Mamushka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2010
- 1,595
- 99
Kama unakiwanja anza kujenga, hiyo pesa itakapoishia utapumzika uvute nguvu kidogo uanze tena. Lakini ukitaka ushauri wa watu wengi mwishowe watakukatisha tamaa, watakupigia mahesabu ya juu mpaka hiyo pesa utaitumia, uchungu wa kujenga utauhisi unapoanza, na raha yake ni pale inapokua imenyanyuka kidogo, hata pesa ikiisha utafanya juu chini ili umalizie. Kila la kheri mkuu nijambo jema sana umeamua.