Nimekumbuka fundisho nililopata nikiwa shule.
Siku ya kwanza kuingia darasani, nilikutana nae. Alikua anakaa desk la tatu toka nyuma yangu. Nilijikuta namchukia tu. Sijui ndio kutopatana kwa damu zetu!!!!!
Aligundua kua namchukia. Sina hakika kama alijua kutokana na jinsi nilivyokua namtazama akiniongelesha ama jinsi nilivyomjibu maswali yake.
Mimi nilifahamu kua alijua kama namchukia baada ya kuniuliza direct "Kwanini unanichukia?"
To be honest, nilishituka kupata swali nisilotegemea, ukizingatia mwenyewe nilidhani nimefanikiwa kuficha chuki yangu ndani ya moyo wangu.
Sikumjibu though niliendelea kujiuliza swali lile lile ndani ya moyo wangu kila nilipomkumbuka akiniuliza swali lile kwa sauti ya kirafiki.
Nilipata jibu. Kutokana na muonekano wake, nilimtafsiri kua ni kijana asiye jiheshimu na mambo ya starehe aliyapa kipaumbele. Sikuwahi kumpa hili jibu though aliendelea kuja kwenye desk langu kuniuliza the same question kila alipopata muda huo.
Swali hili likazaa urafiki baina yetu. He was my best friend... a very good one. Hakuwa yule niliyemdhania.
Namtakia baraka tele katika maisha yake and he will always be my best friend ndani ya moyo wangu.
DONT JUDGE A BOOK BY ITS COVER WAJAMENI.