni hatari kubwa kwa ysalama wa dunia.